Jee nitaweza kushuhudia watanzania wengi wakila milo 3 katika uhai wangu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jee nitaweza kushuhudia watanzania wengi wakila milo 3 katika uhai wangu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sijali, Oct 6, 2012.

 1. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,062
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Nimekaa hapa katika moja ya nchi tajiri zaidi duniani tukiandaa mlo na wanangu. Kila siku, kipindi cha mlo hunipa wakati mgumu sana. Wakati watoto wangu wakiwa na uhuru wa kuchagua, tule kuku, farasi, ng'ombe,kondoo, kunde na maharage n.k., najua 80% ya Watanzania wenzangu hawana hiari hiyo. Kinachouma zaidi ni kuwa kila nikitazama kila pembe ya nchi hii, sioni kitu gani hasa wanacho kuishinda nchi yangu- yaani katika vitu vya kuonekana. Labda vitu visivyoonekana, akili, uzalendo, kuweka malengo, juhudi.....n.k ????!!!!
  Ndipo najiuliza: jee, katika hivi vitu ambavyo kwa wazi wametuzidi na ndio maana wakatimiza mahitajio yao ya kibinadamu, lini sisi tutakuwa navyo? Katika umri wa miaka 42 nilio nao, lini itawezekana kusema 80% ya Watanzania watakuwa wanaweza angalau, si kuchagua, bali kula milo mitatu kwa siku? Ni miaka 20 ijayo nitakapokuwa na umri wa miaka 62? Ningependa kujua ili niingojee kwa hamu siku hiyo na niache kuumia moyo kila wakati saa ya kula inapowadia!
   
Loading...