Je, ni kweli fasihi simulizi ni mali wa jamii nzima?

I Ching

Member
Mar 20, 2017
24
12
Habari za muda huu, natumai nyote wazima poleni na majukumu ya kujenga taifa.

Moja kwa moja Kwenye Mada: Wakati nasoma o-level nakumbukia kwenye Kiswahili tuliambiwa kwamba FASIHI SIMULIZI NI MALI YA JAMII NZIMA tofauti na fasihi andishi ambayo ni mali ya watu maalum ( wanaojua kusoma tuu ).

Sasa tatizo langu linakuja hapa hivi watu wenye ulemavu wa usikivu (VIZIWI) nao pia wanajumuishwa katika fasihi simulizi maana wao hawasikii ( nao pia ni sehemu ya jamii), na fasihi simulizi sifa yake ni kwamba inatumia mdomo kufikisha ujumbe kwa jamii ( jamii hii wanatumia ishara kuwasiliana).

Naombeni niekwe sawa kwenye hili jambo langu wajuzi wa mambo, ahsanteni na siku njema.
 
Katika fasihi simulizi kuna matendo na mijongeo ya mwili mfano katika uwasilishaji wa fanani tuzingatie na hilo.Kama msimuliaji akizungumzia ulimaji anaweza kuambatanisha na matendo ya mwili (mikono).

Na pia nikupongeze kwa hili kwani katika kuisoma fasihi sijawahi kuona kundi kama hili (watu wenyewe ulemavu kama wa kusikia) likizingatiwa ingekuwa jambo zuri ikafanyiwa tafiti jambo hili kama ilivyo fasihi ya watoto.
 
Back
Top Bottom