Jee mwisho wa Shamhuna wawadia?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,191
672
jamani huyu bwana kule kwao wamemkataa kumpitisha kwenye NEC huku ofisini kila kukicha migogoro na anategemewa kugombea nafasi ya urais zanzibar. jee huku ndio mwisho wake umefika au kuna nn?



Shamuhuna ameshindwa kazi - ZFA

2007-12-29 08:41:11
By Mwandishi Wetu


Chama cha soka cha Zanzibar (ZFA) kinataka Naibu Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi, Juma Ali Shamuhuna apokonywe kushughulikia masuala ya michezo kutokana na kushindwa kufanya kazi yake.

Shamuhuna pamoja na kuwa Waziri Kiongozi, pia anashughulikia masuala ya Habari na Utamaduni.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Shirikisho la soka nchini (TFF), Msemaji wa ZFA, Maulid Hamad Maulid alisema chama chake kinataka Shamuhuna amuombe Rais Amani Karume wa Zanzibar amwachishe kushughulikia masuala hayo.

Hamad alisema chama hicho kinataka kuona sasa masuala ya michezo yanarudishwa Wizara ya Elimu.

Alisema ZFA imefikia hatua hiyo kutokana na mwenendo wa siku za karibuni wa Shamuhuna wa kuingia katika mvutano na chama hicho bila ya sababu za msingi.

Hamad aliyeamua kufunga safari kuja Dar es Salaam badala ya kuzungumza na waandishi walioko Zanzibar, alimtuhumu Shamuhuna kwa kuzuia gazeti la kila siku la serikali la Zanzibar Leo kutoa taarifa za chama hicho.

Pia alishutumu kitendo chake cha kuamua kupokonya chama hicho Uwanja wa Mao Tse Tung wakati walipewa na Waziri aliyekuwa anasimamia michezo kabla yake, Haroun Suleiman.

Hamad alidai pia Shamuhuna amekuwa katika siku za karibuni akitoa vitisho dhidi ya viongozi wa chama hicho kudai kuwa hawatapewa ushirikiano kutokana na kutotekeleza matakwa yake.

Pia msuguano umekuwepo zaidi baada ya Shamuhuna kutangaza serikali ilikuwa tayari kuandaa mashindano ya Kombe la Chalenji mwaka 2009 lakini Makamu Mwenyekiti wa ZFA, Haji Ameir akasema isingewezekana kutokana na michuano hiyo kufanyika nchini Kenya.

Hata hivyo, Maulid amedai chuki za Shamuhuna dhidi ya ZFA zinatokana na watu wake kutochaguliwa katika uongozi wa chama hicho kwenye uchaguzi uliopita.


SOURCE: Nipashe
 
Hili ni Zengwe na jamaa ataondoka ampishe mtoto wa Mwinyi . CCM bwana wakikukamia utajua tu .Kaisha huyu .
 
Shamhuna ni opportunist ambae originally kamabi yak ilikuwa pamoja na Komando Salmini waliposhindwa azma yao aya kubadili ktk ili komando aendelee na pia kupigwa mweleka kwa Bilal Shamhuna akandandia gari la Karume kwa mbele akidhani anawatosa wenzie kumbe anajitosa mwenyewe.

Haya ndio matatizo ya kupanda farasi wawili soon atapasuka msamba....
 
Huyu mkuu alikuwa swahiba wa Muungwana, na ni mmoja wa waliotumika sana na Mkapa, kumpiga vita Salim na Malecela ndani ya kamati kuu, the matter of fact kama sio ujeuri wa Mkapa, Muungwana alitaka betweeen huyu Shamuhuna, Khatibu, au Meghji, mmojawapo awe veep badala ya Shein,

Hata hicho cheo chake huko Visiwani, kilikuwa created maalum kwa ajili yake kutokana na a compromise deal kati ya Muungwana na Karume, lakini recently kama kawaida ya siasa, ametokea kuwa on the otherside ya Muungwana, kwenye kikao kimoja cha cc Muungwana alimmuabisha sana kwa kumsema wazi kuwa anatumia muda mwingi kufanya kampeni za urais badala ya kazi aliyompa, na kwamba asipoacha atamnyanga'anya kingora cha polisi,

Since then, imekuwa ni free fall kisiasa kwake, na calling a spade behind his misery sasa ni no body but Salmin na Dr. Bilali!
 
Back
Top Bottom