Jee mfumo wa Ujamaa na kujitegemea ni sahihi kwa Tanzania???? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jee mfumo wa Ujamaa na kujitegemea ni sahihi kwa Tanzania????

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mathcom, Oct 20, 2012.

 1. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Wana jamii na wasomi waliobobea katika mambo ya siasa naomba tuujadili japo kwa ufupi huu mfumo wa "ujamaa na kujitegemea" ambao tunaambiwa na wanasiasa wetu na hata kuambiwa (kama si kufundishwa) mashuleni kwamba ndio unaofuatwa nchini Tanzania. Jee lengo la mfumo huu limefanikiwa kweli, na kwa ufanisi huo (kama upo) jee bado ni mfumo bora wa kuendelea kuwa nao nchini Tanzania??

  Mimi mtazamo wangu nahisi wengi waliopata bahati ya kushika nafasi za juu serikalini au hata secta binafsi, wameacha kifungu cha kwanza na kuchagua cha pili yaani "kujitegemea" nikiwa na maana ya kwamba kila mtu kwa nafasi yake anajikusanyia mali kadri iwavyo ili aweze kujitegemea ama akiwa kazini na hata baada ya kustaafu, hili la "Ujamaa" nahisi kama halipo kabisaaa labda miongoni mwa masikini na fukara wao kwa wao!!

  Naombeni mawazo mbadala au kwa muono wenu wajumbe,
  ahsanteni!
   
 2. l

  luhombi Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  tanzania haifuati mfumo wa ujamaa na kujitegemea kama nadharia ya uongozi wa nchi kwa sasa. ujamaa ni falsafa ya kiuongozi inayojikita katika kuleta uwiano sawa wa kipato kutokana na nguvu ya uzalishaji mali illiyotumiwa na watu. kwa kawaida rasilimali zote za nchi huwa chini ya watu wote,zikisimamiwa na serikali.

  iko migawanyiko au aina tofauti tofauti za ujamaa kwa mfano, ujamaa wa china ni tofauti na ule wa urusi ya zamani au wa africa. kwa tanzania ujamaa ulitangazwa rasmi mwaka 1965 ila utekelezwaji wake ulianza rasmi mwaka 1967 baada ya azimio la arusha. wanafalsafa wengi wa mfumo huu kama carl marx, lenin,mao,stalin na leon trotisky wanaamini kua ili ujamaa ufanikiwe ni lazima nchi husika iwe imepitia mfumo wa kibepari kwanza kwa kua ujamaa ndio hatua ya mwisho ya maendeleo ya binadam
  kwa mtizamo wangu ujamaa ulianguka africa kwa sababu uliruka baadhi ya hatua za kiukuaji. ni kama mtoto anayetamani kutembea kabla hajatambaa
   
 3. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  wewe umeona ujamaa wengine wameona mfuo Kristu,wengine mfumo islam,wengine bepari.Na wengine hawaoni kabisa mfumo wakueleweka.

  Hembu ulizana na watu ni upi upo halafu ndipo swali liendelee.
   
Loading...