Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,669
- 119,297
Wanabodi,
Hili ni swali tuu, "Jee Kuna Uwezekano Viongozi Wetu Tunawaheshimu kwa Machoni Tuu Lakini Moyoni Tunawadharau?.
Nikimaanisha inawezekana heshima tunayoionyesha kwa viongozi wetu sio genuine bali ni superficial tuu kutokana na nidhamu ya woga kwa kuwaogopa kufuatia nguvu ya kimamlaka waliyo nayo, lakini sio respect toka ndani na mioyoni mwetu?. Yaani tunawaheshimu machoni tuu lakini mioyoni tunawadharau?!.
Swali hili limefuatia mazungumzo yangu na baadhi ya watu wengi huku mitaani madongo kuporomoka, wanawazungumzia vibaya baadhi ya viongozi wetu wa wakuu katika hali inayoashiria kuwa wanawadharau sana, sasa nilipokutana na mchango wa mwana JF mmoja ambao ni mmoja wa GT wachache wa ukweli humu JF, akichangia uzi fulani humu, amesema maneno mazito kwenye mchango wake ambayo yamenigusa na kupelekea kuwiwa kupandisha bandiko hili.
Hoja ya msingi ya mwanajf huyu ni kuhusu heshima, yaani "respect is earned and not forced!". Yaani heshima ni kitu kunachopatikana kwa kustahili na sio kulamisha.
Hivyo kufuatia tabia binafsi za baadhi ya viongozi wetu, inawezekana kabisa watu wanawaheshimu kwa heshima za uongo za machoni tuu lakini moyoni mwao wanawadharau?, yaani respect iliyopo ni nidhamu ya woga tuu? .
Kujiheshimu huku kwa kiongozi ni lazima uongee kwa heshima na unyenyekevu, ukiongea lazima uonyeshe respect kwa kuwaheshimu wale unaoongea nao, wale unaowaongoza, na kuonyesha heshima kwa watu wote, wakubwa na wadogo, watu wa chama chako na wapinzani, watu wanaokupenda na hata wasio kupenda, wewe ni kiongozi wa wote, timiza wajibu wako na majukumu yako ya kiuongozi kwa weledi wa hali ya juu huku ukiheshimu katiba na ukifuata sheria, taratibu na kanuni.
Ukionyesha dharau, majigambo, kujisikia wewe ndio wewe, wewe ndio kila kitu hadi watu kukudhania unajidhania wewe ndio kama Alfa na Omega, watu watakeheshimu machoni tuu kwa sababu ya mamlaka yako lakini mioyoni mwao wanakudharau na kukuona ni mtu wa hovyo, mtu wa majisifu, mtu wa kujisikia, mtu wa kujiona wewe ndio wewe, sifa ambazo sio njema kwa mtumushi wa watu.
Kiongozi mzuri ni yule anayejiheshimu yeye na anayeheshimu watu anaowaongoza. Kama ni kiongozi wa kuchaguliwa, Rais, Mbunge, Diwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, hawa ni viongozi wa watu, lakini ni watumishi wa watu waliochaguliwa na watu ili wawaongoze, hivyo kwao watu muhimu kabisa ni wale waliowachagua. Kiongozi ukiishachaguliwa usijione wewe ndio wewe, kwa sababu uligombea wewe na ukashinda hivyo unajisikia ulishinda kwa nguvu zako! ,no way, huwezi kushinda kwa nguvu zako hata uwe ni bilionea kumpita Bill Gates, umeshinda kwa kura za waliokuchagua hivyo waheshimu hawa ili heshima hiyo ikurudie na wewe. Jihesabu huo uongozi wako sio malí yako bali ni malí ya waliokuchagua.
Kama ni kiongozi wa kuteuliwa, heshima mamlaka yako ya uteuzi ila heshimu pía wale unaowaongoza kwa kujihesabu kuwa cheo chako ni dhamana tuu kwa ajili ya hao unao waongoza. Hivyo waheshimu subjects wako ili nao wakugeshimu.
Namalizia kwa kukumbushia swali la msingi, jee tunawaheshimu viongozi wetu kwa dhati au tunawaheshimu kwa uoga tuu?.
Na kwenu viongozi, naomba mjitafakari, mnayoyafanya, mnayo yatenda, mnayo yasema, mjiulize, jee yana command respect?, heshima mnayoipata, inatokana na nyinyi kuistahili heshima hiyo? , do you earning such respect or night heshima tuu ya mamlaka?. Please badilikeni!, True respect is earned and not forced! .
Paskali

Mkuu Nguruvi 3, kwanza naunga mkono hoja, respect is earned and not forced, ili kiongozi uweze kuheshimika, lazima kwanza wewe mwenyewe ujiheshimu, na kuwaheshimu wengine ili ile heshima ikurudie na wewe! .Kuna kitu kinaitwa 'mutual respect' ikimaanisha kwa kiswahili kuheshimiana
Rais Obama alikuwa anatumia maneno haya ''Treat people the way you want to be treated'
Kuna misemo ya kuongezea inayosema ' talk to people the way you want to be talked'
Na msemo mwingine ' Respect is earned not given'
Uzalendo ni tunu inayogusa kila mmoja katika jamii bila kujali nafasi yake.
Ndicho chombo kinachobeba umoja na utaifa. Uzalendo usitumike kama 'chaka' la kuwabagua wananchi, kwamba wapo wanaopaswa kusimamia uzalendo na wapo wanaopaswa kutumikia uzalendo
Mwananchi asiyemheshimu kiongozi aliyewekwa madarakani na wananchi hana sifa ya uzalendo
Equally, kiongozi asiyewaheshimu waliomweka madarakani hana uzalendo