Jee hii inaweza kuwa moja ya sababu ya kundi fulani kuwa mbele kitaaluma? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jee hii inaweza kuwa moja ya sababu ya kundi fulani kuwa mbele kitaaluma?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gozigumu, May 17, 2010.

 1. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanafunzi sita, mwalimu wanaswa kughushi vyeti Send to a friend
  Sunday, 16 May 2010 21:20
  0
  diggs
  digg
  Mkinga Mkinga

  WATAHINIWA sita wa mtihani wa ualimu Daraja A, wamekamatwa kwa tuhuma za kughushi vyeti vya kidato cha nne na huenda wakapandishwa kizimbani leo.

  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa watahiniwa hao ni wa chuo cha ualimu cha West Dar es Salaam, na walikamatwa Mei 12 mwaka huu na Polisi kwa kushirikiana na maofisa wa Baraza la Mitihani (Necta). Wakati wakikamatwa walikuwa kwenye vyumba vya mitihani.

  Watuhumiwa hao, ambao majina yao tumeyasitiri wanadaiwa kutumia vyeti vya watu wengine. Watu ambao vyeti vyao vilitumiwa na watuhumiwa hao ni Bumi Maboko, Grace Elissa, Agness Kaduma.
  Wengine ambao vyeti vyao vilitumika ni David John, Aneth Mandoro pamoja na Bernard Abel
  . Habari zinadai kiuwa mmoja wa vigogo wa chuo hicho pia anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.

  Taarifa za ndani kutoka Necta zinaonyesha kuwa watuhumiwa hao ni miongoni mwa wanafunzi 150 ambao vyeti vyao vilifanyiwa tathmini na baraza hilo na vilibainika kuwa si halisi huku wengine wakitumia vyeti visivyokuwa vyao.

  Gazeti hili lilibahatika kupata nakala ya fomu zilizojazwa awali na wanafunzi hao, ambao zinaonyesha majina tofauti huku picha ndogo, zikiwa na sura zilezile, lakini pia fomu za usajili wa kufanya mtihani zikiwa na picha za kubandika na sio zilizochanganuliwa (scanned) kama utaratibu unavyotaka.
   
 2. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi wajameni tunakwenda wapi kwa staili hii!
   
Loading...