Jee, duniani kuna nchi inayoendeshwa vibaya zaidi kuliko Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jee, duniani kuna nchi inayoendeshwa vibaya zaidi kuliko Tanzania

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Sijali, May 7, 2011.

 1. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,054
  Likes Received: 405
  Trophy Points: 180
  Naanzisha maudhui haya kwa minajili ya kuwafungua macho watu wengi ambao hawajapata nafasi ya kutembea, na ambao siku zote wanalishwa propaganda za watawala. Kwamba nchi ina amani, mshikamano bla bla bla.

  Zamani walikuwa wanatoa mifano ya South Afrika, Angola, Namibia n.k. jinsi mtu mweusi anavokandamizwa huko na kuwa Watanzania wako huru na inapasa kujivunia nchi yao.

  Ila mapambano yalipogeuka kuwa ya uchumi wakawa hoja hizo hawanazo. Sasa nadhani hoja moja tu wanayo, nayo ni ile ya amani. Hii pia inatafunwa siku hadi siku kutokana na kupungua mno kwa migogoro Afrika.

  Katika matembezi yangu, na kusema kweli nimetembelea nchi ambazo zilikuwa katika vita tangu 70 au 80s, kama Chad,Sudan hata Somalia. Ila kitu kimoja ambacho Tanzania ni tofauti kabisa, ni jinsi maisha ya raia wengi yalivyo duni na mabaya. Kwa hili, hata Somalia ina afadhali. Bila shaka, ni uongozi mbaya, tangu uhuru, ndio ilioifanya Tanzania kufikia hapa, ingawaje ina utajiri mkubwa.

  Kama mtu ana jina la nchi yeyote duniani ambayo raia wake wengi wanaishi maisha duni, ya kudhalilishwa na watawala, kuliko Tanzania....aitaje.
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  May 7, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu nilikuwa na Somalia kichwani. Sasa kama na yenyewe mambo ni mazuri kuliko TZ basi tena hakuna nyingine. Manake Somalia ndio nchi pekee ya Kiafrika ambayo inafuata hatua ambazo ulaya walizifuata na kupata maendeleo. Kwa sasa Somalia wako kwenye hatua ya Pirates ambayo wazungu wengi waliitumia kujitajirisha miaka ya huko nyuma kwa kuteka mizigo na mameli baharini.
   
 3. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,054
  Likes Received: 405
  Trophy Points: 180
  Mkuu, at least Somalia hakuna mgao wa umeme wa kufa, ambapo hata kama hukutumia umeme unalipishwa. Tena mtandao wao wa simu mzuri kuliko Bongo mara kumi. Somalia wana mabenki yanayomilikiwa na wazawa na uchumi wao wanaumiliki wao wenyewe. Kati ya haya hakuna hata moja nJIni Tanzania. Wasomali hivi sasa wanamiliki sehemu nzuri ya uchumi wa Kenya. Hilo linawezekana tu kutokana na confidence waliyo nayo. Wabondo wangapi wanamiliki chochote Kenya?
  Usisikie propaganda: dunia hii hakuna anayeishi vibaya kama Mbongo!
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Dah! Hakuna kwakweli.
  Tz inaongoza hadi wazawa tunatamani kukimbia.
   
 5. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ni kweli munaokimbia muna sababu. Labda tumwombe Kagame atutawale angalao kwa mwaka mmoja
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Duh, hata mie najiuliza hili swali nakuwa skeptical sana kwamba kuna nchi ambayo IS HIGHLY MISMANAGED kama Tz, sipati jibu kweli..naamini we are the worst. Ni hatari kwa kweli kwamba hali ni mbaya na kila kitu kipo shaghalabaghala kama shamba la mahindi lililovamiwa na nguruwe pori. Structured lifestyle haionekani popote.
   
 7. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,060
  Likes Received: 1,099
  Trophy Points: 280
  Kukimbia haitasaidia kwasababu kama vijana wote wenye nguvu watakimbia nani atabaki kuijenga nchi?
   
 8. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  inji hii imeoza, imelaaniwa
   
 9. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,992
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  Mbona me ntanenepa wakuu.
   
 10. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Ukifikiria sana shetani anaweza kupenyeza wazo la kujitundika, hakyamungu vile! Mgao wa umeme na maji tangu uhuru. Khaa! Halafu hizi shule za kata ndo mwisho wa uhai wa taifa.
   
 11. C

  Chesty JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,348
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Tanzania ni nchi ambayo potentially ni tajiri sana kama tungekuwa na viongozi wanaojali maslahi ya nchi na sio ya familia zao.

  Ukitaka kujua kuwa tuna viongozi wa hovyo the world has ever seen angalia jinsi miji yetu ilivyokaa hovyo hovyo bila mipango miji. Ni nchi ambayo kila mtu inabidi atafute hela kwa njia yoyote ile ili ajenge nyumba kwa plan anayoijua yeye na iangalie anakotaka yeye, and nobody cares!!

  Ni nchi pekee (nadhani) ambayo unatakiwa kulipa rent mwaka mzima wakati wewe unapokea mshahara kwa mwezi, and nobody cares!!

  Ni nchi pekee ambayo (juzi kwenye maandamano ya mei mosi) waendesha pikipiki walipita mbele ya rais wa JMT wengi wao wakiwa hawana helmets, and nobody cared, including the president!!!

  Ni nchi pekee ambayo viongozi wa vyama vya upinzani wanaweza kutaja majina ya wezi wa mali ya uma na polisi wasifanye chochote mpaka leo!!

  Ni nchi pekee ambayo gharama za bidhaa zinapanda kiholela tu, and nobody cares!!

  Ni nchi pekee ambayo watu wanaweza kupaki magari baa wakanywa pombe na wakimaliza wanapanda magari yao wanaondoka, polisi hawana taarifa hizi na wala hawana mpango!!

  Ni nchi pekee ambayo mgao wa umeme, ukosefu wa maji is the order of the day. Nobody wants to be bothered!!

  Halafu Sugu anaposema pigeni mawe hawa watu mnasema anakosea!!!
   
 12. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  sasa si mpaka upewe hiyo nafasi ya kuijenga hiyo nchi.
   
 13. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #13
  May 8, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Hii nchi ni mismanaged,there is no doubt about that.Na hili swala la viongozi kusema ,'' Nchi hii ni ya amani,siyo kama Somalia,siyo kama Libya'',hii ni makosa. Mtu anataka kujikosha kwa kuwachafua watu wengine. Inakuwa kama watu wengine hawana ruhusa kuwa na amani kwa sababu amani ni hati miliki ya Tanzania.
  It is interesting to note kwamba siku moja kabla ya milipuko ya mabomu Mbagala,Rais Mwinyi alikuwa anasema,'' Tanzania ni nchi safi kabisa. Badala ya kuzalisha wakimbizi,yenyewe inapokea wakimbizi,inawapa hifadhi wakimbizi.'' Kesho yake Tanzania ilikuwa na wakimbizi elfu kadhaa,wamekwenda Uhuru Stadium. Halafu yule yule Waziri mhusika hakuulizwa swali lolote,badala yake nadhani amekuwa promoted,yupo sasa katika Kamati Kuu ya CCM. Ndiyo haya mambo yanayolete maandamano katika Nchi nyingi duniani. The Governments are not self-regulating themselves,wanasubiri mpaka watu waandamane.
  Marehemu Abdulrahaman Babu alihawai kusema[wakati alipokuwa hayupo Serikalini,wakati alipokuwa anaishi Ulaya na Marekani],kwamba,''Kama Tanzania haina vita, maendeleo yake yako wapi?''
   
 14. k

  kipakaMwitu Senior Member

  #14
  May 8, 2011
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 159
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  chesty napita tu, nitarudi baadae.
   
 15. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wenyewe chama cha magamba wanakuambia vijana ni taifa la kesho na si la leo....sasa je,umewahi kuiona kesho? Jibu ni kwamba chama cha magamba hakijali vijana,ila kinajali wazee tu.....kwahiyo ni bora kwenda kubeba maboksi nchi za watu kuliko kupoteza time bongo.
   
 16. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenena!!!naongezea

  Nchi ambayo kiongozi wake priority zake ni kuhudhuria mikutano ya kimataifa,na misiba bila kujua wananchi wanamatatizo gani
  Nchi ambayo kupokea rushwa kwa polisi ni kawaida na ndiyo wanaoongoza kwa kupokea rushwa
  Nchi ambayo inatumia fedha aina mbili tofauti na hakuna wa kumuuliza gavana
  Nchi ambayo miundombinu iliyoachwa na mkoloni ilikuwa mingi na kufanya kazi kuliko sasa,na inazidi kuharibika
   
 17. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,405
  Trophy Points: 280
  Chesty,
  Nimeupenda sana uchambuzi wako. Huo ndiyo ukweli mtupu.

  Pengine umesahau. Hii ndo nchi pekee ambaye raisi alisema hazitaki kula za wafanyakazi kisha akakanusha hakusema hivyo.

  Ndo nchi pekee ambayo rais anawaambia wanafunzi wa kike wanapata mimba kwa kiherehere chao.

  Nchi pekee ambayo mtoto wa rais anakanyaga zulia jekundu kwenye sherehe za kitaifa.

  Hii ndo nchi hovyo kabisa.
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,820
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha sana kusema kweli ukitilia maanani rasilimali chungu nzima tulizojaliwa na Mwenyezi Mungu halafu tunakuwa nchi ya mwisho duniani inapokuja namna nchi yetu inavyoendeshwa na hao wanaojiita Viongozi.
   
 19. FIDIVIN

  FIDIVIN Senior Member

  #19
  May 8, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndg

  Naona watu wameathirika sana na michango ya siasa iliyotawala hapa JF. Tunaamini kila kinachoongelewa humu bora kinaiponda serikali au kiongozi wa chama ukipendacho kasema basi ni kweli. Ya JF si kwamba yote ni sahihi, utapotoka.
  Niseme hivi TZ haijafika hapo mnaposema. Jiulize ni wangapi wanaingia TZ wakiziacha nchi zao, wako wachina, Indians, Africans, unabakia kujiliwaza eti TZ ni mbaya.
  Nakushauri badilisheni mtizamo wenu. Soma Methali 18.21 itawasaidia.
  Ukitaka kujua uzuri wa TZ hebu toka hata mwezi mmoja nenda hiyo nchi unayosema ni nzuri, Somalia, Kenya, Sudan n.k
  Kama hupendi chama tawala usichanganye na kuipenda nchi yako, maana kuitukana nchi yako ni kujitukana mwenyewe.
   
 20. m

  mshikachaki Member

  #20
  May 8, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  nchi pekee ambayo watumishi wake wanalipwa mishahara midogo na wakilalamika wanatishiwa
  nchi pekee ambayo watumishi wake wengi na viongozi wake wanavyeti vya kufoji
   
Loading...