Elections 2015 Jecha anawatia kichefuchefu wengi

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,233
12,508
Jamaa wakimkumbuka Jecha matumbo yao huwa yanawakata, mate yanawajaa midomoni, usingizi unawapaa na wanashikwa na simanzi la hali ya juu. Jecha ni alama yao ya matumaini yaliyofifia mithili ya jina na sauti ya ndege bundi anapolia juu ya paa la nyumba au kwenye mti uliyoko karibu sana na nyumba ambayo ndani yake kuna mgonjwa anayeshindwa hata kumeza uji. Jecha ni jina linalosababisha jamaa wengi kupoteza matumaini kabisa na wasijue what next, how and for what?. Ama kweli Jecha ataingia kwenye historia zetu za sasa na za vizazi vingi sana vijavyo.

Kama A ilikuwa sawa B na B ilikuwa sawa C lakini A haikuwa sawa C, hapo patakuweje wajemeni 2020?
 
Mkuu hakuna anaekosa usingizi kwa yule mtu, ila yeye ametoa somo kubwa sana ni kwa jinsi gani mwenye nguvu anaweza kushindana na asie na nguvu, kuna njia nyingi sana. Alichofanya Jecha kuna tafakuri kubwa sana kuelezea tatizo lilipo Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kilichotokea kule kinaweza kutokea Tanganyika 2020 pia
 
Je, kuna haja ya Maalim kugombea tena 2020?
 
Jecha anakuja kuwabatiza CUF kwa makaa ya moto
Baada ya Idd Amin kutimuliwa Uganda na Nyerere, alikuwa kila wakati anamtaja Nyerere huku akisonya na kukuna kichwa kwa hasira kwa maisha yake yote yaliyokuwa yamebakia. Hivi sasa jamaa zetu kila wakati huwa wanalitaja jina la Jecha na kusonya tu kila wakati.
 
Jamaa wakimkumbuka Jecha matumbo yao huwa yanawakata, mate yanawajaa midomoni, usingizi unawapaa na wanashikwa na simanzi la hali ya juu. Jecha ni alama yao ya matumaini yaliyofifia mithili ya jina na sauti ya ndege bundi anapolia juu ya paa la nyumba au kwenye mti uliyoko karibu sana na nyumba ambayo ndani yake kuna mgonjwa anayeshindwa hata kumeza uji. Jecha ni jina linalosababisha jamaa wengi kupoteza matumaini kabisa na wasijue what next, how and for what?. Ama kweli Jecha ataingia kwenye historia zetu za sasa na za vizazi vingi sana vijavyo.

Kama A ilikuwa sawa B na B ilikuwa sawa C lakini A haikuwa sawa C, hapo patakuweje wajemeni 2020?
Jecha ni mpenda haki anastahili kupewa nishani ya Utumishi bora!
 
Zanzibar tangu 1995 kuna faulo ambazo mwamuzi anaziona ila anapeta.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom