Je, Zitto atakamatwa leo katika uwanja wa ndege wa JKN?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Kwa mujibu wa Zitto Kabwe, leo anatarajiwa kuwasili nchini akitokea Marekani ambako alikuwa kwenye ziara ya "kusikiliza maoni ya Watanzania na kutafuta kuungwa mkono na mataifa ya Magharibi ili kuzuia Tanzania kurudi kwenye bunge la chama kimoja".

Mengi yamesemwa na Wabunge na Wananchi kuhusu safari ya Zitto Kabwe katika nchi za Ulaya na Marekani.

Muhimili wa Bunge kupitia wabunge mbalimbali wamejadili kwa kina na mtazamo tofauti kuhusu safari ya Zitto katika nchi za Ulaya na Marekani na matokeo yake.

Baadhi ya wabunge walishauri serikali kuichukua pasi yake ya kusafiria pindi atakaporejea nchini huku wengine wakienda mbali zaidi na kudai akamatwe na kushitakiwa kwa makosa la kutumia mali za bunge kinyume cha kanuni na sheria za nchi.

Pamoja na madai ya wabunge ndani ya bunge la Tanzania kuishauri serikali lakini hatujasikia kauli rasmi ya serikali kuhusiana mjadala huu.

Tumemsikia Zitto akidai kuna maandalizi ndani ya serikali ya kumkamata atakaporejea nchni na kwamba haogopi kukamatwa!

Je, kutosikia kauli ya serikali ina maana inatupeleka kwenye maxim ya kisheria inayosema, "silence gives consent"

Je, Jeshi la polisi litamkamata Zitto pindi akirejea nchini?

Je, kukamatwa kwa Zitto na kuwekwa ndani kutaendelea kufuta ule uvumi kuwa yeye ni sehemu ya "ruling system" nchini.

Je, kutokamatwa kutaendelea kusadifu hoja kuwa yeye ni sehemu ya "ruling system" nchini.

Je, kukamatwa kwake kutatoa matokeo gani kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini na hasa kwenye harakati za wapinzani?

UPDATE:
Zitto Kabwe ametua leo katika Uwanja wa JKNI na kupokelewa na viongozi wa ACT-Wazalendo.

Mpaka anapanda gari kuelekea nyumbani hakuna polisi ambaye alijitokeza kumkamata!
 
Trust me... Hatakamatwa na hata akikamatwa itakuwa zuga tuu... In 72 hrs to come atadhaminiwa... Mchango wake wa kuiweka CCM madarakani 2015 sio wa kitoto.
Mazingira anayotengeneza sasa ni kwa ajili ya kuvuta mpunga Mwingine October

Jr
 
Trust me... Hatakamatwa na hata akikamatwa itakuwa zuga tuu... In 72 hrs to come atadhaminiwa... Mchango wake wa kuiweka CCM madarakani 2015 sio wa kitoto.
Mazingira anayotengeneza sasa ni kwa ajili ya kuvuta mpunga Mwingine October

Jr

Kumbuka 72hrs ni siku tatu akiwa mahabusu!

Kwa hiyo kwa sasa pia yuko kwenye "mission" ya kuiweka tena CCM madarakani mwaka huu?
 
Back
Top Bottom