Je Ze Komedi imenunuliwa na Mafisadiz?

Shomari

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,112
241
Mimi ninashindwa kuelewa! kama kuna mtu ana uzoefu wowote kuhusu hakimiliki aje atuambie hapa! sababu kila siku ukisikiliza hii kesi ya ze komedi utakuta hakuna kinachoendelea zaidi ya kuoshwa macho na bongo zetu!

Sasa je ? hao ze komedi wamenunuliwa na mafisadi ama wamenyamazishwa? kipi ni kipi?

Pia nimepata hii clip ambayo ninadhani mpoki alikuwa akimuongelea Rost Tamu Mazizi! na Ajali zingine kubwa kubwa! Tah! tah! tah!

Bonyeza hapa
 
Hawa wameshanunuliwa na kesi wamefungua wenyewe kupoteza muda,walishauriwa na wanaofahamu mambo haya kuwa wabadili majina kidogo[herufi chache] na wachape kazi.
Watu wenyewe wanaonekana katika kumbi za starehe,matumizi makubwa,magari mazuri etc.WAMENYAMAZISHWA kuna ulazima gani kufanya kazi kama unalipwa usifanye?
 
nami nasikia sikia kuwa ze comedi wamenunuliwa na mafisadi je wataweza kuwakilisha na kufikisha ujumbe wa walengwa kama wameshanunuliwa??au itakuwa kwa manufaa ya mafisadi?yetu macho
 
Mbona tunawaangalia the comedy tu, hawa ni vijana wanaojaribu kutafuta maisha, lizee lizima kaa Mengi kuwawekea kiwingu ni kwa ajili gani, mbona hatumwambii Mengi kuwa awaache hawa vijana na jina hili kwa mapesa aliyonayo atakua amepoteza nini?. Jamani jamani tukiwaacha kweli watanunuliwa
 
nami nasikia sikia kuwa ze comedi wamenunuliwa na mafisadi je wataweza kuwakilisha na kufikisha ujumbe wa walengwa kama wameshanunuliwa??au itakuwa kwa manufaa ya mafisadi?yetu macho

Jamani...
Ze Comedi is still independent under contract with TBC1, Show zao ni Alhamisi,marudio ni J2, just only the slight change of name.

Wangekuwa hawako free sidhani kama wangekuwa na confident ya kuigiza kuhusu kifo cha Wangwe.

Let them do the best they can offer....
 
ndio, wamenunuliwa na mafisadi. si uliona jana walipoonyesha wanacheza kwenye jengo la Quality group, jengo la Manji?
 
ndio, wamenunuliwa na mafisadi. si uliona jana walipoonyesha wanacheza kwenye jengo la Quality group, jengo la Manji?

Mkuu kidzogolae;
Orijino Komedy kuigiza mbele ya Quality Group building still sio evidence ilosimamia kucha.

Kwahiyo hao jamaa wakiigiza mbele ya ofisi za Vodacom au kudhaminiwa na Vodacom utasema imenunuliwa na Mheshimiwa R.A?

Plz kama una maanisha unachotetea then leta hoja with evidence...una haki ya kutoa maoni/fikra zako.
 
Mimi nilishasema huko kwenye thread nyingine tulipokuwa tunachangia suala la hawa mafisadi wadogo.
Najua wapenzi wengi wa ze komedi na hasa fisadi's supporters wanaweza kusema wanavyosema na kuwapamba wanavyopenda.
Hawa vijana wameshanunuliwa na mafisadi na hawawezi kamwe ku perform kama zamani.
Kiwango lazima kishuke tu. Maana hawana uhuru waliokuwa nao ch 5.
Ndiyo sababu wanaweza ku act kifo cha Mengi lakini hawezi kuonyesha kuwa wahusika ni sisiemu wenyewe. Ila wana act mambo ya wakina mtikila tu wakipigwa mawe.
Sasa subiri uone kama wata act sisiemu kushindwa.
Hawa kwisha. Na si siku nyingi tutaacha hata kuangalia upuuzi wao. Labda watabaki wakiangalia mafisadiz na familia zao.
 
Hata hicho kifo cha Wangwe ilikuwa ni sehemu ya Kampeni za CCM Tarime. Reflection ya ujumbe ilikuwa inalenga kusisitiza kuwa aliuawa.

Wakurya sio wafunga misuli na kanzu, mwanaume suriali, kaptula au utupu kama masai.
Hawa vijana hawana jipya tena kwani mengi ya matukio ya kuigiza na kukosoa yapo CCM na serikalini.

Njaa mbaya, pole Origino Komedi kama sio origino komoni.
 
Kuna wakati nilisikia wanaongelea Manji kuwa mlezi wao na kusudio lake la kuwapeleka ulaya na kadhalilka....pia waligusia kwenda kusoma SA. Inavyoonekana wameshawekwa chini ya himaya ya watu/mtu fulani na kwa jinsi ilivyo kutakuwa na "strings attached" kwenye makubaliano yao ikimaanisha itabidi watekelezwe matakwa ya wahusika....Soma zaidi kwenye habari hapo chini.

Habari zaidi,
1. HabariLeo: Gwiji la habari Tanzania | Manji ajitosa Ze Comedy

2. Global Publishers - Tanzania Newspapers

3. Manji aitwaa Ze Comedy

Kidokezo kutoka habarileo....

Daily News; Saturday,May 31, 2008 @00:05

"Kundi la vichekesho la Ze Comedy limetangaza kuhamishia maonyesho yake katika runinga ya Taifa ya TBC1 kuanzia Julai. Wachekeshaji hao waliokuwa wakifanya shughuli zao East Africa

Television ‘Channel 5' pia wamemtangaza Mfanyabiashara maarufu nchini ambaye pia ni mfadhili wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji kuwa mlezi wao ambaye atakuwa na jukumu la kuwagharimia katika safari mbalimbali watakazozifanya kwa ajili ya maonyesho"...........
 
Mbona tunawaangalia the comedy tu, hawa ni vijana wanaojaribu kutafuta maisha, lizee lizima kaa Mengi kuwawekea kiwingu ni kwa ajili gani, mbona hatumwambii Mengi kuwa awaache hawa vijana na jina hili kwa mapesa aliyonayo atakua amepoteza nini?. Jamani jamani tukiwaacha kweli watanunuliwa

Sawasawa. Anatumia rungu kuua mbu.
 
Jamani...
Ze Comedi is still independent under contract with TBC1, Show zao ni Alhamisi,marudio ni J2, just only the slight change of name.

Wangekuwa hawako free sidhani kama wangekuwa na confident ya kuigiza kuhusu kifo cha Wangwe.

Let them do the best they can offer....

Sasa hivi hata mtu akiumwa na mbu atasema ni mafisadi, some time we are comparing incomprable, mafisadi wawanunue ze comedy kwa lipi?
Akija mtu na pesa yake na kuwaambia njooni mfanye shooting hata kwenye jengo langu nitawalipa wakate eti kwakuwa jamaa annathuhumiwa na ufisadi.

Jamani jamani jamani ufisadi isiwe kisababu cha kutufanya tusiendelee kufikiria jamani.

Wangekuwa hawako free sidhani kama wangekuwa na confident ya kuigiza kuhusu kifo cha Wangwe NIMEIPENDA HII
 
Mimi nilishasema huko kwenye thread nyingine tulipokuwa tunachangia suala la hawa mafisadi wadogo.
Najua wapenzi wengi wa ze komedi na hasa fisadi's supporters wanaweza kusema wanavyosema na kuwapamba wanavyopenda.
Hawa vijana wameshanunuliwa na mafisadi na hawawezi kamwe ku perform kama zamani.
Kiwango lazima kishuke tu. Maana hawana uhuru waliokuwa nao ch 5.
Ndiyo sababu wanaweza ku act kifo cha Mengi lakini hawezi kuonyesha kuwa wahusika ni sisiemu wenyewe. Ila wana act mambo ya wakina mtikila tu wakipigwa mawe.
Sasa subiri uone kama wata act sisiemu kushindwa.
Hawa kwisha. Na si siku nyingi tutaacha hata kuangalia upuuzi wao. Labda watabaki wakiangalia mafisadiz na familia zao.

Kwa swala la freedom hata mimi na doubt maana ile TBC1 si ya wenyewe? But can that conclude kwamba wamenunuliwa?
 
It doesn't conclude lakini unaweza kusoma barua ndani ya bahasha
..With binocular au?? Hawajanunuliwa wala nini.. Nyie mnataka wanachoigiza kiwe vipi?

Nina imani kabisa maigizo yao yanaonyesha hali halisi ya nchi yetu na lazima kuna watu watakuwa wanaguswa wether ni fisadi au sio fisadi lakini message inakuwa delivered. Kumbuka wao ni wasanii na wanaishi kwa kazi hiyo mikwaruzano ya wenye pesa sidhani kama wao inawahusu kwa namna yoyote ile sema wabongo tunapenda ku-raise mambo mengine pasipo kufikiria kwa kina.
 
Hii orijino komedi, ni feki komedi kwa kusema kweli.

Hivi kuna mmoja wenu aliyeshtuka na jinsi vijitangazo vyao vilivyo kati kati ya onyesho?

Onyesho la kwanza TBC1 walitangaza biashara ya umalaya. Lililofuata sikuliangalia. Hili la jana wametangaza biashara ya utoaji mimba.

Whither Tanzania? Au ni mimi peke yangu niliyeona? Na sijasoma popote katika vyombo vya habari Tz vilivyolalamikia hilo. Pengine ndivyo tulivyo?
 
Mkuu kidzogolae;
Orijino Komedy kuigiza mbele ya Quality Group building still sio evidence ilosimamia kucha.

Kwahiyo hao jamaa wakiigiza mbele ya ofisi za Vodacom au kudhaminiwa na Vodacom utasema imenunuliwa na Mheshimiwa R.A?

Plz kama una maanisha unachotetea then leta hoja with evidence...una haki ya kutoa maoni/fikra zako.

Yaani wewe, sijui umeyasoma mawazo yangu na au post yangu iliyopotea kimiujiza?
 
Hii orijino komedi, ni feki komedi kwa kusema kweli.

Hivi kuna mmoja wenu aliyeshtuka na jinsi vijitangazo vyao vilivyo kati kati ya onyesho?

Onyesho la kwanza TBC1 walitangaza biashara ya umalaya. Lililofuata sikuliangalia. Hili la jana wametangaza biashara ya utoaji mimba.

Whither Tanzania? Au ni mimi peke yangu niliyeona? Na sijasoma popote katika vyombo vya habari Tz vilivyolalamikia hilo. Pengine ndivyo tulivyo?

Mkuu
Hujakosea,halafu kumbe nchi ye2 inaruhusu utoaji mimba maana TBC ni shirikisho lililo chini ya goverment.

Nadhani hawajapata consultant mzuri awashauri especially about the side effects.
 
Back
Top Bottom