Je, Z'bar ni kisiwa cha ufuska? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Z'bar ni kisiwa cha ufuska?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Jul 11, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,520
  Likes Received: 81,905
  Trophy Points: 280
  Zichukuliwe hatua Zanzibar isigeuke kisiwa cha ufuska, ulevi
  Maulid Ahmed
  Daily News; Wednesday,July 09, 2008 @20:01

  HIVI karibuni nilikuwa Zanzibar kwa takriban wiki tatu kwa ajili ya shughuli za kikazi. Lakini kutokana na uenyeji wangu kisiwani huko niliona Zanzibar niliyokuwa naifahamu miaka 10 iliyopita sasa si hiyo tena.

  Ninaweza kusema kuwa Zanzibar imeharibika nikiangalia upande wa utamaduni na maadili ya watu wake. Leo ni kawaida kukuta baa kila pembe, ni kawaida kukuta ‘ngono’ ikifanyika hadharani kati ya wanawake na wanawake, wanaume na wanaume na hata wa jinsia hizo mbili.

  Hali hiyo si mjini pekee lakini nimeishuhudia zaidi maeneo ya shamba hasa yenye hoteli za kitalii lakini pia kwa kuelezwa na wakazi wa huko.

  Katika maeneo yenye kushamiri watalii ndipo uchafu huo hutendeka zaidi na hiyo kwa mawazo yangu naamini inatokana na utalii huo.

  Kutokana na hali hiyo ndipo leo tunasikia athari za utalii huo ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ugonjwa wa Ukimwi kisiwani humo kama Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji Samia Suluhu Hassan alivyolieleza Baraza la Wawakilishi kuhusiana na utafiti uliofaywa kutathmini hali ya Ukimwi katika sekta ya utalii.

  Nimefurahi kusikia Serikali yenyewe ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imelitambua hilo. Lakini nadhani umefika wakati wa kuchukua hatua kudhibiti hali hiyo.

  Kauli kwamba ‘Zanzibar njema atakaye aje’ ingefaa ifanyiwe tathmini tena licha ya kusudio lake kuwa zuri la kuwakaribisha watu. Ninachosema ni kwamba iangaliwe namna ya kuwakaribisha watu wema na si kuwakaribisha wabaya wanaokwenda kuiharibu.

  Elimu ya Ukimwi bado naona ipo chini. wananchi wa kawaida wanahitajika kuelimishwa zaidi ikilinganishwa na eneo kama Dar es Salaam lenye kila aina ya starehe ambako watu wake wengi wanaifahamu elimu hiyo na hawaoni aibu kudai kondomu kwa wale wanaofanya shughuli hiyo ya kujiuza au kufanya ngono ovyo.

  Kwa Zanzibar bado aibu ipo! Mtu anaona aibu kumwambia mwanamume avae kondom, anajihisi ataonekana mhuni. Hivi kufanya naye ngono mwanamume wa aina hiyo siyo uhuni? Inanishangaza sana.

  Kwa habati mbaya udogo wa kisiwa hicho unafanya mambo yawe hadharani zaidi. Watoto wa kiume wanajiingiza katika mchezo wa kufanya mapenzi na wanaume wenzao kama inavyofahamika ‘ushoga’ huku wanawake nao wanafanya mapenzi na wenzao tena kwa ufahari bila kujali kama kuna Ukimwi ambao unaendelea kuliteketeza taifa hili.

  Licha ya taifa kupata fedha nyingi kutokana na utalii, ni vizuri zaidi iwapo serikali itaanzisha mkakati wa kuzitembelea hoteli hizo za kitalii na kudhibiti ufuska unaoendelea huko na ikiwezekana kuwachukulia hatua wale wanaojiuza ambao kwa sasa kisiwani huko wameingia kwa kasi.

  Nimeshawahi kuelezwa kuwa katika hoteli za kitalii, kunarekodiwa sinema za ngono. Ingawa sijashuhudia lakini lisemwalo lipo na kama halipo linakuja, hali hiyo isipuuzwe.

  Hizo baa zilizotapakaa kwa wingi si kuwa zinatumika tu kwa ajili ya watu kupata kinywaji kujiburudisha bali zimekuwa vichaka vya ufuska. Zipo baa maarufu za mashoga na hapa nisingependa kuzitaja lakini najua zinafahamika kunapofanyika ufuska waziwazi lakini nashangaa zinaachwa kushamiri badala ya kudhibitiwa.

  Zisipofanyika jitihada za makusudi kukinusuru kisiwa hiki chenye wakazi wasiofikia milioni mbili basi Zanzibar yenye maadili, inayothamini utamaduni na watu wake wakarimu waliokuzwa kwa misingi ya dini itageuka na kuwa kisiwa cha ufuska, ulevi na kilichojaa waathirika wa Ukimwi.
   
 2. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ya kawaida hayo kila penye utalii
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,520
  Likes Received: 81,905
  Trophy Points: 280
  Je, yanaweza kudhibitiwa ili maadili mazuri ndani ya kisiwa hicho kama ambavyo yalivyokuwa yanafahamika na Watanzania wengi hasa wale waliowahi kufika Unguja yasiharibike zaidi?
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Watu Wanashindwa Kuelewa Au Kupotosha Makusudi

  Hivi Mombasa Wako Wapi? Jee Wao Hawakuwa Watu Wazuri,, Tafuta Sehemu Zote Zenye Utalii Uone Hali Hio Ikoje ?

  Kuna Wageni Wanaokuja Hupenda Kufanyiwa Massage Na Mengineo Na Nyinyi Mwahitaji Pesa Zao


  Zanzibar Nnaona Iko Pazuri Ukilinganisha Na Wenzetu Ila Ya Kale Hayarudi Na Pia Kujaribu Kama Wafanyavyo Tusiende Kwa Kasi Ambapo Lazima Tufike Kwenye Tourism Industrial

  Ila Kwa Wenye Kutembea Na Kusoma Mambo Ya Utalii Huna Jinsi Hata Uchina Dubai Na Kwengineko Wenye Kuheshimika Na Kuheshimu Mila Zao Hawana Budi Kusalim Amri Hapo

  Beijing Olympic Waulize China Kwa Upande Wa Culture Imewagharimu Nini Na Nnnategemea Wachina Watatafunwa Sana Tu Olympic Hii


  Kwa Kumalizia Ukinywa Supu Ya Mbuzi Usiogope Kidusi Ila Tia Tangawizi Nyingi Kupunguza Makali
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,520
  Likes Received: 81,905
  Trophy Points: 280
  Kwa maana nyingine hakuna uwezekano wa kudhibiti huu ufuska unaoshamiri kila kona ya Z'bar kwa sababu ya utalii. Kwa maoni yangu hali ikiachwa hivi basi tusishangae miaka michache ijayo watu (wake kwa waume) kuanza kupukutika kwa kasi ya ajabu kutokana na ukimwi. Athari ya ukimwi miaka michache iliyopita ilikuwa ni ndogo sana ukilinganisha na miji kama Dar, Mbeya, Mwanza na Kagera. Elimu ya zinaa katika mikoa hiyo hasa matumizi ya condom imesaidia sana kupunguza uambukizwaji wa wale ambao hawajaathirika kama elimu ya zinaa haitatolewa Z'bar basi kutakuwa na vilio vya kusaga meno.
   
 6. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  Wewe ni mtu wa Pwani na sio mzaha.

  Nimejifunza neno jipya leo:
  Kidusi - unusual smell; bad flavor; smell of wild animal (animal smells); smell of fish


  .
   
Loading...