Je, Zanzibar Ni Sehemu Salama Kwa Uwekezaji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Zanzibar Ni Sehemu Salama Kwa Uwekezaji?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rich Dad, Aug 29, 2011.

 1. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wana JF naombeni Tujadili!
  Kutokana na kushamiri kwa matukio ya hivi karibuni ya uchomaji wa biashara za watu na hasa zinazomilikiwa na watu wasio wazanzibari. Baa zimekuwa zikichomwa moto karibuni kila siku, inasemekana jeshi la polisi na mahakama halioneshi ushirikiano unaotakiwa kuwawajibisha watu wanaokula njama na kufanya vitendo hivyo.

  Cha kushangaza zaidi ni kwamba vitendo hivi wanafanyiwa wafanyabiashara wenye mitaji midogo, wachomaji hawa hawafiki hoteli kubwa ambako kimsingi watu ndo wanakuwa huru zaidi kufanya yale wayapendayo ( kuanzia kwenye kuvaa mavazi yanayoacha sehemu kubwa ya mwili wazi hadi kwenye unywaji wa pombe). Na mfano mzuri ni hoteli ya Zanzibar Beach Resort ambayo nilifikia juzi, nenda huko kajionee mwenyewe usisubiri kusimuliwa.

  Vitendo hivi vikiendelea kufumbiwa macho bila vyombo vya usalama kuchukua hatua stahiki, nina mashaka na huko twendako. Je, Zanzibar imekuwa declared ni taifa la Kiislam? Na kama ni hivyo kwanini Zanzibar bado ni part ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?

  Tafadhali kama unaweza, toa maoni yako kuhusu nini kifanyike ili kuweka mambo sawa ndani ya Zanzibar.
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Zanzibar si sehemu salama kwa uwekezaji.
   
 3. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Je, sababu hasa ni nini? Uislam ndo threat kwa biashara/ wafanya biashara au ni culture ya wazanzibari?
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  BOTH and many others
   
 5. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ukitaka poteza assets zako nenda kawekeze zanzibar kwenye issue za bar au pub.
   
 6. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  zanzibar kila siku panazidi kuwa sehemu hatari kwa wawekezaje-haswa wa tanganyika-maana kuna Islamist hardliners wanaorise zanzibar ambao kwa mtazamo wangu polisi wameshindwa kuwazuia-hawa hardliners hawana tofauti na boko haram wale wa nigeria,wao kazi yao ni kuchoma bar za wawekezaji kila siku,nina imani siku bar zikiwewa zimeisha au zinakaribua kwisha watahamia kwenye biashara nyingine,na nyingine tena,
  SO ZANZIBAR SI SEHEMU YA KUWEKEZA
   
Loading...