Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,981
- 45,904
Baada ya Uchaguzi wa 2015 kuona mwanamke akigombea nafasi ya Urais, Bi. Ana Mghwira wa Act. Bi. Ana Mghwira amewapa matumaini wanawake wengi wa Tanzania kua ukiweka malengo unaweza, ni jambo la mtu kuzifuata ndoto zako tu na mengine Mungu ndiye anayeamua.
Ukijaribu kuangalia mwenendo wa sasa wa siasa za Zanzibar, utaona kabisa kua kuna wanasiasa ambao umri umewatupa, ubunifu umewaishia na sasa wanaonekana siasa zikiwashinda kabisa, kufurukuta 2020 ni kwa kudra tu, na watakua wanalazimisha, nyakati hazitakua upande wao.
Ila kuna kila dalili za kuibuka wanasiasa wapya na machachari katika anga za siasa za Zanzibar, hivi karibuni, mwanasheria na mmoja wa wanafamilia ya Karume amekua vocal sana kuhusiana na issue ya zanzibar. Amekua akizungumza mambo ambayo yeye anaamini si sawa, ingawa kwa wakati huo huo anaweza kua asiwe sawa katika mitazamo yake.
Je ndio kusema hayo ni kama mazoezi ya kuitafuta moja ya nafasi ya juu kabisa ya Uongozi visiwani Zanzibar?
Je, wazanzibari wapo tayari kuwa na mgombea na hatimaye rais mwanamke ifikapo 2020?
Ni jambo la kusubiri na kuacha muda uamue kwani muda ndio umekua jibu sahihi la maswali yetu pale ambapo majibu ya haraka yanatafutwa na kukosekana.