Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Naipongeza serikali kwakuanzisha mfumo mpya wa zabuni ya chakuka cha wagonjwa Muhimbili na kupunguza msongamano wa watu hasa wanaopelekea vyakula ndugu zao,
Lakini, Naomba kujua, Je zabuni ya chakula Hospitali ya Muhimbili ilitangazwa lini na nani alishiriki?
Nimeuliza haya kwakuwa jana 21/06/2016 imetangazwa rasmi kuwa ni "marufuku" chakula toka nje kuingizwa Muhimbili. Zingatieni, hili neno marufuku linanguvu sana hasa likitolewa na chombo kiitwacho SERIKALI.
Siku 10 zilizosalia kufika tarehe moja, hazitoshi kufuata misingi ya manunuzi ya umma, kwa maana ya mchakato wa kutangaza tenda, kumtathimini mzabuni, na kumpa rasmi kazi husika ambayo inakadiriwa kulisha watu 3000 kwa mlo mmoja, hii ni tenda kubwa, kwani inatakiwa milo mitatu kwa siku hali inayopelekea kuwa na wastani wa kulisha watu 9000.
Hoja yangu ni kwamba njia za kufikia haya yanayoitwa mapinduzi ya sekta ya afya zinafuatwa au kuna sauti moja kuu kuliko zote inayoamua haya?
Ni vema na haki umma ukajulishwa mchakato huo wa mzabuni ulivyopita au utakavyopita mpaka mgongwa wangu akala milo mitatu salama...
Ifahamike kuwa, wagonjwa wachaga huoendelea kula mtori, Wahehe hupendelea kula ugali wa ulezi na maharage meupe (nanavara), Wamakonde hupendelea kuka ugali wa mhogo na samaki nchanga,
Swali la pili, je mzabuni wenu ameelezwa hayo na atayazingatia?
Wagonjwa wengi wale wanaoshindwa kula, hubembelezwa kwa lugha za makabila na ikishindikana hutumia tamaduni za kiafrika kuhakikisha mgonjwa huyo anakula... Je wauguzi hawa wameshapewa mafunzo ya kitamaduni ikiwemo kushika hirizi kwaajili ya wagonjwa wetu? Msidhani wote tunaishi Masaki tu wengine bila hirizi na chale hatuishi duniani hapa.
Nimeuliza kwa nia nzuri ili tusijedhani tunaokoa maisha ya ndugu zetu hawa kumbe kinyume chake vifo vikaongezeka maradufu....
Yapo mambo ya kufanyia siasa, lakini Afya tusiifanyie siasa kama tulivyovuruga elimu yetu na kwingineko.
Na: Yericko Nyerere