Je, Youtube, Facebook na Instagram ndo Basi Tena kwa Watumiaji wa Huawei?

myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,612
6,153
Ukiwasikiliza watu kutokana na Google kuwafutia Leseni Huawei, wengi wao watakuambia; Simu bila Youtube; hapana aisee!!!

Kwanza nina kila sababu ya kuamini talaka hii ya Google kwa Huawei ni Talaka Moja a.k.a Talaka Rejea na wala sio Talaka Tatu, a.k.a Talaka Kwenda Mwana Kwenda! Lakini hata kama itakuwa ni Talaka Kwenda Mwana Kwenda, moja ya bidhaa ambazo watumiaji wa Huawei wanatakiwa kuhofia kutokuwa nazo sio YouTube!

Ni kweli, kama wataendelea kukaziana, Youtube App haitakuwepo kwenye Application Store ya Huawei. Hata hivyo, unlike Android kwamba ni "Wachina" ndio wamepigwa ban kuitumia, kwa Youtube, ni Wachina ndio wameipiga ban Youtube! Hii maana yake ni kwamba, pasipo na VPN, you can't access Youtube ukiwa ndani ya China Mainland!

Kwa maana nyingine, hata kama Youtube App haitakuwepo kwenye App Store ya Huawei, nina matumaini kwa wale tulio nje ya China tutaweza ku-access Youtube kwa kutumia web browser!

Lakini hata kama hatutaweza kui-access kwa kutumia web browser, tayari Wachina wana Youtube ya kwao tangia kitambo! Hii YouTube ya Kichina inaitwa YouKu.

Hapa tukumbushane kwamba, wasanii wana-upload kazi zao Youtube sio kwa sababu ni Youtube bali kwa sababu Youtube ndio largest video streaming platform kwa sasa! China wakishakuwa na video streaming platform international version, huko kutajaa mamilioni ya Video kama ambavyo zipo Youtube!

Lakini hata kwa sasa, ukiingia YouKu kuna kazi kibao za wasanii mbalimbali!

Hapa chini ni screenshot inayoonesha kazi za Diamond na zile alizoshiriki kupitia YouKu App (for PC)

YouKu.png

Hapo natumia app na sio browser, app ambayo Huawei wakishakuwa na OS ya kwao, hiyo YouKu ndiyo itapatikana App Store kama mbadala ya Youtube!

ANGALIZO: Kama ni mpenzi wa action movies na una bundle ya kuchungulia, tafadhali usi-visit YouKu kwa sababu utakumbana na ma-trailer ya movies za Kichina ambazo utashindwa kuacha kuziangalia!

Na kama you don't care characters wanaongea nini; kumejaa collection ya kutosha ya movie za Kichina pamoja na zingine za ukanda ule! Na uzuri ni kwamba, movies zingine zina English Subtitles.

Kwa sasa inaboa kidogo kwa sababu ni full Kichina! Na hili linaeleweka kwa sababu walitengeneza hizi alternative platform kwa matumizi ya Wachina na majirani zao! Wakati YouKu web unaweza kutumia Google Translate, YouKu App huwezi ku-translate menu zake!

Hata hivyo, hili sakasaka likiendelea, hawatakuwa na namna bali watalazimika pawe na YouKu English/International version!! Na jinsi Wachina wanavyopanua masoko yao, Huawei wakishika kasi tena kwa kutumia OS ya kwao, wasanii duniani hawatakuwa na namna bali nao watalazimika ku-upload kazi zao kwa wingi zaidi ili ku-serve soko la Huwaei users duniani kote!

Kwa Facebook, Whatsapp na Instagram! Labda kama hali itabadilika siku za usoni, lakini kwa hali ilivyo sasa kukosekana kwa Android hakutafanya watumiaji wa Huawei nje ya China washindwe kutumia hizo apps. Ni Wachina ndio wamezipiga marufuku nchini mwao hizo programu! Hiyo ina maana yake ni kwamba, App Store ya Huawei International Version itakuwa na apps za FB, Instagram na Whatsapp!

Athari ninayoiona kwa hili sakata ni kwa watumiaji wa Gmail, Google Suit na Google Map!

NOTE:Naipenda Honor View20 yangu si kwa sababu ya uwepo wa Android bali kutokana na utundu wa Wachina kwenye tech!

Mchina kokote uliko nami nipo!! Najua Honor series sio maarufu sana kwa Bongo but trust me, ni one of the best smartphones on the planet ingawaje kuinunua Honor View20 inabidi ujipange kidogo!
 
Weee hao google walifanikiwa kuisambaratisha blackberry na ZTE unafikiri mchezo...hii game wachina kama wajanja na brave enough wachutame tu mambo yaende la sivyo wanapotea vibaya mno.

Leo hii mchina ana reserve ya US dollar kubwa kuliko US mwenyewe halafu anajiona yuko safe? Wale wanaweza amua kuprint pesa yao mpya na wakatangaza kurefund soko na pesa isipokuwa zile za China tu matokeo yake yatakuwa kufilisika kwa China maana wana pesa ambazo hazitumiki kwenye soko halali la Dunia.

The one and only Super Power ni USA sisi wengine tuchutame tulishachelewa na jamaa hawapo tayari kuruhusu fahari mwingine ainuke na kuwatikisa. We tazama bifu la US market na EU market lilipoishia, wazungu na umoja wao walichutama na mwanaume hajatengua maamuzi yake hata robo leo hii aluminium inaingia US kwa kodi kubwa sana so inawalazimu wauze bei ya juu na jamaa wanazo za kwao wanauza bei chee hapo taayri EU wanaweweseka hatari.
 
Huawei kwa upande wa simu ndio kama ishajifia kama trump ataendelea kuwaekea ngumu.

1. SoC yake ya Hisilicon inatumia arm architecture inayomilikiwa ARM holding ambao nao wamefata mkondo wa google.

Ingewezekana kutumia x86 au 86-64 lkin platform za intel na amd amabo ni za USA.

Kwa hiyo hata hizo chip zake za kirin ndio basi

Kumbuka hawa jamaa ARM na INTEL ni ngumu sana kuwaepuka kwenye uundaji wa processors.

2. AOSP(android open source project) ambayo ni ruksa kutumia imeundwa kwa kutegemea platform za ARM na InTel

3. Sio rahisi OS mpya kuweza kudominate soko na kupambana na android

Mfano mzuri samsung wana os yao ya tizen na simu zipo zinazotumia tizen ila imeshindwa kuipa changamoto yoyote android kwa kipindi cha miaka 5 toka ianzishwe.

3. Huawei hawatotumia Wi-Fi kwa sababu Wi-Fi alliance imeweka zuio la muda kwa huawei kutumia standards zao, je kuna mbadala wa wi-fi kwenye wireless network?

4. Huawei hawatotumia SD card na micro sd card, japokuwa hili linaweza lisiwe na madhara makubwa kwa sababu huawei wana cards zao ambazo ni nano card.

5. Huawei imebidi wajiotoe wenyewe toka JEDEC hawa wana jukumu la uundaji standards za ram.

Swali, Huawei wanaweza kuunda kila kitu wenyewe bila kutegemea makampuni mengine?.

Ni ngumu sana kwa upande wa tech.
 
Akili kubwa inahitajika.
 
Back
Top Bottom