Je yote yanawezekana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je yote yanawezekana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rafiki2010, Oct 4, 2010.

 1. r

  rafiki2010 Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado ni jambo linaloniumiza kichwa nikitafakari kwa kina ,,,, ukweli ni kwamba tanzania iliyo hai haiwezekani bila kuwa na elimu bora ni wazi ya kwamba inagharimu pesa nyingi ili kufanikisha watanzani wanapata elimu mathubuti,,,,,, na niwazi kuwa watanzania walio wengi ni watu wenye kiwango cha chini kiuchumi ndio maana kukawepo na uchangiaji mdogo wa shule za serikali ambayo ni sawa na bure,,,,,, na kuanzishwa kwa bodi za mikopo kwa watu wilio vyuoni ,,,,,,

  SERA ZA CHAMA FULANI ZINANADI SERA ZAO KWA KUWAAHIDI WANANCHI ELIMU BURE ..

  Embu watanzania tuwe wawazi na kufikiria kwa undani idadi ya wanafunzi wanaohitaji kupatiwa elimu hiyo ukiwianisha na uchumi wa nchi yetu,,,,,, mfano halisi mbali kwa nchi kama botwana iliyo kuwa ikiwapatia wananchi wake elimu bure sasa imekiri kushindwa kuendelea na zoezi hilo iwapo ni nchi yenye mafanikio makubwa kiuchumi kuliko tanzania ,,,, sasa je kwa nchi kama tanzania itawezekana kutoa elimu bure au ndio campain za kutaka kuingia ikulu ,,,, nduga zanguni tuwe makini maamuzi yetu OCTOBER 31st ,, KWANI MAAMUZI SAHIHI HUTOLEWA MUDA SAHIHI NA WATU SAHIHI KWA MANUFAA YA UMA NA TANZANIA KWA UJUMLA ,,, HUSHIMU KURA ewe kijana,,mzee,,baba ,, mama

  TANZANIA YENYE MAENDELEO HUJEMGWA NA WATANZANIA WENYEWE
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Bwana mdogo haya mambo yanawezekana watu walishapiga mahesabu yao. Hata kwa kuweka mfuko wa kuchangia elimu tutachangia tuu, chama flani unamaanisha chadema na cuf? Yes kama wameonyesha moyo wa hivyo tupotayali kikubwa nikuupinga ufisadi ambao ccm wameung'ang'ania utadhani wamezaliwa nao.
  Nimeona nikujibu sababu umeniumiza saana.toa kura yako kwa chama chochote isipokuwa ccm tu imeshindwa kwa kila kitu.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  Elimu bure inawezekana kabisa bila zengwe kabisa. Wenye migodi mikubwa kutokana na mikataba feki ya CCM wanapata misamaha ya kodi yenye jumla ya Tshs 700 bilioni kwa mwaka. Hawalipii hata kodi ya mafuta na hivyo kupata ruzuku ya barabara ambazo magari yao yenye uzito wa kupindukia yanapita na kuziharibu. Hivi kama mama ntilie analipa kodi tuna sababu gani mgeni tumpe ruzuku na asichangie maendeleo ya nchi hii? Huyu ni mwekezaji au ni bomu la kutupwa?

  Vyuo vikuu ili kila mwanafunzi apate mahitaji yake tunahitaji bilioni 38 tu kwa mwaka kama nyongeza kwenye bajeti iliyopo CCM wanasema hilo haliwezekani. Lakini chini ya utawala wa Chadema Dr. Slaa ameahidi kuifuta misamaa hiyo ya kodi na wanafunzi wa vyuo vikuu wote watapata mikopo kulingana na gharama halisi za maisha.

  Shule ya msingi na elimu ya sekondari hadi kidato cha sita ili wanafunzi wote wasome bure na kupata mahitaji yao yote nyongeza ya Tshs bilioni 400 yahitajika kwenye bajeti CCM wanasema haiwezekani. Lakini kwa kufuta misamaha ya kodi, Dr. Slaa anasema hilo la elimu ya msingi hadi kidato cha sita yawezekana kwa bwerere na bila zengwe lolote.

  Suala hapa siyo kuwezekana bali ni utashi wa kisiasa unakosekana kabisa. CCM wapo mbele katika sera zao za utajirisho wa viongozi na ndiyo maana pale Bw. Chenge alipoulizwa juu ya kurundika mapesa nje alijitetea: mbona hivyo ni "vijisenti" - akimaanisha asibughudhiwe kwa sababu yeye ni mwadilifu akijilinganisha na vigogo wengine ndani ya CCM. Hadi leo, Bw. Chenge hajaguswa kwenye kashfa ya "radar" kwa sababu ulafi uliopo ndani ya CCM unawazuia wote viongozi kuwajibishana linakuwa ni swala la nani amvike paka kengele wakati sote ni paka?

  Kwneye maandiko matakatifu imeandikwa:-

  CHAGUA DR. SLAA................CHAGUA CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  The Following User Says Thank You to Rutashubanyuma For This Useful Post:

  Mchukia Fisadi (Today) ​
   
 5. giraffe

  giraffe JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 504
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Dr Slaa anatisha sana
   
Loading...