Je, yawezekana hii kashfa ya mawaziri ni kutimia kwa unabii wa Dr Jakaya Kikwete? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, yawezekana hii kashfa ya mawaziri ni kutimia kwa unabii wa Dr Jakaya Kikwete?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ishaka, Apr 22, 2012.

 1. Ishaka

  Ishaka Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 1, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Nakumbuka, mara baada ya kuapishwa baraza la mawaziri katika viwanja vya ikulu, Rais Kikwete aliwaasa mawaziri wake akisema "...mkizembea, ipo siku tutakabidhi nchi kwa wapinzani". Ni dhahiri aliijua dhamiri safi ya dhati ya wapinzani tishio wa ccm ambao kwa hakika ni mtetezi makini,tumaini na nuru ya watanzania kuelekea Ukombozi kamili wa uchumi wao.
  Sasa ukweli umejulikana, Mungu wa Israel yuko upande wa wapinzani, na kila mwenye pumzi amche Bwana Mungu wake ili tuweze kuvuka makaburi tunayochimbiwa na mafisadi tufike salama katika maisha mazuri tuliyokusudiwa na Mungu. Mimi nilikuwa sijaelewa vizuri vuguvugu la kutaka nchi yetu iwe na sheria inayoruhusu kuwa na uraia wa nchi mbili! sasa naanza kupata majibu...watu wamehamishia utajiri wetu katika nchi hizo wanazozitaka kuwa raia! sasa Mungu kawafunua na tutarajie kuona mengi, hiyo ni trela tu. Mabadiliko ni lazima, tuache uoga tuige mfano wa Mwl Nyerere wakati akidai uhuru wa taifa hili maana haikuwa kazi rahisi mkoloni kusalimu amri, lakini ilibidi.
  Pamoja tunaweza, utaifa mbele. Mungu ibariki nchi yetu Tanzania na wabunge mashujaa "G70"
   
Loading...