Je, Yanga SC itakuwa imefanikiwa hata wakishindwa taji la kombe la shirikisho barani Afrika?

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Kwa kuwa mafanikio yanaweza kutofautiana kulingana na malengo ya kila klabu, napenda kusema kuwa ni suala la mtazamo. Kwa mfano, ikiwa Yanga SC ilikuwa na lengo la kufika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Afrika, basi bado inaweza kuchukuliwa kama mafanikio ikiwa itafanikiwa kufanya hivyo.

Hata hivyo, kwa upande mwingine, ikiwa lengo la Yanga SC lilikuwa ni kutwaa taji la Kombe la Shirikisho la Afrika na hawakufanikiwa kufanya hivyo, basi inaweza kuhesabiwa kama kutofikia malengo yao.

Ni muhimu kutambua kuwa mafanikio ya klabu ya mpira wa miguu yanaweza kuwa ya kiwango tofauti kulingana na malengo, historia, na hali ya klabu. Yanga SC ni klabu kubwa na kongwe sana nchini Tanzania na Afrika Mashariki, na kwa hivyo ina mashabiki wengi wanaotarajia mafanikio makubwa.

Hata hivyo, mpira wa miguu ni mchezo ambao hauwezi kudhibitiwa kabisa, kwa hivyo mafanikio yanaweza kutofautiana kutoka msimu mmoja hadi mwingine.

20230603_004046.jpg
 
Mafanikio kutwaa taji tu tofauti hapo utakuwa hauna tofauti na azam au Geita kwa kuwa nyote mtakuwa mmeshiriki kombe la looser na nyote mmefeli kunyakua kombe.

ACHENI KUJIFARIJI KWA KAULI ZA KIPUMBAVU.
Sawa kumbe hao Azam na Geita nao watapata gawio kama Yanga atalopata akiwa mshindi wa pili. Pia watakua wameweka historia Nchini kadhalika watakuwa wamepewa ndege na Mkuu wa Nchi kwenda kushiriki Fainali. ____
 
Malengo ya Yanga yalikuwa kufika angalau makundi tu Klabu bingwa Afrika ( CAFCL ) lakini waliishia raundi ya pili wakaangukia loosers cup. Kwa kifupi hata wakichukua CAFcc ni kwamba wamefeli Maana hayakuwa malengo yao kucheza loosers cup.

Hata hivyo bingwa wa Afrika ni mmoja tu . Atakaeshinda Kati ya Wydad vs Aly Ahly. Hawa wenzangu na mimi wa CAFcc ni wapambe tu wa bingwa wa CAFCL .
 
EWE MWANANCHIIIII HAKIKA LEO NI SIKU AMBAYO TUNAENDA KUUDHIHIRISHIA ULIMWENGU KWAMBA YANGA NI KUBWA KIASI GANI NA TUNA UKUBWA KIASI GANI KATIKA SOKA.
NAJUA KUNA WATU HAWATA PENDA HISTORIA TUNAYOENDA KUIANDIKA LEO HII.

NIKUOMBE TU KAMA HUNA USTAHMILIVU NA TIMU YA YANGA USIANGALIE MECHI YA LEO.
MECHI HII NI KWA AJILI YA WABOBEZI WA SOKA.
💚💛💚💛💚💛💚💛💚💛💚💛
 
Kila mtu ana njia yake ya kupima mafanikio kulingana na malengo aliyojiwekea ....yanga waliweka malengo ya kufika makundi lakin wamevuka mpk fainali hii inaonesha wamezidi malengo yao si mbaya kusema WAMEFANIKIWA
 
Muda unazidi kuyoyoma wa mwarabu kwenda kufanya yake.
 
Mafanikio yao itakuwa ni kutazama hiyo game kwenye big screen wajione wanavyoloweshwa na mwarabu.
 
Kwa kuwa mafanikio yanaweza kutofautiana kulingana na malengo ya kila klabu, napenda kusema kuwa ni suala la mtazamo. Kwa mfano, ikiwa Yanga SC ilikuwa na lengo la kufika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Afrika, basi bado inaweza kuchukuliwa kama mafanikio ikiwa itafanikiwa kufanya hivyo.

Hata hivyo, kwa upande mwingine, ikiwa lengo la Yanga SC lilikuwa ni kutwaa taji la Kombe la Shirikisho la Afrika na hawakufanikiwa kufanya hivyo, basi inaweza kuhesabiwa kama kutofikia malengo yao.

Ni muhimu kutambua kuwa mafanikio ya klabu ya mpira wa miguu yanaweza kuwa ya kiwango tofauti kulingana na malengo, historia, na hali ya klabu. Yanga SC ni klabu kubwa na kongwe sana nchini Tanzania na Afrika Mashariki, na kwa hivyo ina mashabiki wengi wanaotarajia mafanikio makubwa.

Hata hivyo, mpira wa miguu ni mchezo ambao hauwezi kudhibitiwa kabisa, kwa hivyo mafanikio yanaweza kutofautiana kutoka msimu mmoja hadi mwingine.

Unakuwa umefanikiwa nini kzma umerudi mikono mitupu bila kombe? Uzi wa kipumbavu huu!
 
Yanga kuleta kombe itakuwa ni sawa na mama samia leo hii aache urais eti aende chadema akagombee uenyekiti
 
Kila mtu ana njia yake ya kupima mafanikio kulingana na malengo aliyojiwekea ....yanga waliweka malengo ya kufika makundi lakin wamevuka mpk fainali hii inaonesha wamezidi malengo yao si mbaya kusema WAMEFANIKIWA
Makundi ya mashindano yapi? CAFCL au CAFcc? Kama malengo yalikuwa ni makundi CAFCL na hawakufika basi wamefeli. Tuwe tu wawazi.
 
Makundi ya mashindano yapi? CAFCL au CAFcc? Kama malengo yalikuwa ni makundi CAFCL na hawakufika basi wamefeli. Tuwe tu wawazi.m
Makundi ya champions league walifeli wakaja na plan B ya makundi alya shirikisho huko wakafaulu...sawa hatuwapendi Ila kumpongeza mtu ni njiaa ya kujifunza
 
Malengo ya Yanga yalikuwa kufika angalau makundi tu Klabu bingwa Afrika ( CAFCL ) lakini waliishia raundi ya pili wakaangukia loosers cup. Kwa kifupi hata wakichukua CAFcc ni kwamba wamefeli Maana hayakuwa malengo yao kucheza loosers cup.

Hata hivyo bingwa wa Afrika ni mmoja tu . Atakaeshinda Kati ya Wydad vs Aly Ahly. Hawa wenzangu na mimi wa CAFcc ni wapambe tu wa bingwa wa CAFCL .
Duh akili hizi, huenda ni baba mwenye familia
 
Back
Top Bottom