Je, yanayoendelea Kibiti ni ishara ya kupimwa kwa hali ya usalama wetu?

abdulrahim

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
408
286
Habari Wakuu!

Binafsi natamani kujua nini kiini cha mauaji yanayoendelea kibiti kila kukicha. Pia nashindwa kuelewa na kuamini kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kushindwa kutambua wauaji,Chanzo cha mauaji na kuthibiti hali hiyo.

Kwa namna moja ama nyingine binafsi hali hii naweza kuifananisha na kipimo cha hali ya ulinzi na usalama wetu nchini. Ikiwa tumekuwa tukisikia kwamba Tanzania ni nchi miongoni mwa nchi zilizo salama, Inakuaje kikundi cha watu kinaendelea kutekeleza mashambulio pasi na vyombo vya usalama kutoa taarifa sahihi na kuthibiti kwa muda muafaka..

Nawasilisha!!
 
kama ni kikundi tu kimeamua kutekeleza mauaji hayo na yanafanikiwa sizani kama wa mikoa mingine uku tupo salama.nakinachoendelea ni kuwatamanisha maana watakuwa wanaona wanaweza kufanya lolote na popote...
 
Kwa namna moja ama nyingine binafsi hali hii naweza kuifananisha na kipimo cha hali ya ulinzi na usalama wetu nchini. Ikiwa tumekuwa tukisikia kwamba Tanzania ni nchi miongoni mwa nchi zilizo salama, Inakuaje kikundi cha watu kinaendelea kutekeleza mashambulio pasi na vyombo vya usalama kutoa taarifa sahihi na kuthibiti kwa muda muafaka..

Personally nashindwa kuwaelewa watu wa intelijensia kwanini hili swala limekuwa gumu kwao
 
Tatizo ni Serikali baada ya kukaa na wananchi ili kulimaiza jambo hili wao wanatuma Police ambao wanaliendea jambo hili kwa Jazba mwisho wa siku wanauwa na kuuwawa kwaiyo watu wanaishi kwa kulipizana kisasi!!
 
Usalama wetu ni mdogo sana.

Zile bunduki walizoporwa askari waliposhambuliwa kwa kushtukizwa na kuuawa pale mwandege hazijapatikana mpaka leo!!!

Kina ****** wanataka et askari waonyeshe uaskari wao kwenye kuwatoa wabunge nje ya bunge.
 
Ubabe Wetu Nikuwatuliza Wapinzani Sbb Ndyo Adui Wa Usalama Wetu Nakuwatuliza Bungeni Kwa Nguvu Wasijewakatembeza Mkongoto Hadi Kwa Spika,,,huko Kwngneko Big No Tumeshndwa
 
Back
Top Bottom