Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Amani iwe kwenu wadau!
Kwa kumbukumbu zangu kuna mabadiriko ya sheria yaliyohusisha Fedha za zao la korosho na vyama vya ushirika. Mabadiriko yale yalipingwa vikali sana na wabunge wa kusini akiwemo Nape na kupelekea Hawa Ghasia kutumia diplomasia kujiuzuru uwenyekiti wa kamati moja ya Bunge. Serikali kutaka Fedha za korosho ililazimisha, Kilichofuata ni kuharibika kwa soko na biashara ya zao la korosho. Saivi hakuna anayethubutu kusema chochote kuhusu zao hili.
Ilifuata suala la Fedha za halmashauri/ Mapato yake kwenda Serikali Kuu. Kilichofuata ni halmashauri kushindwa kujiendesha na nyingi ziko hoi.
Funga Kazi ni hili la bajeti ya mwaka huu, Fedha za Tanapa, Tawa na Ngorongoro kwenda Serikali kuu. Hii inamaanisha wale jamaa wakitaka hata hela za kurekebisha lodge zao, barabara za Mbugani na mazingira ya mbugani itabidi waombe hela kutoka Serikali kuu na zifuate mchakato uleule kama ofisi zingine za Serikali ambazo zikiombaga hela huwa kama sio zinachelewa kwa miezi basi hazipewi kabisa.
Je, kwa marekebisho haya, Huu ndo mwisho wa kuendelea na kustawi kwa Sekta ya Utalii Tanzania?
Waliopendekeza marekebisho haya hawajajifunza kwenye Halmashauri na Kwenye korosho kusini?
Mwisho naisi kuna mtu anataka aonekane anavunja rekodi ya makusanyo kumbe hakuna lolote. Anachofanya ni kuzielekeza tu Fedha zote ziingie serikali kuu kupitia TRA jambo ambalo nina uhakika hata Kikwete angefanya tena kwa jinsi alivyostawisha uwekezaji, makusanyo kwa mwezi yangekuwa hata Trilioni 3
Ijumaa Kareem!