Je, wezi wa Wizara ya fedha wameshafahamu aina ya Rais tuliyenaye?

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,698
4,693
Kwa wakulima wa mahindi na mpunga, tunaelewa uharibifu wa nyani na tumbili na ndege. Huwa tunaanza kuweka matambala na kichwa cha bandia ili wanyama hawa waamini huyo ni mlinzi.

Wanyama polepole huanza kuzoea na kugundua kwamba hayo ni matambala na hakuna kichwa, ni chungu cheusi. Hapo sasa mazao huanza kuliwa.

Tumeanza kuona wizi na ulaji wa hovyo. Tena ndani ya wizara mama yenye kushikilia hazina ya taifa na nchi. Wizara ya Fedha wanaanza kuikomba nchi kweupeee! Hisia yangu hawa ni nyani waliogundua kwamba hatuna tena mlinzi wa fedha ya umma. Rais wetu utajua mwenyewe! Kama nawe una maneno yale ya kusema nchi hii utaiacha kama alivyoiacha Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Magufuli. Aliyesema simtaji.

 
Hii ofisi nayo kama iko kisiasa zaidi huwa inamfavor yule aliyemweka madarakani na mara nyingi sio wakweli!
na katika hili hata Professor Assad aliingia mtego huu wakati wa Kikwete hakuzungumza mabaya awamu ya tano akayaona mabaya.
huyu mwingine woga wa kukosa kazi na tamaduni za kujikombakomba zinafanya pia aponde kila kitu.
njaa bado ni tatizo kwa taaluma zetu!
VOTE ya ikulu ni kichaka haikaguliwi mzee, huko ndiyo wanakopigia pesa
 
Kwa wakulima wa mahindi na mpunga, tunaelewa uharibifu wa nyani na tumbili na ndege. Huwa tunaanza kuweka matambala na kichwa cha bandia ili wanyama hawa waamini huyo ni mlinzi. Wanyama polepole huanza kuzoea na kugundua kwamba hayo ni matambala na hakuna kichwa, ni chungu cheusi. Hapo sasa mazao huanza kuliwa.

Tumeanza kuona wizi na ulaji wa hovyo. Tena ndani ya wizara mama yenye kushikilia hazina ya taifa na nchi. Wizara ya Fedha wanaanza kuiokomba nchi kweupeee! Hisia yangu hawa ni nyani waliogundua kwamba hatuna tena mlinzi wa fedha ya umma. Rais wetu utajua mwenyewe! Kama nawe una maneno yale ya kusema nchi hii utaiacha kama alivyoiacha Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Magufuli. Aliyesema simtaji.

View attachment 1800357
Hii typicaly ndiyo yalikuwa maisha kipindi cha utawala wa Kikwete. Maofisini watu walikuwa wanatafuta visingizio vya kulipana posho. Mheshimiwa Samia asipokuwa makini na mkali hali inaweza kuwa mbaya hata zaidi ya kipindi cha Kikwete.
 
Back
Top Bottom