Lord OSAGYEFO
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 3,086
- 4,881
Wacha wajichotee mbona kina HALIMA Mdee na GENGE lake Wanaiba Mishahara?Kwa wakulima wa mahindi na mpunga, tunaelewa uharibifu wa nyani na tumbili na ndege. Huwa tunaanza kuweka matambala na kichwa cha bandia ili wanyama hawa waamini huyo ni mlinzi. Wanyama polepole huanza kuzoea na kugundua kwamba hayo ni matambala na hakuna kichwa, ni chungu cheusi. Hapo sasa mazao huanza kuliwa.
Tumeanza kuona wizi na ulaji wa hovyo. Tena ndani ya wizara mama yenye kushikilia hazina ya taifa na nchi. Wizara ya Fedha wanaanza kuiokomba nchi kweupeee! Hisia yangu hawa ni nyani waliogundua kwamba hatuna tena mlinzi wa fedha ya umma. Rais wetu utajua mwenyewe! Kama nawe una maneno yale ya kusema nchi hii utaiacha kama alivyoiacha Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Magufuli. Aliyesema simtaji.