Je, wezi wa Wizara ya fedha wameshafahamu aina ya Rais tuliyenaye?

KWA MAWAZO YANGU TATIZO NI KATIBA , KATIBA, KATIBA. KWA DHAMANA ANAYOPEWA RAIS KUCHUKUA REHANI YA ROHO ZOTE MFANO LEO TZ KAMA ROHO MIL.60. ILIPASWA RAIS AWEKEWE KIBANO KIKALI KIKATIBA HATA WANAOTAKA URAIS WANGEJIPIMA NA KUJIULIZA SANA KABLA YA KUGOMBEA. KWA SASA RAIS ANAWEZA HATA KUIUZA NCHI, KUTUUZA, KUTUCHINJA HATA ASIULIZWE NA YEYOTE. NI HATARI! . KWA NYAKAZI ZA LEO KILA CHOMBO CHA DOLA/NCHI KINAPASWA KUANGALIWA NA KINGINE HATA MAHAKAMA. YAANI KUANGALIANA TU HAIJALISHI WEWE NANI. WEWE NI NANI IWE HAKI TU. HII KATIBA YA SASA ILIMFAA NYERERE PEKE YAKE KUIKUSANYA NCHI KWA USAFI NA UZALENDO WAKE KAMA BABA WA TAIFA.
 
Repoti ilikuwa na matobo ile....!!!

Mfano. Taasisi ama shirika la umma linaandikiwa hati chafu kwa kutumia fedha za umma kwa weledi...hilo lilikuwa tobo. Badala ya taasisi kupongezwa inalimwa hati chafu. Najua utashangaa!

Nakueleza sasa.
====
Kuna mashirika yalilimwa hati chafu kwa sababu yamenunua magali mawili au matatu yenye umbo la kawaida lakini magari hayo ni imara sana na gharama za uendeshaji magari hayo ipo chini sana badala ya kununua gari moja lenye umbo la kuvutia lenye mapambo yanayoharibika baada ya muda mfupi na vifaa vyake vingi siyo imara pia gharama za uendeshaji gari hilo ipo juu mara dufu kulingalinisha na jumla ya gharama za uendeshaji magari mawili matatu. Kumbuka gari moja la umbo zuri lina uwezo wa kubeba abiria ama mzigo sawa na gari moja la kawaida.

Sababu wanazotoa nikuwa eti taratibu za manunuzi hazikufuatwa kwasababu taratibu ilikuwa kununua gari moja zuri ambalo siyo imara! Hii yote ni kwa sababu taratibu nyingi za manunuzi na fedha zimefungamana na taratibu za baadhi ya wafadhili ama wakopeshaji ambao hawafurahii fedha zao wanazofadhili ama kukopesha zinatumika kwa tija. Hawafurahii kwa sababu fedha zao zikitumika kwa tija, sisi kama nchi tutaacha kuwapigia magoti kuomba ufadhili ama mikopo jambo ambalo litawakosesha soko la fedha zao kufadhili ama kukopesha.
===
Ukisoma report ya cag kwa macho mawili utagundua kuwa kulikuwa na wizi wa kutisha, lakini ukiisoma kwa jicho la tatu utagundua ufafanuzi unaofafana na mfano niloelea hapo juu.
Mkuu hayo magari yalikuwepo kwenye budget? pia kwani mlishindwa kunini kuomba kubadilisha matumizi kwa kibali cha KM wizara ya fedha?
 
Ushabiki upi sasa?hata kipindi cha jiwe pesa inakuwa ikiliwa tu, lakini nani alikuwa na uwezo wa kusema?kwani sasa ukiibuka upigaji utasikia "wapigaji wameanza"!!! Kwani waliisha lini?wapigaji wapo tu na wataendelea kupiga kutokana na mfumo wa kulindana uliopo ndani ya ccm.
Hao ccm wenyewe waulize ndani ya chama alichowafanyia Mwendazake watakwambia Kama walikua wanapiga.kiukwel ana weakness zingine lkn wezi JPM walimuogopa sana.ilikua mbinu Sana uweze kumuibia sio kiboya Kama ivi
 
Kwa wakulima wa mahindi na mpunga, tunaelewa uharibifu wa nyani na tumbili na ndege. Huwa tunaanza kuweka matambala na kichwa cha bandia ili wanyama hawa waamini huyo ni mlinzi.

Wanyama polepole huanza kuzoea na kugundua kwamba hayo ni matambala na hakuna kichwa, ni chungu cheusi. Hapo sasa mazao huanza kuliwa.

Tumeanza kuona wizi na ulaji wa hovyo. Tena ndani ya wizara mama yenye kushikilia hazina ya taifa na nchi. Wizara ya Fedha wanaanza kuikomba nchi kweupeee! Hisia yangu hawa ni nyani waliogundua kwamba hatuna tena mlinzi wa fedha ya umma. Rais wetu utajua mwenyewe! Kama nawe una maneno yale ya kusema nchi hii utaiacha kama alivyoiacha Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Magufuli. Aliyesema simtaji.


Kwani ile ripoti ya CAG aliyoiagiza mama toka BOT na TPA Jan -March 2021 inasema je?
 
Back
Top Bottom