Je, Wewe upo 'Tight' kwenye fani au kazi gani?

maishapopote

JF-Expert Member
May 28, 2009
3,241
5,349
Wakuu, Nimeona nilete hii Mada hapa naamini Itatusaidia Wengi sana. Kama kuna kitu unaamini unakijua, na kukielewa kiundani, iwe kielimu au kwa uzoefu! ningependa ukiweke hapa na mtu anaweza kukuuliza swali ukamsaidia chochote kile

Mimi Nafahamu Kidogo kuhusu;

1: Ujenzi, Architecture, Biashara na Connection

2: Nina uzoefu kwenye ushauri wa Ndoa, Mahusiano, Biashara na maisha ya kupambana

3.kubadilisha nafasi kuwa hela,kuweka bidhaa mpya sokoni, bible history kidogo...na crime in general

Tukubaliane kusiwe na masihara tutasaidiana sana
 
1)Mimi mwalimu wa Geography nipo njema kwenye Geography nitandike swali lolote la Geography nitakujibu.

2)Mwana mazoezi Gym niulize chochote kuhusu mazoezi hasa ya kunyanyua vyuma (Free Weight).
 
Natamani Sana kujua elim ya mitishamba. Kama Kuna naeweza kunisaidia naomba anipe mwanga.

Naamini nyuvu ya Mungu ipo katika Nature ila tumepumbazwa mahali
Mkuu Miti shamba ina mambo mengi hatuyajui.

Case no.1 ukiwa umevunjika mguu, ukishawekwa pop au zile chuma nenda kwenye maduka haya ya Kiislamu ya kienyeji. Kuna dawa inaitwa mumiani nunua ni nyeusi tii. Sharti lazma uichanganye kwenye supu ya kuku ndo uinywe unakunywa mara tano au sita. Wiki mbili tu mfupa umeunga

Case no 1. kuna dawa naijua ukiikamua iko kama mlenda, hiyo dawa kama unaharisha damu ukinywa inakata hapo hapo yaani kama uchawi

Case no 3. kuna watoto wanakua na hizi tezi permanent kama vile wako infected na ugonjwa mjubwa sana, ukimgusa mtoto kwa nje chini ya taya unakuta zimevimba, kuna mti kule Moshi unauzunguka mara kumi then hugeuki nyuma kesho yake yanapotea.


Shida kubwa ya miti shamba ni kwamba elimu yake inapotea kwa kasi sana na watu wengi hawapendi miti shamba.
 
mkuu watu wa hivyo wapo ila wanataka wenyewe,mara nyingi wakiamua wanafanikiwa mapema mno maana wana connection nyingi sana
Mtu kama mwalimu.

Imagine.anachosema gent, swala la kukumbukwa lisiwe kama wajibu bali iwe ni kama shukrani, ndio itapendeza zaidi lakini wakabaira hawafanyi hivyo. Kama haitoshi ndio kwanza wanatoa matamko ya hovyo sana kuwahusu.

unakuta mtu kwa ujasiri kabisa anaandika,si uende hata ualimu.
 
mtu kama mwalimu.

imagine.anachosema gent,swala la kukumbukwa lisiwe kama wajibu bali iwe ni kama shukrani,ndio itapendeza zaidi lakini wakabaira hawafanyi hivyo.kama haitoshi ndio kwanza wanatoa matamko ya hovyo sana kuwahusu.
Mkuu tutembee kwenye mfano wako huo huo, hivi tujiulize ukweli ni walimu wangapi wamefanikiwa kimaisha? walimu wanajuana na watu wangapi? mwalimu unakuta hana hata kabiashara ka pembeni..hata tuition kweli? yeye ni kufundisha tu basi hapana imagine madoctor walivyo busy lakini wana biashara pembeni, tunachosema watu wengi hawatumii nafasi za connection walizonazo kwenye maendeleo.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom