je wewe unapenda kukumbushwa enzi za primary mkikutana na classmate wako? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

je wewe unapenda kukumbushwa enzi za primary mkikutana na classmate wako?

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by mnyikungu, Jul 6, 2011.

 1. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 581
  Trophy Points: 280
  jamani leo nimecheka sana sababu nimekutana na classmate wangu wa primary nikawa nimemsahau jina ila nikawa nalikumbuka jina la enzi za shule nilipomwita jamaa alikasilika kweli, lakini si huyo tu kuna mwingine hapendi kukumbushiwa mambo ya primary sababu alikuwa anajikojolea darasani. mimi binafsi napenda sana coz yananifurahisha mno. je wewe unapenda kukumbushiwa ya primary? au ukikumbushiwa unarusha ngumi?
   
 2. Da Pretty

  Da Pretty JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 3,050
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Nasikia raha sn nikiwaza utoto na vituko tulivyofanya!
  Kuna wakati natumia muda mwingi kwenye page yetu ya primary mtandaoni! Yani kama tunaonana vile! Kwangu ni raha na kiukweli yapo mabaya wengine hawapendi kukumbushwa,kama mtu mwenye akili timamu cwezi kumkumbusha cku aliyofanya jambo baya lolote la kumdhalilisha.
  Nafurahia!
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Aaaa,napenda sana,huwa siku za weekenda nawatumia sms rafiki zangu kuwakumbusha mambo ya primary enz hzo tulikuwa tunakaa kwenye vumbi tukiwa classs
   
 4. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2011
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 581
  Trophy Points: 280
  yaani nikikutana na classmate fulani hivi huwa nacheka sana maana alichowahi kunifanyia ni fedheha lakini kwa sababu ya uprimary hata ckujari

   
 5. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  tulisoma darasa la udongo,madirisha yalikuwa kama milango ya dharura!!!!! nikikumbuka huwa stresses zinapungua kiasi,
   
 6. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Kuna Bwe.ge mmoja, alikuwa mkubwa kwangu wakati ule na alikuwa anapenda kweli kunionea..
  Yaani nikimuona tu nilikuwa nalazimika kukimbia, la sivyo nachezea kichapo...
  Alishaninyang'anya sana Asikirimu na sambusa kila akinikuta nazo..
  Nilikuwa nalazimishwa kumpa majibu ya mitihani na ole wangu afeli hata kama tumefeli wote ananipa kibano..
  Kilichokuwa kikiniuma zaidi ni pale alipokuwa anampiga mdogo wangu eti kisa alitaka kunipiga nikakimbia..
  Nimekuja kukutana naye Ukubwani, eti anajifanya ameokoka.
  Alinikera zaidi nilivyomkumbusha jinsi alivyoninyanyasa akajifanya hakumbuki...
  Mpaka leo nina usongo naye nataka angalau aniombe radhi kwa mateso aliyokuwa ananisababishia..
  Vinginevyo nataka nimpe kichapo ili ajue uchungu wake manake sasa hivi ninammudu vyema..
   
 7. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,896
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Aisee mm niomekuta na mmoja jana, imekuwa miaka 19 tangu tuonane! Hatukuzungumzia sana ya zamani ila sikumbuki tuliachana vp, tulikata kilaji acha kabisa. Ila ni furaha sana!
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Nakumbuka nikiwa darasa ka pili kuna jamaa akiitwa Evodi huyu jamaa alikuwa anacheza mpira balaa, na mara nyingi walikuwa wanatufunga.
  Ilikuwa kila recess(mapumziko tunakipiga chandima drs la pili na la tatU) Jamaa alikuwa anaaminika apigwi chenga. Basi kuna siku tunacheza nao saa sita hiyo mapumziko tuko moja moja mpira ukanijia nikaweka pajani nikatisha kushota jamaa akajaa kushoto mie nikapita kulia, akaja beki mwingine nikampiga tobo halafu nikamwona kipa anajitayarisha kuja nikafumba macho nikapiga ule mpira kwa dochi kwa kasi ukaingia golini ikawa mbili moja na kengele ikagonga tukarudi darasa aisee nilikuwa celebrity ghafla
   
 9. X-not

  X-not Member

  #9
  Jul 7, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahaaaaa! dah mnenikumbusha mbali kweki!
   
 10. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2011
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 581
  Trophy Points: 280
  pole sana mi mwenzio nilikuwa wa kwanza kupiga kwahiyo alikuwa hanionei mtu.
   
 11. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli ni vizuri ila kwanini umkumbushe mtu mambo ya kuwa kikojozi kwa wewe itakusaidia nini sasa?
  Kama hauna makumbusho ya mambo ya wote kucheka basi bora unyamaze. Mtu kua kua

  Kwa mimi nilikuwa na jina la utani madarasa yote shuleni namaanisha primary yote. walikuwa wananiita nilitungiwa la kichekesho tu as niliongea neno nikakosea basi likawa ndilo langu hadi leo ila.
   
 12. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2011
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 581
  Trophy Points: 280
  sina maana kuwa umkumbushe mtu ukikojozi wake la hasha! ila watu wengine hawapendi kukumbushia mabo ya shule sababu wanahisi kama hata mabaya yao utayakumbushia, lakini hata hivyo kama mliyosoma naye ni mtani wako hiyo haina ubaya, maana hata mimi kuna mtu tukikutana naye huwa tunakumbushiana kila kitu.
   
Loading...