Je, wewe una phobia (uoga)?

uvugizi

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,235
873
WOGA, ambao kwa lugha nyingine wanaita PHOBIA ni ugonjwa ambao unapatikana kwa walimwengu wote ila inategemeana aina na approach yake.

Kuna aina nyingi ya phobia ( woga)

1. Glossophobia -- ni woga wa mtu kushindwa kuongea mbele za watu.

2. Acrophobia - ni woga ambao mtu anaogopa vitu virefu, kupanda milima, gorofa, nk

3. Aviophobia - woga ambao mtu anaogopa kupanda ndege.

4. Dentophobia -woga wa mtu kung'oa Jino.

5. Homophobia - woga unaomshika mtu akiona damu , au mtu anayevuja damu.

6. Arachnophobia - woga unaompata mtu kwa Mdudu nge.

7. Cynophobia - woga wa mbwa , na Mimi hapa nipo bado sijaweza kuondokana na hili.

8. Nyctophobia -- hofu ya Giza au wakati wa usiku, Mara nyingi hii inaanza kwa watoto, ikiendelea ukubwani ni tatizo .

Woga kitaalamu inatokea kwa sababu mtu ameweka kumbukumbu za habari na mambo mabaya kichwani mwake.

Kuna mtu alivyokuwa anakuwa aliteswa na mjomba, mama wa kambo, alitengwa nk. Sasa kama hakukombolewa huyu mtu atakuwa mtu mwenye tatizo la WOGA.

Woga una madhara ambayo hasa ukiingia nao katika Mahusiano iwe ni kazini, ndoa, makanisani nk, ni rahisi kuvunjika.

Mtu muoga siku zote anaona ubaya tu kwa sababu ana kumbukumbu mbaya .

Dalili zao kubwa kujijua wewe ni Muoga, unatetemeka miguu na mikono hasa unaposimama mbele za watu. Mapigo ya moyo kwenda mbio, kukata kwa pumzi,kutoka jasho nk .

Mtu Muoga kusonga mbele ni shughuli hasa kama ni mfanyabiashara, hawezi kuona fursa, wengi wanapenda kuwa chini ya,,,, hasa kuajiriwa.

Usiwe na woga bila sababu kwani woga ukizidi unapata ukichaa (schizophrenia)

Je unatokaje, kuna madawa yanaitwa ant anxiety medication lakini sikushauri tumia neno la Mungu.

Soma 1petro5:7
"Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote , kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu".

Lakini andika Woga wako katika karatasi na ukiwa peke yako, soma huku ukiipinga hiyo hali, ndani ya Siku 21. Subconscious mind itapokea na kufuta hiyo hali

Be inspired
 

Attachments

  • Coping-with-Fears-and-Phobias.pdf
    1.2 MB · Views: 82
  • Fearing-others-the-nature-and-treatment-of-social-phobia.pdf
    7 MB · Views: 129
Hydrophobia kile kitendo cha kuogopa maji """"

Genophobia.. ....



""""Mental ni hataree...wengine tuna bulimia nervosa
 
'Soma 1petro5:7
"Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote , kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu".

Lakini andika Woga wako katika karatasi na ukiwa peke yako, soma huku ukiipinga hiyo hali, ndani ya Siku 21. Subconscious mind itapokea na kufuta hiyo hali
'This is the best solution ever...
 
WOGA, ambao kwa lugha nyingine wanaita PHOBIA ni ugonjwa ambao unapatikana kwa walimwengu wote ila inategemeana aina na approach yake.....

5. Homophobia - woga unaomshika mtu akiona damu , au mtu anayevuja damu.

Bob homophobia ni hofu mbele ya watu wanaopractice same sex.

Hofu ya damu huitwa hemophobia
 
Mm hofu yangu ni mwoga wa kupanda gari, nikipanda gari nakua kituko...
 
Woga kitaalamu inatokea kwa sababu mtu ameweka kumbukumbu za habari na mambo mabaya kichwani mwake.
Mtu muoga siku zote anaona ubaya tu kwa sababu ana kumbukumbu mbaya.
Nikusahihishe tu kijana, Binadamu anapozaliwa huzaliwa na woga aina mbili.
1. woga wa kushindwa
2. woga wa vitu virefu (falling)


So woga sio lazima uwe kumbukumbu mbaya.
Je unatokaje, kuna madawa yanaitwa ant anxiety medication lakini sikushauri tumia neno la Mungu.

Usikaririshe watu neno la Mungu pekee linatosha kutibu woga, hata yeye alisema "jishughulishe utapata".. Dawa Muhimu kutumia anyway AKILI KUMKICHWA.
 
Mimi huwa nina challenge vitu vingi ambapo mpaka watu wananishangaa
Nilikuwa nina hamu sana ya bungee jumping nikafanya pia siku naruka kwenye helicopter ndio kabisa natamani nirudie Mara kumi
Napenda kukaa juu mbele kama picha la titanic nikiwa kwenye meli kuangalia dolphin.

Lakini woga ambao nimeshindwa ni kenge huyu kiumbe ananikera mpaka nikaamua kumla siku moja ili asinisumbue kichwani lakini wapi.
Napenda sana nyoka
 
No 2 inanihusu....mfano nikae juu gorofani halafu niangalie chini naweza kuzirahi kwa presha.....hata daraja la kimara nitapita bila kuangalia chini.

No 8. Unilazi usiku mwenyewe ni bora nikeshe naangalia movie
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom