Je, wewe ni mtoto wa kwanza katika familia: Fahamu jinsi Potential yako inavyowindwa ili uharibike

Kwa mila za zamani mkubwa akifariki basi yule mdogo mume analithi yote aliyokua nayo mkubwa. Hivyo wewe hapo unahitajika kusimama katika nafasi ya marehemu..
Wewe si mzaliwa wa kwanza ila unabaraka za mzaliwa wa kwanza aliyetangulia. Simama katika nafasi yako sasa

đź‘ŤShukran kwa ufafanuzi
 
Kweli mkuu yaani mpka mda mwingine nagombana na mke wangu kwa kutotumiza majukumu yangu ya family yangu wakati pesa inaisha kwa kuwasaidia wadogo zangu kwa mambo yao nk, nakumbuka mpaka nilichelewa kuingiza umeme ktk kibanda changu kwa mda wa miaka kama 4 wakati huo mdogo wangu namsomesha shule ya private ada laki 8 plus nauli na chakula kila siku nampa kwa mwaka ilikuwa ni pesa ndefu wakat umeme ilikuwa ni laki 3 plus gharama za wayaling nk... Naamini Mungu atanilipa kwa mambo yanoyowatendea wadogo zangu
Ndio ukubwa huo..ndio ghalama ya kua mkubwa.
Ukubwa di idadi ya miaka yako au ndevu zako.
ni kuweza kusimama katika nafasi yako.
Keep standing..keep providing mate
 
Yupo tayari mkewe asiavae nguo kwenye Eid au Xmass ili tu wadogo zake walipiwe ada, ukikuta mzaliwa wa kwanza anayejitambua na kusimamia majukumu yake hufanya kila kitu ili tu ndugu zake wasipitie tabu alizozipita na wazazi wake wakati anazaliwa.

Mkuu ulipotoa haya mawe, naomba ukachimbe na mengine utuletee! Asante sana.
 
Kisu kimegusa mpaka mfupa I'm the first born magumu nnayopitia nayajua mimi mwenyewe shetani amejua sana kuharibu maisha yangu nimejikuta mpaka machozi yananilenga baada ya kusoma huu uzi but bado nina IMANI mganga wangu ni mzawa wa Jerusalem ipo siku atanifungua kutoka katika gereza la kimwili na kiroho nlilofungwa masilu na masiku.....be blessed Da Vinci
 
Kila mtu kwa Mungu ana hadhi sawa. Tofauti zinazoweza kuwa za vipaji zina lengo la kutajirishana kwa manufaa ya wote.

Hakuna mtu bora kwa maana ya hadhi ya binadamu kwa Mungu.

Mawazo kwamba wazaliwa wa kwanza ni potential au hawafanikiwi katika uchumi nakadhalika hayana ukweli wowote; ni hisia tu.

Mungu amemuumba mtu kwa lengo moja tu, mtu amjua, ampenda na amtumikie.

Kuna vitu vinavyofanya mtu awe potential au kinyume chake. Katika hivyo vitu wazazi wakichukuwa nafasi ya kwanza na jamii ndio huandaa mwelekeo wa mtoto.
Hapa kuna suala la elimu, mafundisho na uelewa wa mambo. Elimu, mafundisho na uelewa mambo ukikosekana watoto huangamia.
 
Ondoa shaka Ndugu yangu mpendwa. Mada imewalenga Wazaliwa wa Kwanza ambao wapo pande zote. Muumba wetu ni mmoja tunaemwabudu na yeye hana Dhehebu.

Nikupe tu mfano rahisi: Safari toka Dom kwenda Dar, wako watakaosafiri kwa basi, watakaoruka kwa ndege, watakaotumia pikipiki na hata watakaotumia miguu. Hao wote watamaliza safari yao salama kufika Dar. Ndivyo ilivyo ktk kufika kwa Muumba wetu.
Kuna tatizo kubwa la uelewa.

Suala la Mungu halifafanuliwi kama safari ya kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam au kwingine kokote. Kuelewa hivi ni makosa makubwa.

Hapa kuna suala la taratibu zinazoongoza na kutawala hivyo vyombo, unalifafanuaje.
 
Kila mtu kwa Mungu ana hadhi sawa. Tofauti zinazoweza kuwa za vipaji zina lengo la kutajirishana kwa manufaa ya wote.

Hakuna mtu bora kwa maana ya hadhi ya binadamu kwa Mungu.

Mawazo kwamba wazaliwa wa kwanza ni potential au hawafanikiwi katika uchumi nakadhalika hayana ukweli wowote; ni hisia tu.

Mungu amemuumba mtu kwa lengo moja tu, mtu amjua, ampenda na amtumikie.

Kuna vitu vinavyofanya mtu awe potential au kinyume chake. Katika hivyo vitu wazazi wakichukuwa nafasi ya kwanza na jamii ndio huandaa mwelekeo wa mtoto.
Hapa kuna suala la elimu, mafundisho na uelewa wa mambo. Elimu, mafundisho na uelewa mambo ukikosekana watoto huangamia.
Tatizo ni nini.?
Nimekosea wapi mate..?
 
Kuna tatizo kubwa la uelewa.

Suala la Mungu halifafanuliwi kama safari ya kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam au kwingine kokote. Kuelewa hivi ni makosa makubwa.

Hapa kuna suala la taratibu zinazoongoza na kutawala hivyo vyombo, unalifafanuaje.
Je ww ungeelezeaje
 
Back
Top Bottom