Dr Orb
Member
- Aug 4, 2019
- 10
- 40
Historia kuu inayozingatiwa kuhusu hesabu za miaka ni ile yenye mlengwa wa kidini. ambapo historia hiyo inasema miaka 2019 ilianzia mwaka 1 ambapo Yesu kristo alipozaliwa kwa mujibu wa Dionysius Exiguu.
Hesabu hii haikuwa na uhakika na ilikuwa kimakadirio tu ya bwana Dionyius. Sababu kuu ya yeye kufanya hivi ilikuwa ni kwamba baada ya kifo cha Kristo si vyema kuendelea kuhesabu muda kwa kutumia mifumo ya watu waliomuua mkombozi wao (YESU KRISTO). Hivyo basi, ili kumaanisha alichokusudia ikawa ni vyema kuongeza neno A.D katika miaka, ikimaanisha Ano Domino yaani kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili ikiwa na maana hii "baada ya Mkobozi (Yesu)".
kwa hivyo popote uonapo miaka na neno A.D uelewe kuwa inamaanisha ni miaka iliyotajwa baada ya Kuzaliwa Mkombozi(YESU). mfano 1222A.D, maana yake ni miaka 1222 baada ya mkombozi (Yesu). Mfumo huu ulikubaliwa na kupewa kipaumbele na dola la kirumi kwa kuwa uligusa imani ya kikristo ambayo tayari dola ya kirumi ilikuwa imeshaipokea na kuitumia kama imani rasmi.
Katika muendelezo na jitihada za kueneza na kuusambaza ukristo, Baadae miaka ya 1500 ilikuja kukubalika na kuwekwa katika mfumo wa mahesabu ya kalenda uliowekwa na Julian na Gregory(hawa ni warumi), mfumo huu ndio huu tunaoutambua mpaka sasa na upo kimkondo kwamba 2019 ni miaka baada ya kuzaliwa YESU. Mahesabu ya kalenda ya Gregoryndio yanayotajwa kuwa na usahihi mkubwa wa kimahesabu kuliko kalenda yoyote duniani.
Kwa vile mfumo wa mahesabu ya kalenda ya Gregory yana usahihi mkubwa hivyo basi yalirasmishwa duniani kama ndio mfumo maalumu wa mahesabu ya miaka na kutumiwa na jamii nyingi kama zile za kiarabu na kichina,. Uingizwaji wa mfumo wa mahesabu wa Dionyius ulileta shida hasa katika mlengwa wa kiimani hususa ni nchi zisizoamini Ukristo kama Nchi za Asia na Afrika.
Jambo hili lilipelekea vita ya kikalenda kwa kuwa sasa ulijikita kidini zaidi, ilipelekea kila jamii kujikita na kalenda yake katika mlengwa wa imani zao. vita hii ikasababisha kuwapo kwa malekebisho ya uwakilishaji wa miaka kutoka kutumia A.D mpaka B.C.E (Before Common Era). ikiwa na lengo la kupunguza makali ilihali maana bado ni ileile.
Pamoja na mabadiliko hayo lakini bado Jamii nyingi za Ulimwengu haziungu mkono mfumo huu wa Gregory kwa kuwa ni wa kidini zaidi. Jamii kama Waethiopia, Wachina, Wahindi, Waarabu na Wayahudi bado wanaupinga mfumo huu mpaka sasa na wana mifumo yao safi kabisa ya mahesabu ya kalenda ingawa bado yanafuata Mfumo wa kimahesabu wa Gregory lakini si kwa nadharia kwamba huu ni mwaka wa 2019.
Lakini pamoja na yote haya shughuli nyingi za kimataifa zinaendeshwa kwa kutumia mfumo huu wa mahesabu wa Dionyius ambao ni wa kidini zaidi. na nchi hizi zinazopinga mfumo huu hutumia zaidi kalenda zao kwa mambo ya ndani ya nchi lakini katika masualla ya kimataifa wanalazimika kutumia Mfumo huu wa Dionyius.
Hata hivyo mifumo ya kuhesabu kalenda ni migumu na inatofauti sana kati ya jamii na jamii. ikiwa utapenda kufahamu zaidi link nimeweka hapa chini kwa baadhi ya kalenda maarufu duniani.