Je, wewe ni miongoni mwa wale wanaopenda kununua vitu kwa kuwa una pesa si uhitaji?

uvugizi

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,235
873
AFFLUENZA ni ugonjwa unaosababishwa na watu wenye vipato,, kununua vitu hovyo hovyo , hata kama haitaji ,naweza kuwaita "" shopaholic" ,,,,,,

Kwa lugha nyingine tunasema wana shopping addiction .

Affluenza ni ile hali ya kutumia vitu katika hali ya juu sana,,,, nia na madhumuni anahisi anajenga Furaha na kuridhika ana nguo kanunua hata kuzivaa havai, CD anunua nyingi kusikiliza hazisikilizi,, ana viatu akivaa Leo mpaka mwakani na bado ananunua ,, ana vitu vingi hata kuvitumia hatumii.

Kiimani hili ni pepo , lakini katika afya ya akili ni ugonjwa . Mara nyingi unaharibikiwa kabisa afya na akili.

Dalili kubwa au utamjuaje mtu ana huu ugonjwa .

1. Shop addition ..... Yaani unapenda manunuzi yasiyo kuwa hata na uhitaji , mradi na wewe uwe navyo.......utataka vitu , kwa modern. gari toleo jipya, nguo fashion mpya,, hata mahusiano mapya,,,
Hata inafika kujitukuza kupitia vitu ( over emphasis on labels),,,, mtu anajivuna kwa kuwa na gari model Fulani , account za instagram kuwa na status Fulani , watu , hutaona wakipiga picha vijijini kwao kwenye shida na tabu zote.

Na kawaida mwenye affluenza huruma hana ( lack of empathy for others),,,, wanajiona bora kuliko yeyote ,,,,, wao mtu akiwa katika magumu/shida/maskini kwao wanaweza kumuona kama mjinga ,,,

Affluenza inabebana sana na wale wenye kipato

Nini namna ya kutoka hili ..... John de graaf na David wann katika kitabu chao cha """ The all consuming Epidemic .... Suluhisho kubwa ni kujifunza namna ya kubudget yaani ..... Jifunze pia kutunza fedha zako na kusaidia wengine na kushirikiana na watu matumizi bora ya pesa siyo kushiriki kutumbua

Chukua nafasi ya wengine katika matatizo yao ( Empathy)

Hapa ndipo nilipokumbuka Yale maneno ya biblia

luka 6:38 """" wapeni watu vitu, nanyi mtapewa: na wale siyo mjipe ninyi

Be inspired
 
Back
Top Bottom