Je, wewe CV yako ya mazishi, itachukua dakika ngapi kusomwa?

Kuna jamaa nimekutana naye mtaani, akasema ya kuwa, kusoma sana pamoja na kufanya kazi sehemu nyingi nyingi, kunasababisha CV ya mazishi kuwa ndefu.

Akimaanisha CV ya mtu aliyesoma sana na kufanya kazi sehemu mbali mbali inakuwa na kurasa nyingi, na kupelekea usomwaji wa CV hiyo kwenye mazishi kuchukua muda mrefu hata lisaa limoja.

Je, wewe CV yako ya mazishi, itachukua dakika ngapi kusomwa?
Hakuna CV ya mazishi
Kuna wasifu yaani kuongelea mambo ambayo marehemu amefanya
 
Kuna jamaa nimekutana naye mtaani, akasema ya kuwa, kusoma sana pamoja na kufanya kazi sehemu nyingi nyingi, kunasababisha CV ya mazishi kuwa ndefu.

Akimaanisha CV ya mtu aliyesoma sana na kufanya kazi sehemu mbali mbali inakuwa na kurasa nyingi, na kupelekea usomwaji wa CV hiyo kwenye mazishi kuchukua muda mrefu hata lisaa limoja.

Je, wewe CV yako ya mazishi, itachukua dakika ngapi kusomwa?
Yani mnataka kuimpress watu hata mkiwa wafu! Hata ikiwa masaa 6 inasaidia nini? CV nzuri ni kuishi vizuri na watu.
 
Kuna wengine CV ndefu mpaka kazungushwa nchi nzima waijue ila bado anapondwa
Sasa sijui huwa zina faida gani au cv nzuri na huko tunakoenda kuna ajira pia?

Kuna watu mna vituko
 
Kuna kabila la watu kule Tibet,mtu akifa mwili wake wanaupeleka mlimani na kuuacha huko

Wakishauacha kisha wanakuja ndege walao nyama wanautafuna mpaka unabaki mifupa

Wale ndege wanaaminika ni malaika

Hivyo wanapouafuna mwili na kisha kupaa juu agani inaaminika kuwa eti wanaruka na roho ya marehemu na kuipeleka mbinguni

We subiria risala ndefu kama ya Magufuli

Ukristo umejaà unafiki aisee

Mimi ingekuwa amri yangu itaheshimiwa nikifa ningehusia kwenye wosia wangu wanichome moto badala yakunitembeza wakiniuzisha sura kwa kisingizio cha kuniaga
Kwahiyo waislamu hawasomi historia ya marehemu?
 
Tafadhal! Wasifu kiingereza ni biography au description. CV ile C ni Curriculum na V ni vitae. Kwa kiswahili Curriculum ndio mtaala. C.V.moja kwa moja ina uhusiano na mamvo ya masomo, shule, na vyuo.
Tofauti ni hii inatumika wapi na ile inatumika wapi; nyingine kwa ajili ya maombi ya kazi na nyingine kwa ajili ya kumuongelea marehemu; ila kitu ni kile kile, tofauti ni muda gani hii inatumika
 
Yangu itakua,
"Anayemdai Marehemu??, anayedaiwa na Marehemu?? wamuone anko J, haya twendeni tukazike hakuna Matanga isipokua kwa ndugu waliotoka mbali ndio wabaki nyumbani"

Kwisha.
 
Back
Top Bottom