Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,982
- 45,900
Nimeyasikiliza maelezo ya kamanda siro Leo wakati akitoa feedback kuhusiana na operesheni iliyokua ikiendelea ya madawa ya kulevya!
Kamanda katika maelezo yake alitaja umri wa Wema sepetu kuwa ni miaka 28.
Baada ya kusikia hilo, nilipitia pia profile yake Instagram ambapo aliweka taarifa kuwa yeye aliwahi kuwa miss Tanzania wa mwaka 2006.
Kwa hesabu za haraka tofauti kati ya mwaka 2017 na 2006 ni miaka 11, ambapo ili kupata umri wa sasa wa miaka 28 alionao utaona kwamba mwaka huo 2006, wema alikua na miaka 17!
Kama hesabu hizo zipo sahihi, basi ni wazi kwamba Miss Tanzania wa mwaka 2006 alishiriki shindano kinyume cha sheria za nchi! Na mwandaaji atakua ameshiriki katika kosa kwa kuruhusu mtu asiye na vigezo kisheria kushiriki shindano husika!
Ikumbukwe kwamba hii si mara ya kwanza kwa swala la utata wa umri wa washiriki ama washindi wa shindalo hilo la ulimbwende kuibuliwa!
Je, waandaaji hawaoni umuhimu wa Kumfuta katika orodha ya waliowahi kuwa washindi wa taji lao la Miss Tanzania ili kujitenga na udanganyifu huu?