Je, Waziri Ngeleja amefanikiwa kuzima maandamano? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Waziri Ngeleja amefanikiwa kuzima maandamano?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtego wa Noti, Dec 23, 2010.

 1. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,231
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Ndugu wanaJf, leo waziri wa nishati na madini ameongea live na watanzania kuhusu mambo mgao wa umeme na suala la ongezeko la gharama za umeme. katika maongezi hayo yaliyokuwa yakirushwa live na TBC, alikuwa na mtu wa tanesco na mtu wa ewura. Waziri alizidi kusema kuwa mgao wa mgao wa umeme utaendelea kuwa historia kutokana na mipango ya kuzalisha umeme iliyopo ikiwa ni pamoja na kuzalisha 1500MW hadi ifikapo 2015.
  Lakini alisema kuwa ongezeko la gharama za umeme ni kiasi kidogo sana, yaani ni sh 11 tu. anashangaa watu wanaokuza kuwa gharama ni kubwa mno ilihali ni ongezeko dogo tu.
  alisema pia kuwa watanzania ni watu waelewa sana na haamini kama watakuwa tayari kuharibu utaratibu waliojiwekea wa kutatua mambo yao. akasema kama wakiandamana watakuwa wanavunja amani kwa kuwanufaisha watu fulani.
  Hivi wanaJF mnaona matamshi haya yatasitisha mgomo uilopo au ndio ametia petrol kwenye moto wa maandamano? Nawasilisha!!
   
 2. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Kuandamana kwa Watanzania watamnufaisha nani kama si Watanzania wenyewe wenye kupata tabu ya Umeme? Nani wa kunufaishwa katika maandamano hayo? je wanataka tuendelee kuwa wapole na kujisifu watanzania wanaishi kwa amani wakati matatizo kila kona ni kilio?

  Huo ni ujinga wa kutupwa tulishaonekana kama ni watu wa kuburuzwa siku zote watutishe tu ila ipo siku tutaelewana tu.
   
 3. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,231
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Huo ni ujinga wa kutupwa tulishaonekana kama ni watu wa kuburuzwa siku zote watutishe tu ila ipo siku tutaelewana tu

  na tukikaa kimya awamu hii itakuwa mekula kwetu...hii tunayoita amani ndiyo wanatumia kutufanya sisi misukule na kutuendesha kwa kila kitu....
   
 4. e

  emrema JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa Kenya , Zambia,Zanzibar na Nchi zenye wananchi wenye uchungu na maendeleo MAANDAMANO yangeshaanza, lakini kwa wabongo aaaah wakila ugali wao wakalala usingizi baasi wamesahau.Hatuna sababu ya msingi kulipa gharama kubwa hivi ya umeme.Sisi ni kati ya nchi chache Africa tunaoongoza kwa gharama ya umeme na nishati ingawa tuna rasiloimali zote.Tuachane na siasa haya ni maisha yetu. Mtaani ninapokaa maduka yamepata hasara mwezi huu ina maana vipato hamna. wengi wenye biashara na kazi ndogo ndogo wamekwama . mnategemea nini kama sio kuanza wimbi la wizi na ukabaji kwenye makazi yetu. TUINGIE LEO BARBARANI KAMA NI KUTUUA WAMESHATUUA JAMANI.
   
 5. e

  emrema JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Suluhisho rahisi hili hapa, kwanza TANESCO ibinafsishwe kwa wananchi wanunue hisa kama Kenya na Kenya Power yao. Pili kuwepo na makampuni binafsi ya kuzalisha umeme na kuuza moja kwa moja kwa wananchi bila kuuchakachua kwa TANESCO hapa lazima gharama zitashuka tuuu. Tuangalie mifano ya simu leo gharama ni chini sana. Utafiti wangu mdogo tuu nimegundua wananchi wana uwezo kabisa wa kuendesha TANESCO kama watapeWa hisa. Wanaotumia simu Tanzania ni wengi kuliko wanaotumia umeme na asilimia zaidi ya 80 ya wananchi wenye simu wanatumia shilingi 60,000 hadi 80,000 kwa mwezi. WANAUCHUMI MPO WAPIIIIIII?
   
 6. M

  Mchekechoni JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Right now Ngeja is live on star tv, just bla bla tu! Kama na bulet...booom! Umeme huo kushney...mmh kudadadadadededeki!
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Aache ujinga wake huo, kama hilo ongezeko ni dogo sana basi lisiwepo, siwaache kuliongeza kama ni dogo? wanaliongezea nini sasa? au watulipie wao, si ni dogo? pambaf kabisa hebu aniache nisije nikapata unnecessary ban bure
   
 8. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huyu waziri kisha lewa madaraka hawezi tena kutatua tatizo la umeme kama ongezeko dogo wanaongeza la nini si waache kuongeza au washushe bei tupate ahueni. Kundamana kupinga huu upuuzi tutaandamana yeye kama wazirianapata umeme wa bure na kila leo kuingia mikata ya kitapeli ambayo inaleta matatizo kwa shirika na tunaoumia kulipia gharama ni sisi wananchi, kwanini hafikirii kurekebisha mikataba iliyopo ili shirika lipate ahueni ya gharama na sasa hivi yupo kupiga debe ili DOWANS kampuni ya shwahiba wake RA ilipwe 185 Billioni
   
 9. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,231
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  ajiuzulu vinginevyo....
   
 10. n

  ngoko JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sawa Mhe. waelimishe , ongezeko la gharama ni kwa manufaa ya umma wote na si wachache, that's maumivu ni kwa umma na wachache kivulini wakilipiwa gharama hizo na jasho la huo umma.
   
 11. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,231
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  hata leo alipokuwa akiongea na Star tv alisisitiza kuwa watu wasiandamane maana ongezeko lenyewe ni kiduchu mno. anazidi kuwasisitiza watu wasiishangaze dunia kwa sababu tanzania ni nchi inayo aminika kwa amani na utulivu...
   
 12. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,231
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  ngeleja anasema ewura wanafanya kazi nzuri mno katika kudhibiti ongezeko la bei za vitu kama umeme, maji na mafuta...
   
 13. khayanda

  khayanda JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Yawezekana watanzania tumekuwa sugu kupokea maonevu, na viongozi wetu wanajua hilo. Hivi umeme hapa duniani ni lazima uwe na nembo ya TANESCO? Yaletwe makampuni mengine ambayo yanauwezo wa kututengezea umeme kwani tuna vyanzo vingi, kuanzia upepo hadi mawimbi ya baharini na ziwani. Ila sitashangaa, jamaa anaweza hata akaweka mgao ikulu maana haina mtu ila kuna kiumbe kinachoonekana kama mtu. Raisi wetu ameingia ikulu kazi yake imekwisha na anaacha jamaa watuvune tu, watuuzi majenereta, wachakachue mafuta hata tugari twetu tulitobahatisha tufe pia.
   
 14. khayanda

  khayanda JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ewura nao na viongozi wetu lao moja. Ewura imewekwa kuharalisha ufisadi katika eneo lote la upatikanaji wa nishati hapa TZ. Watanzania tusiposema na kukataa kwa vitendo tutaendelea kuumizwa siku zote. Tukilalamika kuhusu mishahara, wansema inatosha yao wanaiita posho tu ambayo kwa mwezi mmoja pato la mbunge tu lingeleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo kwa kila jimbo. Tuwafanyeje hawa jamani???????
   
 15. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mwaka jana alipolazimika kuwasha IPTL alitoa ahadi hizo hizo!uwezo wake wa kufikiri mdogo!
   
 16. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  ngeleja ni very dormant, hajui kujenga hoja na pia kila analoongea ni kwajili ya kulinda maslah ya rostam na mamvi lowasa hao ndio waliomtoa vodacom na kumpeleka kwenye wizara hiyo. Ni mchafu wa tabia alishawahi iba dem wa mtu mwanafunzi wa u dom ambae alimkuta club. Alitumia cheo chake na fedha za kifisadi kumdhalilisha laurent na kumchukulia dem wake. Naye hukum yake ipo njiani. WATANGANYIKA ANDAMANENI MSIMUOGOPE HUYO MPAMBE WA MAMVI,MKWERE NA ROSTAM JANGIRI
   
 17. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ngeleja anashangaza sana anakazana kujenga miradi ya high voltage ukiwemo huu 132kv unao pita kwa kakobe uliogharimu zaidi ya 60bills wakati kituo cha ubungo hakiwezi kutoa umeme wa kawaida??
  Sasa wamekazana kutandika nyaya hizo lakini mwishoni hakuna umeme unao pita. Juzi mitambo imelipuka karibu na nguzo namba moja. Kwanini fedha zote hizo zisitumike kujenga na kuimarisha mitambo tanesco mpaka sasa tunaingia kwenye giza????
   
 18. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  that ngeleja..., sina hata la kusema. Nina umia sana.
   
 19. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  that ngeleja..., sina hata la kusema. Nina umia sana.
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Dec 25, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  unfortunately Ngeleja is another boy who represents some dudes
   
Loading...