Je, wazee wa sasa wanaishi vipi wakati sisi tunapigia kelel pension chini ya miaka 55? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, wazee wa sasa wanaishi vipi wakati sisi tunapigia kelel pension chini ya miaka 55?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SubiriJibu, Aug 5, 2012.

 1. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,124
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Baadhi yetu sisi ni vijana lakini miaka michache ijayo tutaitwa wazee. Hili suala la pension litatukuta tukiwa wazee. Sijikiti sana kwenye suala la kuchukua pension kabla au baada ya miaka 55.

  Nadhani kosa kubwa tunalofanya ni kujadili suala la miaka 55 iliyowekwa na serikali bila kuanza kwanza kujadili wazee wa sasa hivi wanajikimu vipi. Wanakabiliwa na changamoto zipi kimaisha. Nani anawatunza.

  Mifano niijuayo mimi ni michache, haitoshi kutoa picha kamili. Lakini pia uchache huo haunifanyi niogope kuisema hapa JF.

  Wapo wazee ambao walikuwa na vyeo vya hali ya juu na mishahara minono ambayo sisi wengine tunaweza tusiwafikie kamwe. Walipata nafasi tele ya kwenda safari za nje zilijaa perdiem zilizonona. Wamesomesha watoto wao na baadhi ya watoto wao ni ma-director kama wao wa kampuni zao binafsi.

  Ungetegemea mzee wa aina hii asisumbue kimaisha wakati huu. Lakini siwataji majina ila wanakera mpaka unasahau kwamba ndiye yule aliyeogelea kwenye pesa kibao huku akiishi nyumba nzuri kule Oysterbay au Masaki au Isamilo au Capri Point.

  Kila siku wanaleta malalamiko maofisini kwamba pension yao inapunjwa au la. Ni waombaji wakubwa.

  TUje kwa sisi vijana. Hivi hizi ndoa zetu ambapo kijana ukimsaidia mama yako au baba yako mke anakuja juu kama mbogo unategemea nini?

  Sasa, siendelei na mifano binafsi ninajua na nyinyi mnayo. Hiyvo kwanza tujadili maisha ya wazee wa sasa hivi ili tujue kama kweli mtanzania anaweza kujikimu mwenyewe au la anapozidi umri wa miaka 55.

  Kama katika mjadala itaonekana kwamba wazee kuanzia umri wa miaka 55 wanapiga niahsra kisawasawa basi binafsi sina matatizo na kuchukua hela ya NSSF hata ukiwa na miaka 32.

  Lakini kama maisha ya wazee wa sasa hivi yanawashinda kumudu na sisi hatuwezi kuwsaidia kwa sababu yoyote ile basi tusidanganyane ni afadhali serikali itumie nguvu kutoruhusu hela kuchukuliwa chini ya miaka 55.

  Natarajia mawazo na si kejeli au matusi.
   
 2. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wastani wa Umri wa kuishi watanzania (life expectancy) ni miaka 52 na ki-takwimu ni 5% ya vijana ndo watafikisha umri wa 55!

  Je ukichanganya na za mbayuwayu huoni ni bora mtu achukue chake mapema? Kama huamimi mfuate mzee wa kuanzia miaka 55 yeyote, akutajie rafiki zake 10 wa ujanani, kisha akutajie walio bado hai wangapi mpaka sasa!

  Hao unaowataja waliokuwa wanakula bata Osterbay, Isamilo nk, wengi walikuwa wanajiona miungu watu kwa kustarehe nchi mbali mbali sasa wazoee kama wale wa East Africa!

  Vijana wa sasa hivi wengi wamejifunza kutoka kwa wazee hao hivyo wanataka wapewe hela yao wajijenge kiuchumi na kijamii! SSRA waachie pesa za vijana wakajiendeleze kielimu!
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  SSRA tunataka hela zetu miaka 55 mtakaa nyinyi na watoto zenu sie tunataka chetu mapema!
   
 4. cmoney

  cmoney JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  vijana siku hzi mnavaa vifuko wakati wa mapenzi na kwenda kutupa vitoto badala ya kuzaa kama mimi mwe watoto 32..mkienda mbinguni mtakuta mmeua watoto wangapi?...maneno ya mzee kwe njia panda clouds fm..hv unadhani kwa mfumo huu wa maisha walioishi ingekuwa rahisi hiyo pensheni kubaki?
   
 5. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,589
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tunataka pension tujijenge mapema na siyo kuitegemea serikali iliyojaa mafisadi kila sector.
   
 6. Mzee Msemakweli

  Mzee Msemakweli Senior Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 159
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nakushauri urudi kwa waliokutuma ukawaambie kuwa vijana wa leo wanazitaka pesa zao. Thamani ya shilingi ya leo sio ya kesho.

  Sasa hivi watu tunataka kufanya kazi kwa mda mfupi kisha tujiajiri na huo ndo ujanja sio ufanye kazi hadi uzeeke. SSRA ni wezi na wanyang'anyi.

  Laana ikae juu yako na wale wote waliokutuma. Unataka kuniambia mahitaji yako ya leo yangoje hadi ufikishe miaka 55?
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hatukubali sheria mpya ya SSRA FULL STOP.
   
 8. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,456
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Naona umejitahidi sana kutetea serikali kuhusu sheria dhalimu ya kuibia wafanyakazi pesa za mafao yao.
  Labda nianza kwa kukufahamisha kuwa nchi hii haijali kabisa maslahi ya wananchi wake. Ladba kama wewe ni mgeni hapa Tanzania, lakini nina uhakika kabisa kuwa unajua jinsi serikali ya nchi hii ilivyo dhalimu kwa wananchi wake.
  Serikali ya Tanzania iko hivi:-
  • Serikali ya Tanzania iko tayari kutoa wananchi wake wauwawe kwa ajili ya maslahi yake ya viongozi wake, mfano ni pale wachimbaji wadogo wa madini wanapozikwa wakiwa hai kwenye migodi ndani ya nchi yao wenyewe ili tu kupisha muwekezaji anayeiba dhahabu na kulipa mrahaba wa 3% !!
  • Serikali ya Tanzania iko tayari kuua wananchi wake ili tu kubakia madarakani baada ya kushindwa uchaguzi, mfano ni mauaji ya watu Zanzibar baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000.
  • Serikali ya Tanzania iko tayari kukandamiza wananchi wake wanaodai haki zao kwa amani kabisa, mfano utekaji nyara na utesaji wa Dr. Steven Ulimboka aliyekuwa anadai haki za madaktari kwa amani kabisa.

  Kwa mifano hii michache sana, nadhani hata kama wewe ni mgeni sana hapa Tanzania, utapata picha kuwa serikali ya Tanzania haijali kabisa maisha na maslahi ya watanzania. Sasa, kwa ukweli huu, nadhani hata wewe unaweza kuona kuwa sheria hii mpya ya mifuko ya pension ni sheria kandamizi iliyotungwa kwa nia ile ile ya kunyonya na kudhulumu mafao ya wafanyakazi wa Tanzania.
   
 9. Mtumpole

  Mtumpole JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mafao.jpg Wengi wa Watanzania ni waoga.
   
 10. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,124
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Nimeuliza swali rahisi sana ambalo hakuna mchangiaji aliye tayari kunifafanulia. Je, wazee wa sasa hivi wanaishi vipi?

  Maana yake mchangiajia anashindwa hata kueleza baba na mama yake wanajikimu vipi?

  Sasa, kama kwa majibu haya machache ambapo mtu hawezi na hataki kabisa kusikia neno wazee wa sasa, mnataka serikali ifanyeje kuhusu wazee wa kesho?

  Kwa namna moja action zenu ndizo zinaifanya ipate kichwa cha kfanya hivi hata kama nyinyi kidhamira hampendi lakini kimatendo ni wazi wazee wa kesho hawana wa kuwajali maadamu hata humu tu JF hakuna hata mmoja anayelionyesha hilo kwa wazee wa sasa.
   
 11. l

  livingafrican Member

  #11
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 11, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Suala siyo miaka 55 au 32. Suala ni kwamba serikali inajaribu kucheza patapotea kwani haijulikani hizo hela za kuwalipa wanachama zitatoka wapi kwani wameishazitumia kinyume na malengo yaliyokusudiwa. Hii ni sheria kandamizi na hata tukikubali kuchukua baada ya kufikisha miaka 55,hizo hela hazitakuwepo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
   
Loading...