Je, watumishi wa umma watarajie nyongeza ya mishahara 2019/2020?

Acheni uchochezi, kuwa mtumishi wa umma ni wito na uzalendo.... na lengo sio kuwa matajiri.

Usile Mbegu.
 
Kazi inabadilika kwa kupungua au kwa kuongezeka?
kazi inaongezeka, na risk ya kazi inaongezeka pia. unavyokua na cheo kikubwa ndivyo unavyopewa majukumu muhimu zaidi hususani ya kuwasimamia wengine na ndivyo unavyokua kwenye hatari kubwa ya kuwajibishwa/wajibika.
 
Acheni uchochezi, kuwa mtumishi wa umma ni wito na uzalendo.... na lengo sio kuwa matajiri.

Usile Mbegu.
sio uchochezi ndugu ni mawazo tu yanayolindwa na ibara ya 18(1) ya katiba yetu, hata JK alikuwa anawapa nyongeza na halikua lengo lake kuwafanya wawe 'matajiri'.
 
sio uchochezi ndugu ni mawazo tu yanayolindwa na ibara ya 18(1) ya katiba yetu, hata JK alikuwa anawapa nyongeza na halikua lengo lake kuwafanya wawe 'matajiri'.
Tunatekeleza ilani ya chama, sio katiba ambayo mshaikana.... subirini inayopendekezwa.

Usile Mbegu.
 
Wanaozitunga Sheria na kuzisimamia ndio Wavunjaji wakuu wa Sheria hizo,Alafu wepesi wa kujificha kwenye kichaka cha "Tuwe Wazalendo" Sifa na Utukufu Apewe Bwana, Hatuna namna.
 
Swala la maslahi ya watumishi limekua kitendawili katika awamu hii ya tano, kuna mengi yasiyo elezeka, baadhi ya watumishi wamepanda madaraja na vyeo huku wengi wakiendelea kupiga 'mark time'! kima cha chini cha mishaharahakija badilika, kama TGS... ilikua TSh 200 mwaka 2016 imeendelea kuwa 200 mpaka leo, nayo serikali haijaishiwa visingizio, walianza na uhakiki na sasa mheshimiwa waziri mkuu amekuja na story mpya inayoiita 'tume ya mishahara na motisha', kama kawaida ya wanasiasa PM amewomba watumishi wawe wavumilivu kwakua mheshimiwa rais ameunda hiyo tume na 'soon' mambo yote yatakaa sawa!
Leo waziri wa fedha Dr. Mpango baada ya kuwasilisha mapendekezo ya serikali juu ya ukomo wa bajeti ya 2019/2020 ndio tunaanza kupata picha kuwa inawezekana hizi ahadi za PM ni kujaribu tu kuwapooza watumishi.
katika mwaka wa fedha 2018/2019 serikali ilitenga Tsh 7,409,952,000 kwa ajili ya mishahara, katika mapendekezo ya serikali juu ya ukomo wa bajeti ya 2019/2020 serikali imependekeza Tsh 7,558,974,400 kwa ajili ya mishahara. Tofauti ya mwaka huu na ule ujao wa fedha ni Tsh 149,022,400 tu! kumbuka ongezeko hilo pia linahesabia mishahara ya ajira mpya zitakazo pewa vibali mwaka 2019/2020, sasa je kwa idadi ya watumishi wa umma iliyopo, na kwa ajira mpya zitakazo tolewa, kutakua na nyongeza yoyote kwa watumishi??? au ndio mchezo utaendelea wa kuwapandisha vyeo wafunga buti huku wengine wakiambiwa wawe wavumilivu tume ya raisi imalize kazi yake?

muonenii huruma rais anajenga nchi, ni vizuri mkamuomba angalau mishahara ya sasa ipinguzwe kwa 5%. pesa iendee kwenye maendeleo
 
Nimesikiliza TBC ongezeko la bajet ni Tsh bill 600 tu ukiigawa kwa 12 miezi kwa mwaka ni sawa nabongezeko la bill 50 tu kwa mwezi.
 
muonenii huruma rais anajenga nchi, ni vizuri mkamuomba angalau mishahara ya sasa ipinguzwe kwa 5%. pesa iendee kwenye maendeleo
mkuu maendeleo yapo tu, lakini maisha ya watumishi yanakikomo :)
 
Back
Top Bottom