Je, watu wa Serikali za dunia wana siri zipi ambazo wengi wetu hatuzijui?

elishaezekiel

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
563
1,458
Watu wa Serikali za dunia wana siri zipi ambazo wao wanazijua sisi hatuzijui. Hawa watu huwa hawana hofu wala uoga

Wanaweza kuonea watu bila hofu yoyote. Wanaweza teka mtu bila wasiwasi wa kuwa kunaMungu hata wakatesa au wakatoa uhai wa mtu wakisahau kuwa na wao ni watu na watakufa anyway ( kwa sababu kufa ni lazima)

Hawa watu huwa wanawaza kweli in the long Perspective mfano miaka mia ijayo watakuwa wapi??

Huku kusahau kunasababishwa na nini... nijuavyo mimi mtu mwenye hekima kamwe wazo la kifo chake halitoki akilini mwake.... wala hawazi kujisahaulisha akajifanya ataishi milele kitu ambacho ni kujidanganya!!

Najua kujidanganya ni vizuri kwa roho ya watu wachanga.

Watu wakomavu huuface uhalisia wa maisha kama ulivyo ya kwamba siku moja lazima afe na ataoza, atanuka atabaki mifupa...

Hawaogopi kunyonya watu wengine lakini wao Serikali zao wako makini kunyonywa.. angalia wanavyowasaka wakwepa kodi!

Hawana hofu ya kuwatumikisha watu kwa ujira mdogo lakini wao hwawezi na hwataki kutumiwa hivyo hujilipa vitita kwa kazi ndogo mfano wafanya kazi wengi kulipwa ujira mdogo na kukatwa pesa zao kwa kisingizio cha kodi

Watu wa Serikali hizi kuhubiri amani wakati wao wanalindana kijeshi... hapa kuna ukweli gani kuhusu asili ya mtu ambayo hawa watu wanaijua ila sisi tunafichwa??

Mfano kusema uongo mbele ya kadamnasi bila hofu then wao hawataki watu wawadanganye wao...

Au ili umtawale mtu ni lazima umfiche ukweli
Uweze kumdanganya kuhusu uhalisia wa mambo yalivyo

Hizi Serikali zina siri zipi.... Kwa maana mimi huwaona watu walio kwenye madaraka kama watu wa kawaida mno... na uwezo wao mwingi wa kiakili ni mdogo

Bila shaka uongozi ni (UONGO +ZI).
Sidhani kama watu wasomi wa karne ya 21 wanaweza kumuamini (KIONGO + ZI)

Na wanavyojua kuassume hizo position zao utacheka.
 
Ni watoto wa baba wa uongo, ambae ndio kiongozi wao, mkuu wa dunia hii. Kwa hiyo wanafanana tabia na matendo.
 
Wanayo yafanya hutekelezwa na viongozi wa usalama (makachero)
makachero hupeleka Taarifa kwa mkuu wa nchi kuwa kuna wtu wana nia mbaya na serikali au nchi au Raisi binafsi.
Hapo Raisi kwa vile anawaamini anatowa maamuzi washughulikiwe kimya kimya kabla ya kutekeleza mipango yao. Wakati mwingine huchelea kuwakamata na kuwashtaki
Endapo watabahatika kufikishwa mahakamani inakuwa vigumu kuthibitika makosa ya mambo ambayo hayajatokea.

Hapo ndio Viroba hutumika na kutupwa chumvini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom