Je wateja wenye ngozi nyeusi hupata huduma mbovu ukilinganisha na wazungu………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je wateja wenye ngozi nyeusi hupata huduma mbovu ukilinganisha na wazungu………!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtambuzi, Jun 13, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mighahawa kama hii huzua mangung'uniko kwa wahudumu kuwa na ubaguzi wa rangi

  Utafiti nilioufanya hivi karibuni katika mighahawa inayoitwa ya kitalii hapa nchini nimebaini kwamba wateja wenye asili ya afrika hususan wenye rangi nyeusi hupata huduma duni ukilinganisha na wazungu.

  Utafiti huu niliufanya katika mighahawa ya mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar. Nililenga mikoa hiyo kwa sababu ni miji ambayo hutembelewa na watalii kwa wingi na ina mighahawa mingi ya kitalii ukilinganisha na mikoa mingine.

  Utafiti wangu ulijikita zaidi kwenye maeneo yafuatayo:
  1. Mapokezi
  2. Kukalishwa kwenye meza
  3. huduma ya vinywaji
  4. huduma ya vyakula baada ya kuagiza
  5. Huduma ya kuletewa Ankara (Bill)

  Nilikuja kugundua kwamba wakati wazungu wakifika kwenye mghahawa hupokelewa kwa bashasha na kuelekezwa kwenye meza na kukalishwa lakini wateja wenye ngozi nyeusi wanaweza kufika hapo kwenye mghahawa na wakabaki wakishangaa, hakuna mtu wa kuwapokea wala kuwealekeza kwenye meza. Ni mpaka pale watakapoulizia iwapo wanaweza kupatiwa meza.

  Kwa upande wa huduma ya vinywaji vile vile wazungu watapelekewa menu na kuchukuliwa oda ya vinywaji wakati wanasoma menu, lakini wateja weusi kila kitu mpaka wafanye kuomba. Na hata baaada ya kuagiza wazungu wanaweza kuletewa oda yao mapema zaidi ukilinganisha na wale wateja weusi wenye asili ya Afrika. Kwenye swala la Ankara (Bill) nalo ni kizungumkuti, mzungu ataletewa bill yake mapema sana pale atakapoomba lakini mteja mwenye rangi nyeusi itamchukua muda kuletewa bill yake.

  Nilijaribu kuongea na baadhi ya wahudumu (waiters) wa mighahawa hiyo lakini wengi walipinga kwamba hawahudumii wateja kwa kuangalia rangi lakini baadhi yao walikiri udhaifu huo wakisukuma lawama kwa baadhi ya wahudumu wenzao ambao hukimbilia wazungu kwa sababu wao baada ya huduma huacha bahashish (Tips) tofauti na wateja wenye rangi nyeusi wenye asili ya Afrika ambao hawana utamaduni wa kuacha bahashsh (Tips). Hata hivyo walikiri kwamba wapo wateja weusi wenye asili ya Afrika ambao wanaacha bahashish (Tips) baada ya huduma.

  Lakini pia walidai kwamba wateja wenye rangi nyeusi ni wasumbufu na pia wana kitu kile kinachoitwa inferiority complex, kwamba wakifika kwenye mghahawa wanajiona kama wao wanachukuliwa na wahudumu kama wateja wa daraja la pili na hawathaminiwi na hapo ndipo utata unapoanzia kwani watakosoa kila kitu tofauti na wazungu ambao hata wakicheleweshewa oda zao huuliza kwa upole.

  Mhudumu mmoja mbaye alijitambulisha kwa jina la Dullah anayefanya kazi katika mghahawa mmoja pale Sea Cliff alisema kwamba, kingine kinachosababisha kuzua manung’uniko ni aina ya vyakula vinavyoagizwa na wateja….

  “kuna aina ya vyakula ambavyo havichukui muda mrefu kuandaliwa na kama mzungu kaagiza aina hiyo ya chakula ni wazi atalelewa haraka ukilinganisha na mteja mwingine aliyeagiza chakula kinachohitaji matayarisho maalum. Kwa mtu anayeelewa mapishi kama wenzetu wazungu hawezi kulaumu lakini kama ni mbongo lazima atalaumu….” Alisema Dulla.

  Hata hivyo nilipoongea na wateja mbalimbali niliokutana nao katika mighahawa hiyo walikiri kwamba kuna aina ya ubaguzi wa rangi katika mighahawa ya kitalii hapa nchini na sio mighahawa tu hata katika maduka makubwa kama supermarkets.
   
 2. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  watu weusi hamuweki UNDER THE TABLE au kwenye kale kachenchi hambakishi kidogo unabeba chenchi yote ,hamna KEEP CHANGE
   
 3. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama ni ubaguzi wa rangi mara zote.

  Nataka kukueleza wazi kwamba upatikananji wa huduma ya haraka na nzuri uko mikononi mwa wahudumu (waiters). Sasa katika nchi nyingi za wazungu wana utaratibu wa kutoa tip baada ya huduma, kiasi kama 10% ya bili unayoletewa. Kuna sehemu ni aibu kutoacha tip, na kuna nchi wahudumu walikuwa hawalipwi mishahara wanatarajiwa wapate tip. Sasa tatizo ni kwamba sisi waswahili bwana, hata mhudumu atuhangaikiaje, hatutoi tip na tunadai chenji hadi thumuni ya mwisho. Tena mhudumu akijisahaulisha tunapayuka wazi, haroo, lete chenji yangu nataka kuondoka, weee vipi?

  Mara kadhaa nimetoa tip ya japo kitu kidogo kama Tshs 1000 huwa nakuta wahudumu wanashangaa, kwani hawajazoea kuona mswahili anatoa tip ku-appreciate huduma.

  Hivyo basi, next time ukienda mgahawani ukapata bill ya Tshs 30,000/- uwe tayari kumkatia mhudumu 10%, yaani Tshs 3000/- kama tip. Kisha siku nyingine urudi pale uone utakavyodakwa kama mpira wa kona na wahudumu.

  Hapendwi mtu pale...tip yake tu!
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Synthesizer lakini kwa mujibu wa sheria za nchi yetu hairuhusiwi kutoa bahashish (Tips) na hata pale Airport kuna kibao kimeandikwa kabisa "marufuku kutoa bahashish" je hili mnaliongeleaje?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  nivea, je na kwenye maduka makubwa ya supermarkets nako tuwe tunaweka UNDER THE TABLE?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Utafiti huu niliufanya katika mighahawa ya mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar. Nililenga mikoa hiyo kwa sababu ni miji ambayo hutembelewa na watalii kwa wingi na ina mighahawa mingi ya kitalii ukilinganisha na mikoa mingine.UTAFITI UMEFANYIKA KWENYE MIGAHAWA MZEE MTAMBUZI.SUPER MARKET NA MADUKA NI ANOTHER CASE:A S check_03:
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  nivea, sijui unatumia mmawani kama mimi, hebu soma hapa chini:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi KASIMU CHA TOCHI MZEE MTAMBUZI HAHAHAHA NIAZIME HIYO YA KWAKO MTAMBUZI
   
 9. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,398
  Likes Received: 6,587
  Trophy Points: 280
  ilishawahini tokea arusha..katika hoteli flani ya kitalii..tulikwenda kuulizia bei ya vinyago..kati ya wamiliki wa vibanda vya vinyago hakuna aliyesimama kutukaribisha katika banda lake wote walikuwa wanatuangalia tu..mpaka tulipotoa lugha ya matusi ndio wakaonesha kutaka kutuhudumia..wakiwaona wazungu wanawakimbilia kama sijui wameona nini vile wakati kuna wazungu wengine ambao hawana pesa wamechoka zaidi yetu..
   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  mkaliwakitaa Hiyo kwa wachonga vinyago ipo sana, wao wanaamini kwamba hii ngozi nyeusi haiwezi kumudu gharama za kunua vinyago ......
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Issue hapo ni kwenye tips.

  Sema wahudumu wanatakiwa kujua kwamba kutowachangamkia wateja weusi pia inachangia wao kukosa tip, sio weusi wote hawatoi tip.

  Mimi natoa tip kutokana jinsi huduma ilivyokua. Sasa nikiingia kwenye migahawa uliotaja na wakatoa huduma mbovu kwa vile wanajua weusi wote hatutoi tip na mimi pia sitatoa tip kwa vile nimepewa huduma mbovu.

  Wao wanatakiwa kutoa huduma nzuri kwa watekja wote.
   
 12. MamaParoko

  MamaParoko JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 465
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe uko kama mimi, naangalia mapokezi kwanza na huduma then tip inategemea na hayo.
   
 13. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Nadhani pia suala la inferiority complex linahusika pia.

  Nimegundua kuwa Watanzania walioishi nchi za nje wengi ni wepesi wa 'kudhani' wamedharauliwa.

  Labda ni kwa vile wamezowea kupata huduma nzuri huko nje watokako, au labda wamezowea kubaguliwa huko watokako. Lakini kwao wao ni rahisi mno ku-shtuka wanapoona huduma ya kwake haifanani na ile alopewa Mzungu [hata kama hawana facts zote]

  Binafsi ninadhani huduma Tanzania ni mbovu na ubora wa huduma anaopata Mzungu kulinganisha na Mzawa ni ncha tu ya tatizo hili
   
 14. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi, huo ulikuwa ni mfumo wa siasa za ujamaa na kujitegemea. Utakuta nchi nyingi za mfumo huu au ule wa kikomunisti zilikuwa na sheria hii ya kukataza bakshishi. Hata China walikuwa nayo, ila sijui kama bado ipo. Kumbuka kwa mfano, wabunge wanaruhusiwa kutoa bakshishi. Sasa hii iliyopigwa marufuku uliyoiona airport ni ipi? Kwanza inabidi tuwaambie airport services watoe hilo tangazo, halina maana.
   
 15. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Mie sikubaliani na hili. Kama ni suala la inferiority complex basi tuseme wanayo wale ambao Watanzania wanaoenda kwenye hii migahawa huku katika subconsciousness yao wameshaamua kwamba wao hawastahili huduma za kiwango ambacho wanapewa wazungu. Hivyo wanapoona wanabaguliwa kihuduma compared na wazungu wanajionea sawa tu, wala sio tatizo. Kwa wenzetu Kenya hili ni jambo la kawaida kabisa, kwa kisingizio cha kukuza utalii! Hili ni tatizo nyerere alililaani kwa nguvu zote, akiliita kasumba, na kwa kusikitisha sana limeanza kurudi tena Tanzania mika zaidi ya 40 baada ya uhuru.

  Binafsi namlaumu sana Mkapa kwa kuliendekeza hili tatizo kwa kuwakuza wawekezaji wazungu isivyostahili, kiasi kwamba baadhi ya wazungu waliokuja kwa jina la wawekezaji wameanza kuwafanyia Watanzania ubaguzi wa rangi katika nchi yao wenyewe. Ni aibu sana ukichukulia kwamba tulikuwa mstari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi. Baadhi ya wazungu wa South Africa hapa nchini wanawafanyia watanzania vitendo vya kibaguzi ambavyo hata kwao South Africa wasingethubutu kamwe kuvifanya, na viongozi wetu hawaoni kama hilo ni tatizo.

  Tumeimba jeshini "kasumba ni lazima ikomeshwe, kasema Nyerere baba wa Taifa" lakini inaonekana wengi wetu tumesahau. Si muda mrefu tutarudi kwenye majina ya "kuku wa kizungu", au "anaishi "uzunguni".
   
 16. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Hata mimi pia nimelishuhudia jambo hili kwenye migahawa mingi! Ni ulimbukeni tulionao Watanzania kwa kudharauliana sisi kwa sisi, sijui tuna matatizo gani. Tunasahau kabisa kuwa hao wenye ngozi nyeupe, wamekuja kuchuma mali yetu wenyewe na fedha wanayotumia kwa sehemu ni jasho letu wenyewe! Tunapaswa kupendana na kuhsehimiana sisi kwanza ili nao watuheshimu vinginevyo dharau yao kwetu haitaisha kamwe!
   
 17. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #17
  Jun 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Synthesizer..
  mimi nafikiri jukumu la kutokobeza ubaguzi ni letu sote, japo lazima nikubaliane na wewe kuwa kiongozi wa nchi kuonyesha mfano na kuhamasisha watu wake kwenye hili tatizo ni muhimu sana. Unajua watanzania tunapigana na maadui wasiostahik.i Mfano angalie ''vita'' iliyopamba moto sasa hivi.. vita ya kipengele cha dini kiingizwe au kisiingizwe kwenye sensa.. watu wanaapizana na kufokeana utafikiria ni jambo sensitive kwelikweli. Lakini akitokea mzungu akamnyanyasa mtanzania hisikii chochote.
   
 18. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Macho, ni kweli, viongozi wetu ndio wanatupotosha na kushusha heshima yetu. Kama ni vijana kujiingiza kwenye madawa ya kulevya na Watanzania kujulikana huko nje kuwa ni wauza madawa, hizo ni ishara tu za kuonyesha kwamba nyumbani Tanzania kuna tatizo. Nchi yenye rasilimali nyingi kama Tanzania haipaswi kuwa na vijana wauza madawa ya kulevya kwa kiasi hiki.

  Viongozi wetu wengi hawana hata ile inayopaswa kuwa common sense. Tunaelewa, maana kama ambavyo mara nyingi nimeona kwenye signature ya mwana JF hapa, tatizo ni kwamba common sense is not common to everyone.

  Najua Tanzania tuna watu wenye akili wengi sana, ambao wangeweza kuongoza nchi yetu vizuri na kuipa heshima inayostahili. Lakini si watu wa namna hii ambao hujitokeza kwenye duru za siasa. In fact, kwa jinsi siasa za Tanzania zilivyokuwa siku hizi, watu wenye akili na busara hujiweka mbali sana na siasa. Huwa inatokea tu accidentally wanaweza kugundulika na kuombwa waingie kwenye mfumo wa uongozi wa nchi.
   
 19. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Kwa baadhi ya sehemu ni kweli na pia mawaiter wanaangaliaga na mwonekano wa mteja mwenyewe
   
Loading...