Je Watanzania wangetumia ushupavu wa kuchukiana kupambana na ufisadi hali ingekuwaje?

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,376
6,708
Nikiangalia jazba na mihemko mitaani na hata jamvini kuhusu waislamu na wakristo na wanavyokamiana, najiuliza jazba, utayari, usongo, mnakasha na juhudi zinazoelekezwa kwenye kuvunja na kuchoma makanisa, kuandamana hata kuwachinja polisi zingeelekezwa kwa mafisadi tungekuwa wapi kama siyo kujikomboa? Ni bahati mbaya watu wetu wako tayari kufia vitu visivyo muhimu huku wakiogopa kufia vya muhimu. Mfano, kwanini tuwe tayari kutoana roho kwa juu ya imani ambazo hakuna mwenye uhakika wake kuliko maisha yetu ya kila siku yaliyotekwa na mafisi na mafisadi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom