Je Watanzania walio ughaibuni Wanaijua Tanzania ya sasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Watanzania walio ughaibuni Wanaijua Tanzania ya sasa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngareni3, Oct 21, 2009.

 1. N

  Ngareni3 Member

  #1
  Oct 21, 2009
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa hapa Ughaibuni kwa muda sasa na nimepata bahati ya kukutana na watanzania wenzetu walio huku ughaibuni kwa muda mrefu.

  Nimejifunza jambo moja kutoka kwa hao woote.

  Watu hawaijui tena nchi yao!!!

  Inaonekana wengi wamebaki kutegemea habari za blog mbali mbali kujua kinachoendelea nchini. Mtu atakuuliza jambo la mwaka arobaini na saba hadi unashangaa.... jambo lisilo katika internet basi halijulikani. chochote unachomuuliza mtu anataka Kusearch.... mambo ya ngangamfumuni huko moshi utayapata katika internet? Mambo ya Nkasi utayapata humo? Ni kweli hapa wenyeji hawatumii tena memory zao. hata ukiuliza duka la sukari li wapi anakuambia "go to the internet and google it, it must be around here...? Toba, siye hatujafika huko...

  Mtu atakuambia vipi Beer bado ni za mgao huko? Au kwenda Arusha from Dar mabasi yanaondoka usiku? Au treni inaondoka muda gani from Dar to Moshi? etc

  Ni vizuri kujua pia Tanzania pamoja na matatizo yetu, masuala ya ufisadi, mgao wa umeme unaondelea zipo hatua kadhaa ambazo nchi yetu imepiga kwa sasa, lazima kujivunia. Huduma kutoka ktk wizara mbali mbali imeimprove kwa kiasi kikubwa. Zipo Wizara ambazo ni za kupigiwa mfano. Customer care unayoipata pale inaridhisha. Jeshi letu la Polisi pamoja na matatizo yake ya asili, lina mabadiliko ya kutia moyo. Ni wazi bado wapo polisi wachache wasio waaminifu au walioamua kutobadilika, kama msemo usemavyo, msafara wa mamba kenge wamo....

  Wengi bado wanaliwaziwa suala la uraia wa nchi mbili. Hili nadhani nami niungane na maoni ya watanzania wengi nyumbani si suala la kuendekeza. Kheri tuwe na watanzania wachache wenye moyo na nchi yao. Uraia wa nchi mbili si kwa manufaa ya nchi wala manufaa ya wananchi walio wengi.... kwanza ni watanzania wangapi wenye paspoti? hii itasababisha mafisadi wawe huru kuiba na kukimbia. najua wapo watz waaminifu wataofaidi na uraia wa nchi mbili lakini nadhaniwakati bado....

  Vinginevyo niwashauri watz hawa walio huku ughaibuni kujenga mazoea ya kurudi mara kwa mara nyumbani na kujua hali inayoendelea. Kutegemea blogs kujua hali ya nyumbani si uzalendo.....

  karibuni nyumbani, mimi nitaondoka kuelekea huko Krismas....
   
 2. N

  Ngareni3 Member

  #2
  Oct 21, 2009
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habari ndo hiyo.....
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kuwalundika mamia ya maelfu kama si mamilioni ya watanzania walioko ughaibuni katika fungu moja ni utovu wa kufikiri.Wengine wanaenda nyumbani kila baada ya mwaka mmoja au miwili.

  Na kwa taarifa mtu wa ughaibuni katika ulimwengu huu wa utandawazi anaweza kuijua bongo kuliko aliyeko mjini Dar, sembuse Malampaka huko.

  Moreover, wengine hawako interested na story hizi ki hivyo, wanasaidia familia zao na kuchill katika falsafa za Marijani Rajab za ''Kula ugali wako ukalale'

  Sikia mamboooo.
   
 4. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2009
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Huyu nae sijui anaongea lugha gani, mtu akiuliza train ya kwenda bara inaondoka saa ngapi ina maana ameshaisahau Tanzania. Watu wa ughaibuni hawategemei blogs peke yake, kuna simu za mkononi mpaka vijijini, wengi tunapata habari za nje ya Dar kabla hata hao jamaa wa mjini hawajazipata.
   
 5. E

  EAGLE Member

  #5
  Oct 21, 2009
  Joined: Oct 17, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KUDOS bluray
  Nashawishika kufikiri mtoa hoja ana tatizo binafsi ama na internet au walio ughaibuni kama anavyo waita. Je hajui hata simu watu wanapiga, wanapokea SMS na kupata habari within minutes achilia mbali wanao kwenda kila mwaka mpaka mara mbili? why the stereotype?
   
 6. C

  Chakarota Member

  #6
  Oct 21, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani tusimlaumu mtoa hoja kwani labda amekutana na mtu aliondoka 40+ years, mimi kwa maoni yangu mtoa hoja ametoa kwa nia njema kama kuwabembeleza wa-Tz walioko nje wasisahau kwao hata kwa matembezi especcially vizazi vyao,kwani kuja na kujionea maendeleo au hata si maendeleo ni bora kuliko kusikia/kuambiwa.
  Mimi nafsi yangu niliwahi kukutana na mjamaa huko Uarabuni yeye kutoka Zenj na ana miaka 34 tangu (kwa maneno yake) akimbie zenj. wakati wa karume srn. sababu aliwekwa ndani miaka 3 bila ya kusomewa kosa wala kuulizwa just kwa kua yeye alikua aki-ishi same building na Humud aliompiga risasi Karume 1972. Sasa zile adhabu na khofu alizozipata basi hana confidence tena ya kurudi anahisi kama akishuka tu watamkamata tena. Nilijitahidi kumu-assure na kumpa dhamana kua yale hayapo tena sasa,lakini amenishinda aliponita na kunionesha kwenye internet mambo yanayotendeka huko Pemba kwa mpaka leo anapigwa na kuuliwa mtu kwa kua ni Cuf hapigii voti CCM. Nilishindwa la kumjibu na nika withdraw my invitation and my guarantee that he will be safe in znz. Kweli tunaona uchungu kua mbali na ndugu zetu walioko nje lakini hatuna cha kuwavutia na cha kuringia kua Tz ni safe haven.
   
 7. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  tusione uchungu, they are safe and sound, tena hawako mbali sana basi, dunia ishakuwa ndogo hii
  mi huwa nawahofia zaidi ndugu zangu kule kijijini ambao, kuwasiliana nao na simu mpaka wani beep wakiwa kwenye network, na kuonana nao inabidi niandae au waandae safari ya siku 3 kwenda tu... hawa wa nje sms, calls, emails nje nje kilasiku, wakiamua kuja ni the matter of hours tu wametua mjini
   
 8. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Poleni sana msioijua nchi yenu ya kifisadi na giza
   
 9. K

  Koba JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Sijui nia ya mwandishi ni nini lakini seems yuko negative sana na watu wa nje maana anataka kufanya kama watu wamepotea au hawaelewi chochote,angalia comment yake ya dual citizenship yaani ni bogus bogus...watu wa nje wanajua kuhusu TZ kuliko yeye anayeishi huko na wana msaada mkubwa sana kwa ndugu zao nyumbani kuliko yeye anayejiona ni mzalendo zaidi kwa kuishi ndani ya TZ,watu wanakaa nje for a reason na kama life sio nzuri ungewaona wamesharudi zamani sana,acheni kujilinganisha na watu nje,wewe do your thing na wenyewe watafanya ya kwao hawajakuomba msaada wowote!
   
 10. p

  p53 JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35


  Walewale...
   
 11. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #11
  Oct 21, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  You can know Tanzania more now than before, we have radio, blogs, news paper, maps and youtube.

  I have some friends , graduates from UDSM they have internet in their working stations, they neither know JF nor any websites of Tanzanian online news paper!

  It depends on individuals it does not matter where are they!
   
Loading...