Je watanzania waishio nje wana nafasi yoyote kwenye mfumo wa siasa wa nchi yetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je watanzania waishio nje wana nafasi yoyote kwenye mfumo wa siasa wa nchi yetu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Richard, May 1, 2012.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Hili swali limenijia baada ya kuona majaribio kadhaa ya baadhi ya watanzania kama vile bwana Mwakalinga alipojaribu kugombe jimbo la Kyela kwa kushindana na Dr Harrison Mwakyembe, pia Dr Shayo na juzijuzi bwana William Malecela ambao wamejaribu kugombea nafasi ya ubunge kwenye bunge la Afrika Mashariki.

  Ni mategemeo ya watanzania wengi ambao wengine wamediriki kujiingiza katika nafasi mbalimbali za uongozi katika matawi ya CCM yalizagaa nje ya nchi hususan Ulaya na Marekani.

  Je ni sababu zipi ambazo zinawafanya watanzania hawa kushindwa kuingia kwenye mfumo wa siasa wa Tanzania ukizingatia kwamba wao ni watanzania na ni wanachama wa CCM na wamezaliwa nchini Tanzania kusoma hapo na kwenda tu nje ili kuongeza maarifa katika fani zao mbalimbali?

  Mimi kama Richard sina uanachama wowote katika chama chochote cha siasa na nnapenda kuendelea kuwa "analyst" tu au mfuatiliaji wa mambo mbalimbali lakini nimekuwa nikitatizwa na jambo hili kuhusu kutokubalika kwa watanzania waishio nje kutoka kwa watanzania wenzao.

  Je wanaonekana si watanzania, ni wageni na siasa za Tanzania, je watabadilisha mambo mengi ambayo watu wengi hawatapenda kwa nia njema tu au ndio wamekwishapotea kwa wao kuamua kuishi nje ya nchi.

  Ningependa kuona hoja mbalimbali zinatolewa kutoka kwa watanzania wenzangu wale walio nyumbani Tanzania na wale wanaoishi nje kwamba nini tatizo hapa.

  Nini maoni yako, karibu.
   
 2. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu Richard,
  Hongera kwa maswali mazuri na ya maana kubwa mno, mimi hili swala limeniumiza kichwa sana hasa siku bungeni wale mabingwa wa kweli walipopigwa chini katika kuwachagua ma mp wa EALA.
  Nilichojifunza ni kuwa sisi tukubali kwanza kuwa mfumo mzima wa nchi ni wa zamani na wenye ujinga mwingi, situkani kwa nia njema nasema sisi ni wajinga.
  Rai wetu mwenye uzoefu tu wa nje lakini sio alimradi nje, nchi zilizostaarabika, hata kama hana cheti hata moja, lakin anaweza leta maendeleo kuliko profesa mwenye ma phd wa hapa nyumbani.
  ila wale wabunge waliokuwa na CONGRETE PROGRAMs walipigwa chin kwa sababu ya kuwa tu walipojieleza walikuwa too transparrent hawakuwa na manjonjo kama hao walioshinda, kwa kuwa wameshakuwa really civilised, hawakutumia uhuni bali walieleza clearly what will be done in a very gentlemen way, cha kushangaza wale wote wazuri isipokuwa moja au wawili tu. ilikuwa bora wangetueliwa kamati ya kuwachagua sio mambumbumbu waliokaa tu bungeni samahani kamantusi
  Kwa hiyo kama Tanzania maendeleo tuyategemee ujinga ukiisha sijui lini
   
 3. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Kama tatizo ni kuwepo kwa mfumo mzima wa nchi ambao ni wa zamani, je ni mfumo upi huo na kama upo ni nani wa kuubadilisha?
   
Loading...