JE WATANZANIA TUPO TAYARI KWA TRAIN (as public transport) DAR.........

kupe

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
1,035
326
Tatizo la Watanzania wengi wao wanapenda vitu virahisi rahisi.au story wanavyosikia vijiweni kuwa ulaya kuna public transport kuna ma tren ya umeme ,wao wanadhani ni kama kufumba macho na kufumbua . Haya mambo hayataki mzaha kama wa huku kwetu , yanataka u serious . wao wamewekeza hela za kutosha NA UMAKINI WA HALI YA JUU . na raia wao wamestaarabika vya kutosha . ni kweli kuwa ulaya wapo wasio na akili, mateja (wavuta unga ) na masikini ...... lakini sio kama mateja na masikini wetu. wote hao wanao ustaarabu. kabla ya kufikiria mambo ya train je wananchi wetu wako tayari na mazingira yanaruhusu kwa usafiri huo wa kistaarabu na haraka. maana tren ya umeme inataka
ustaarabu wa hali ya juu. inakwenda kwa muda. hakuna kondakta wala mpiga debe .hakuna wa kumwambia au kumuomba eti kama nauli umepungukiwa .mara mtu kaingia na samaki wanavuja maji kwenye tenga , mwingine kaingia na chakula mchana kwenye ma plastic na ndoo anapeleka posta kuuzia wafanyakazi . Na sio daladala zenu mlizozoea tajiri mwenye gari mjinga . dereva naye mchafu hana akili na konda mchafu hana akili na baada ya kumaliza kazi dereva analala guest na konda analala kwenye dcm anajisaidia kwenye mfuko wa plastic bag (rambo)harafu anatupa barabarani asubuhi wakiamka wanaanza kazi. Train ni ghali sana kuziendesha sio mchezo . zinataka service ya uhakika .Watanzania sio mnakubali tu kila mnachoambiwa . boresheni kwanza usafiri huu mlikuwa nao sasa hivi kabla hamjavamia huko. tren yenyewe na vituo vyake huko ulaya au huko mnakofananisha ni visafi kuliko airpot yenu. au sijui stand ya basi mkoa ubungo.Au mnataka baada ya miezi sita ziwe miguu juu kama UDA. MIMI NAFIKIRI BADO HATUJAWA TAYARI NA HAYA MAMBO YA TREN LABDA KAMA NI MRADI WATU WANATAKA KULA SAWA
 
Back
Top Bottom