Je, Watanzania tunataka uhuru wa habari?

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,470
5,477
Katika ulimwengu wa sheria na mamlaka huwa kuna haki vs wajibu

Kila haki ina wajibu. Vivyo hivyo, uhuru wowote una mipaka.

Leo ntaka nilete mjadala juu ya uhuru wa habari na iwapo kama taifa tunahitaji media yetu kuwa censored. Mimi sio guru wa maswala ya media ila naamini kwamba Uhuru lazima uwe na mipaka.

Swali la kujiuliza ni nani mwenye mamlaka ya kuweka mipaka hiyo? Ni nani anaamua kwamba sasa hapa habari hii isiende hewani na anatumia vigezo gani? Nani anaamua kwamba h/abari hii uliyotoa sio sawa na kutoa adhabu kwa vyombo vya habari?

Je, media censoeship iwe tu katika maswala ya kisiasa? Je, kunaweza kuwa na open media censorship?Je ni media gani ziwe censored na zipi zisiwe censored?

Je, haki ya individuals kupashana habari je inalindwaje?Je, haki ya faragha inalindwaje?

Naleta mjadala huu kwa sababu naamni kabisa kwamba uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu sana kama mhimili wa tano.Mhimili wa nne ukiwa ni nguvu ya umma.

Tujadili hapa ni kwa kiwango gani watanzania wanataka uhuru wa habari na kwa malengo gani? Kuleta chokochoko? Kusambaza umbea, kufanya uchochezi?

Tujadili hapa tukizingatia desturi zetu na hali ya nchi yetu na uwezo wa media zetu.
 
Mpaka dikteta aliyepo madarakani ang'oke ndio uhuru wa vyombo vya habari utarudi. CHADEMA tufanyieni kazi hiyo.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
UHURU WA HABARI UNAOTAKIWA NI ULE WA MEDIA KUWA HURU KURIPOTI AU KUTOA MAONI BILA KUBUGUZIWA HATA KAMA HABARI HIZO ZINA NEGATIVE OPINION KUHUSU MAMBO MBALIMBALI AMBAYO SERIKALI INAYATEKELEZA

Mfano leo hakuna mtu asie jua jambo jema alilofanya Mh.Rais kujenga UKUTA wa Mererani maana tunaanza kuona matokeo yako.

LAKINI LEO MFANO AKITOKEA MTU(najua hayupo) AKAJA NA NEGATIVE OPINION NA AKAWA NA HOJA ZA MASHIKO KUHUSU UJENZI WA HUO UKUTA NA AKAIWAKILISHA VIZURI ASIBUGHUZIWE ETI KWA KUWA KATOA HABARI/MAONI AMBAYO YANAONEKANA KAMA NI KUPINGA MAZURI YALIYOFANYIKA
 
Moja ya viashiria vya kutokuwepo kwa Uhuru wa habari ni kitendo cha Media zote kubwa Tanzania kuogopa kurusha mkutano wa Chadema leo.
 
Uzi kama huu unanisaidia sana kuelewa uelewa watanzania, Kwanza hakuna wachangiaji. Wengi wa wachangiaji ni Biased. Ila tuendelee na mjadala kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa uhuru.
 
Uzi kama huu unanisaidia sana kuelewa uelewa watanzania,Kwanza hakuna wachangiaji.Wengi wa wachangiaji ni Biased.Ila tuendelee na mjadala kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa uhuru.
Hasa Lumumba huwezi kuwakuta kwenye huu uzi.
 
Tunautaka sana uhuru wa habari Nchini ambao huyo dikteta anazidi kuuminya siku hadi siku ili tu aimarishe udikteta wake na hii imesababisha baadhi ya vyombo vya habari kufungiwa na yule Kabendera kubambikiwa kesi iliyosababisha kifo cha mama yake.
 
Tunautaka sana uhuru wa habari Nchini ambao huyo dikteta anazidi kuuminya siku hadi siku ili tu aimarishe udikteta wake na hii imesababisha baadhi ya vyombo vya habari kufungiwa na yule Kabendera kubambikiwa kesi iliyosababisha kifo cha mama yake.
Mkuu unautaka kweli?Unautaka kiasi cha kuwa tayari kufanya chochote ili uupate?
 
Ijumaa ilikuwa Eid ya Waislamu lakini tv zote bado zinaleta nyimbo za kanisani hakuna hata kuona Waislam wanaongelea sikukuu yao kwenye media na wapumbavu bakwata tawi la Wakatoliki walikaa kimya na wakipewa nafasi wao wanaongelea amani ya nchi wakati Waislamu wanataka kujufunza dini yao kupitia media.
 
Back
Top Bottom