Je, Watanzania 'tulioshadadia' Mitandaoni 'Kumfitinisha' Msanii Diamond Platinumz na Tuzo za BET ambayo ameikosa tuliifikiria Tanzania zaidi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,518
108,793
1. Je, wale 'Washadadiaji' wa Mitandaoni tunajua kuwa aliyeshindwa huko BET siyo tu Msanii Diamond Platinumz pekee bali hata Watanzania wote tumeshindwa?

2. Je, wale 'washadadiaji' wa Mitandaoni tunajua kuwa Kitendo cha Diamond Platinumz Kuikosa hii Tuzo ya BET kuna Fursa kadha wa kadha Tanzania inaenda Kuzikosa?

3. Je, wale 'washadadiaji' wa Mitandaoni tunajua kuwa Kitendo cbetu cha Kiswahili na Uswahili wetu wa Kumshambulia ( Kumsagia Kunguni ) Diamond Platinumz huko nje ( katika Mataifa mengine ) kimetufanya tuonekane ni Wapumbavu wakubwa?

4. Je, wale 'washadadiaji' wa Mitandaoni tulijiongeza kabla ili kujua kuwa 'Music Industry' ya Tanzania ambayo pia ingechochea Ajira kwa Watanzania ingefanikiwa zaidi kama Msanii Diamond Platinumz angefanya vyema katika Tuzo za BET?

5. Je, wale 'washadadiaji'wa Mitandaoni tunajua kuwa katika hili la Kumuunga mkono Msanii wetu Diamond Platinumz tulipaswa tuweke pembeni Chuki zetu nae kwa muda ili afanikiwe na atungarishe vyema Watanzania Kimataifa na huenda angekuwa pia ni Kivutio kikubwa cha Wageni ambao wangemiminika Tanzania na hata Kukuza Uchumi wetu kwa namna moja au nyingine?

6. Je, wale 'washadadiaji' wa Mitandaoni tunajua ya kwamba pamoja na Roho Mbaya zetu 'zilizotukuka' za Kumchafua na Kumfitinisha Msanii wetu Diamond Platinumz bado Yeye ( Nasib Abdul ) anaendelea kubakia Bilionea na Utajiri wake huku Sisi Umasikini wetu na Shida zetu za Kimaisha zikizidi tu Kulundikana kama si Kujilimbikiza kwa Baraka zake Shetani ambaye muda mwingine huwa anatushangaa Watanzania?

7. Je, wale 'washadadiaji' wa Mitandaoni mna habari kuwa hata huyu Msanii Mshindi wa hizi Tuzo za BET nae huko nchini Kwake anasakamwa mno na Watesi ( Critics ) wake hadi Kupigwa 'Madongo' ila katika Kipindi cha Kumpigia Kura huko waliweka tofauti zao pembeni na hata huko ( humu ) Mitandaoni walihakikisha hawamchafui ili Mataifa mengine tujue 'Mapungufu' yake?

Nami GENTAMYCINE namalizia kwa kusema ya kwamba ifike muda Watanzania tuacheni kuwa Washsmba na wenye Roho za Kishetani na Kichawi kama tulizozionyesha katika Kumchafua na Kumfitinisha Msanii Nasib Abdul ( Diamond Platinumz ) na tutambue kuwa Kitendo tulichokifanya ni cha Kipopoma ( Kipumbavu ) mno na tusikirudie tena kwa Msanii mwingine hata kama ni mwana CCM au mwana CHADEMA au ni 'Pro Government' pia.

Kama mpenda Burudani nimeumia mno.
 
Pole sana ila Sadala anastahili alichopata ulikwepo kipindi cha kampeni
 
Pole sana ila Sadala anastahili alichopata ulikwepo kipindi cha kampeni
Tulipaswa tumchukie zaidi Msanii Diamond Platinumz ( Nasib Abdul ) kwa ajili ya Chuki zetu nae za Kisiasa Yeye akiwa mwana CCM kama Mimi GENTAMYCINE na Wewe pamoja na Wenzako mkiwa ni wana CHADEMA au tulitakiwa tuiangalie zaidi Tanzania kama nchi ( na Fursa nilizozitaja ambazo tungezipata ) Yeye akiwa ni 'Flag Bearer' wetu katika Mashindano haya / Tuzo hizi?
 
Theoretically ni sawa uhalisia hell no na tutabaki hivyo ... ccm na cdm lini walikaa meza moja kujadili agenda mfano leo mama hataki katiba mpya na hana option ingine
 
Theoretically ni sawa uhalisia hell no na tutabaki hivyo ... ccm na cdm lini walikaa meza moja kujadili agenda mfano leo mama hataki katiba mpya na hana option ingine
Nadhani Familia yako upesi sana inatakiwa ipige Simu katika Hospitali ya Wagonjwa wa Akili ili uwekewe Kitanda chako tayari kwa kuanza Matibabu yako Kesho uweze Kupona.

Tumemsikiliza Mama ( Mheshimiwa ) Rais Samia Suluhu Hassan vizuri kabisa na hakuna aliposema kuwa hataki Katiba Mpya ila Kiungwana kabisa na wenye Akili tumemuelewa ametuomba tumvumilie ili aiweke nchi sawa Kiuchumi na atulie kisha hili la Katiba litakuja tu.

Huwa nawaheshimu mno Watu wa CHADEMA ( hasa kwa Mawazo yao mithili ya Madini ya Thamani Migodini ) na japo Mimi GENTAMYCINE ni mwana CCM na sioni Aibu ( Haya ) au Uwoga Kukiri hili ila sijawahi kukutana mwana CHADEMA wa hovyo hovyo ( Fool ) kama Wewe JF.
 
Inatakiwa kuwa fundisho kwa wasanii wengine wasiige mafano wa Naseeb Abduli kusapoti ukandamizaji wa haki za watanzania. Badala yake wasimamie haki za watanzania.

Haina maana ya kushadadia hayo yoote uliyoyataja eti tumeyakosa wakati hata haki tuu hatuna na hatuwezi kuipambania. Ni hatua nzuri na wasanii wengine wajue wajibu wao kwenye jamii yao. Siyo tuu kuunga juhudi kila kitu.

Na jambo ambalo hujajua ni kuwa waliohusika kushadadia sio wana Chadema bali ni watanzania wapenda haki. Ukijiona wewe sio mpenda haki huwezi kuwa upande wa hao uliowaita Chadema utakaa upande wa wasiopenda haki hao uliowaita CCM.
 
Mkuu wewe ndiye ulimshauri aimbe 'acha nikae kimya' wakati wa utekaji?maana alionesha kiwango kidogo sana cha ufahamu.Anataka awe wa kimataifa wakati akili yake si 'precautious'!
 
Tulipaswa tumchukie zaidi Msanii Diamond Platinumz ( Nasib Abdul ) kwa ajili ya Chuki zetu nae za Kisiasa Yeye akiwa mwana CCM kama Mimi GENTAMYCINE na Wewe pamoja na Wenzako mkiwa ni wana CHADEMA au tulitakiwa tuiangalie zaidi Tanzania kama nchi ( na Fursa nilizozitaja ambazo tungezipata ) Yeye akiwa ni 'Flag Bearer' wetu katika Mashindano haya / Tuzo hizi?
Mkuu kwani huko CCM hakuna wapigakura wa tuzo za BET?
Mbona unatuchosha ulitakuwa kuwahamasisha mapema hao wanaompenda wampigie kura. Game is over, kilichobaki na fundisho tu.
 
Kwanza nani Kawaambia ile ilikuwa tuzo kwa taifa? Ile ni tuzo kwa mwanamuziki sio kwa watanzania au waganda au wakenya ndio maana hakukua na uwakilishi wa mataifa bali wa vipaji. So msituchanganye kuna mambo ya kitaifa na mambo ya mtu binafsi. Hicho ndicho hiyo sekta ilichochagua. Mambo ya muziki wa dunia nasisi wachungaji wapi na wapi bro? Kuna watu wengine hata huo mziki wake hatuujui halafu mnasema ni jambo la taifa, acheni kutafuta kivuli kwenye sebule za watu mkiwa na matope mtachafua sebule zenyewe.
 
1.....tunajua kuwa aliyeshindwa huko BET siyo tu Msanii Diamond Platinumz pekee bali hata Watanzania wote tumeshindwa?
popoma mimi niondowe hapo. mlioshindwa ni wewe na kundi la mapopoma wenzio akiwemo huyo aliyekosa tuzo.
 
BET, Emmy, Grammy, CMT na taasisi nyingi kubwa za kimarekani huwa hawatoi tuzo zao kwa kusikia maneno ya mtandanaoni. Wana vigezo vyao na majajai wataalamu wnompima kila mgombea kwa kutumia vigezo hivyo. Waliokuwa wanapiga kelele mtandanao walikuwa wanaabisha tu lakini hawakuwa na affect yoyote. Diamond kaikosa kwa vigezo; tuzo hizo siyo kama zile za AFRIMMA za nani kapata wafuasi wengi mtandani ambapo mgombea anaweza kuwalipa watu wengi wampigie kura mtandaoni mara nyingi tu.

Ila watanzanaia tumesonyesha ujinga sana kupigia kelele nominationa ya Diamond as if yeye ni special sana badala ya kuacha utaratibu uchukua mkondo wake. Nimemwona Burna boy aliingia kwenye red carpet akiwa mtu simple tu bila mbwembwe zozote.
 
BET, Emmy, Grammy, CMT na taasisi nyingi kubwa za kimarekani huwa hawatoi tuzo zao kwa kusikia maneno ya mtandanaoni. Wana vigezo vyao na majajai wataalamu wnompima kila mgombea kwa kutumia vigezo hivyo. Waliokuwa wanapiga kelele mtandanao walikuwa wanaabisha tu lakini hawakuwa na affect yoyote. Diamond kaikosa kwa vigezo; tuzo hizo siyo kama zile za AFRIMMA za nani kapata wafuasi wengi mtandani ambapo mgombea anaweza kuwalipa watu wengi wampigie kura mtandaoni mara nyingi tu.

Ila watanzanaia tumesonyesha ujinga sana kuipgia kelele nominationa ya Diamond as if yeye ni special sana. Nimemwona Burna boy aliingia kwenye red carpet akiwa mtu simple tu bila mbwembwe zozote.
Barna boy sio mshamba wa kuvaa mpk mavazi ya kike ya wamasai wkt yeye ni mwanaume kisa tuzo.
 
Back
Top Bottom