Je, watanzania ni nini cha kujivunia kwa sasa, amani au utulivu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, watanzania ni nini cha kujivunia kwa sasa, amani au utulivu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nhunda, Feb 22, 2011.

 1. N

  Nhunda Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanajamii nimekuwa nikijiuliza nikipi ambacho mtanzania ana jivunia kwa sasa? zamani watanzania tulikuwa tukijivunia Amani. Je ni sahihi kuendelea kujivunia Amani? Je nikweli Tanzania inastahili kuendelea kuitwa Kisiwa cha Amani kamailivyo zoweleka kuitwa?

  Mimi ndugu wanajamii ningependekeza wanasiasa wetu wasiendelee kusema Tanzania ni Nchi ya AMANI na badala yake waseme Tanzania ni Nchi ya UTULIVU. Kwasababu watanzania tunajitaidi sana kuwa watulivu katika nchi isiyo na amani hata kidogo nchi iliyo jaa kila aina ya uchafu, mauwaji ya kila aina, ufisadi wa kuonekana hata kwa asiyeona na uzembe mkubwa wa viogozi serikalini. Haya yote watanzania tunayavumilia na kuendelea kuwa WATULIVU. Ama kweli Tanzania ni kisiwa cha utulivu na sio kisiwa cha Amani.

  Watanzania tunazidi kuwa watulivu hata pale tunapopokonywa haki zetu kwa mfano juzi tu kwa uzembe uliosababishwa na serikali watu wamekufa kwa mabomu Gongo la mboto lakini watanzania tukaimarisha utulivu wetu, watu wamepigwa mabomu ya machozi Arusha bila sababu ya msingi utulivu tumeuenzi.

  Kwahiyo ndugu wanaJf kwa upande wangu Tanzania si Nchi ya Amani kwasababu Serikali inavunja chembe zinazofanya Amani iitwe AMANI lakini inatumia uvumilivu walionao watanzania kama faida yake ya kujitangazia kwa mataifa kuwa TZ ni Nchi ya AMANI. Ninadhani serikali inatudhurumu ingekuwa inatanganza kwa mataifa kuwa watanzania ni wavumilivu ingetutendea haki zaidi, je wewe mwanajamii waonaje?
   
 2. kwamtoro

  kwamtoro JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2014
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 4,815
  Likes Received: 770
  Trophy Points: 280
  Watawala wanafanya ujinga, tukighadhabika wanakimbilia kujifunika kwenye shuka LA amani. Amani, amani inatunyonga kila kukicha. Watanzania tuanze kulichukia hili neno amani tuwekane sawa ili tuheshimiane na kila moja atekeleze wajibu wake kwa kutomuona mwenzake mjinga kwa kukimbilia neno kuu la watawala amani
   
 3. F

  Faridi JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2014
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 674
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 60
  Watanzania ni waoga,lakini ieleweke paka akiwa muoga ukimukimbiza akifika kwenye kona na akaona hana pakukimbilia atageuka nyuma na kukuparura.
   
Loading...