Je, Watanzania mmejiandaa vipi kisaikolojia kwa ujio mpya wa Richmond (Dowans)?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,052
40,715
Update: 16/05/2023
Hayawi hayawi sasa yamekua. Megawati 180 kwa miaka 25 Zanzibar



Update: 04/12/2022

==========================
Update: 08/12/2022


========================
Tumeshuhudia nguvu kubwa ikielekezwa kwenye kuutangaza ukame sambamba na kutangaza upungufu wa umeme kutokana na kuoungua kwa maji, hiyo ni pamoja na meneja wa bwawa la mtera kukanusha kwamba uzalishaji umeme umepungua kwani maji yapo ya kutosha, hivyo hatujui wa kumuamini.

Pia tumeshuhudia waziri mwenye dhamana akifanya ‘publicity stunt’ kwa kuruka na ‘helicopter’ ili kuutangaza ukame kwa kishindo zaidi huku akimtumia mwanahabari nguli kabisa aitwaye ‘Millard Ayo’, kama vile anavyotumiwa na GSM na Palm village kutangaza bidhaa zao, hapa bidhaa inayotangazwa ni ukame.

Pia katika ziara hiyo ya kuutangaza ukame, amenukuliwa akisema kwamba wameshuhudia ukama wa kutisha, na wanachukua hatua za muda mfupi kutatua tatizo. Hii ikanikumbusha mwaka 2006 tulipoambiwa mvua hazitaweza kujaza mabwawa hata baada ya miaka 10, na hivyo Lowassa akishirikiana na Ngeleja, Singasinga na Rugemarila, wakatupiga mtama wa wima wima kwa kuagiza mitambo ya kukodi ya Richmond ambayo ilibainika kuwa ni kampuni ya mfuko wa shati, na haipo popote duniani zaidi ya kwenye mafaili tu.

Wiki haikupita tangu waagize, zikanyesha mvua kubwa hadi mabwawa yakataka kupasuka, ikabidi wafungulie maji, umeme ukarudi katika hali ya kawaida, lakini Lowassa na wenzake wakaendelea kula capacity charge ya milioni 150 kwa siku bila kuzalisha umeme hata chembe. Zengwe likaibuka bungeni, Mh. Harisson Mwakyemba akamvalia dera Lowassa, Lowasaa ikabidi ajipige mtama wa kifudifudi mwenyewe na kuachia ngazi. Kupooza aibu ikabidi mitambo ibadilishwe jina, ikaitwa Dowans, halafu tukaambiwa tuinunue kwa bilioni 100, bunge likagoma, tukaendelea kuikodi na kulipa capacity charge , umeme ukapanda bei vinaya mno!

Watu wakala sana kupitia umeme, Dowans ikaitwa Symbion, watu wakaendelea kula, IPTL nayo watu wakaendelea kula, wakachota mpunga wote Escrow, tukabaki tunashangaa kama mtoto mdogo aliyenyang’anywa jojo, asijue alie au acheke..., akaja Mwamba wa Kaskazini , Jiwe la Majiwe, Jabali la Majabali, pande la mtu, J. P. M. ; Mola ailaze roho yake mahala pema peponi 😭😭😭😭😭😩😩😩😩😩😩😩, akawapiga Tanganyika Jeki jizi liliogawa pesa kwa akina Methodus Kilaini wa Kanisa katoliki, Anna Tibaijuka, Ngeleja, Kupitia benki ya Mkombozi ya Kanisa Katoliki, watu wakaenda na viroba kupokea pesa, Mama Tibaijuka akanunua Mboga za milioni 40, hadi leo bado anakula hizo mboga, Chenge akalamba bilioni 1.6 na wengine wengi tu, ili kuua soo la wizi kupitia hii Sekta, jizi hilo si lingine bali ni Rugemarila na yule Singasinga, JPM akaja kugundua kwamba kulikuwa na mchezo wa kufungulia maji usiku ili kuleta mgao na hivyo kukodi mitambo kwa bei mbaya, na alilisema hili bila aibu siku ya kwanza anahutubia bunge, je, huu mchezo umerudi tena?!

Kipindi chote cha JPM kikaoita salama, fast forward 2021 mama anapokea kijiti, Makamba anapewa seat ya mbele kimkakati, ghafla tunaambiwa kuna mgao, from nowhere, na publicity stunt zimeanza kuupromote ukame as if ni bidhaa iliyosokoni, nyie manuza ukame au ni nini?!

Badala ya kupanua miundo mbinu ya gesi Kinyerezi wanaleta porojo za ‘ufumbuzi wa muda mfupi’. Sasa mimi nasema hivi, siko tayari kuona upigaji wa akina Ruge unarudi, tutalala uchi barabarani safari hii, jaribuni sasa.

=======











 
Dah, namba lazima zisomeke.

Ile juzi ya kuruka na helikopta nilihisi kabisa ni mbinu ya kujitetea kuna ukame ili wapate ruhusa ya kuanza kukodi hayo mamitambo wapige hela.

Na muda huu hawajaishia kwenye umeme, wameenda mbali zaidi kwemye migao ya maji.

Kipindi cha Magu hakukuwa na mambo ya mgao na huwezi kukanusha kwasababu kwa macho yetu tulishuhudia.

Tanzania tunarudi kule kule tu, Tajiri wa bungeni ambae hata akitumia jenereta mwezi mzima atajuaje shida ya mgao?
 
Back
Top Bottom