Je, Watanzania Kuiomba BAE na Serikali ya Uingereza Pesa za Rada zisirudi Serikalini ni Kukosa Uzale | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Watanzania Kuiomba BAE na Serikali ya Uingereza Pesa za Rada zisirudi Serikalini ni Kukosa Uzale

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zimmerman, Jul 15, 2011.

 1. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Hili ni swali lililojitokeza indirectly katika kipindi cha majadiliano cha Star TV™ –Tuongee Asubuhi – kuhusiana na mustakabali wa pesa za Rada kurudi Tanzania. Lengo la Star TV™ lilikuwa ni kupata maoni ya mtanzania wa kawaida kuhusiana na suala hilo. Katika jopo la majadiliano alikuwepo pia Job Ndugai, naibu spika wa bunge la JMT. Huyu ndie aliyeongoza msafara wa wabunge kwenda UK kuzidai hizi hela na maoni yake yalikuwa muhimu ili kupata picha halisi ya kile kinachoendelea.

  Sasa katika kuelezea yaliyojiri kwenye msafara wao, Job Ndugai akaulizwa na mwongozaji wa kipindi kuhusiana na wasiwasi walionao watanzania wa kawaida katika suala la hizi pesa kurudi kupitia mkono ule ule uliozipuyanga mwanzo. Na, oh, kitu kipya nilijokifahamu leo tu ni kuwa kumbe hizi pesa ni mkopo kutoka benki ya Barclays (yaani, unachukua mkopo wa riba kununua kifaa kisicho muhimu kwa maendeleo ya msingi ya nchi maskini, what a strange nation!). Tuendelee. Sasa Job akajibu, akasema hata yeye alishangaa pale alipoona analetewa makabrasha ya barua za wazi watanzania walizotuma kupitia mtandao kwa serikali ya UK na BAE kwamba hizo hela bila wasiwasi zitapuyangwa tena kwa sababu bado serikali ni ileile, ya chama kile kile, wezi wale wale waliosafishwa na bunge juzi juzi tu kwamba ni wasafi. Job akashangaa, akawaza, eti inawaezekana watanzania kweli wakakosa uzalendo kiasi hiki, yaani, cha kutoiamini serikali yao kiasi kwamba hata hela za kuwanufaisha watanzania bado hawataki zirudi Tanzania?


  Well, kwa kifupi kila mmoja hapa anaweza akawa na majibu yake katika hili; wapo wengine kama Job wanaona ni kukosa uzalendo, na wapo wengine wenye maoni tofauti na Job.

  Mimi kwa maoni yangu waliotuma hii barua ya wazi huko Uingereza ni wazalendo, tena sana. Baadhi yao ni watanzania walipa kodi sana tu, baadhi yao wanafanya kazi kwa bidii siku zote wakati mwingine hata Jumamosi na Jumapili na siku za sikukuu bila posho, baadhi yao ni wastaafu walioitumikia nchi hii pengine hata kuhatarisha maisha yao, na hawapingi hizi hela zisirudi Tanzania kuwanufaisha watanzania, ila wanapinga zisirudi kupitia mkono ule ule uliozitapanya. Kama Job Ndugai hawezi kulielewa hili naye ni naibu spika wa bunge, basi, Tanzania tujihesabu hatuna viongozi wanaoelewa mambo ya msingi kwanza.
   
 2. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa mmojawapo ya waliotuma barua za kuunga mkono hoja ya BAE ya kurejesha 'chenji' hiyo kupitia NGOs badala ya kuzirejesha mikononi mwa wezi wale wale. Katika b-pepe yangu nilitumia neno wezi (thiefs) na mfumo wa wizi wa kidola (kleptocracy). Nilifarijika sana kusikia kuwa BAE waliyapa uzito maoni ya Watanzania. Mimi ni mzalendo!
   
 3. mulambakao

  mulambakao Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni swala la aibu ambayo mimi m-Tanganyika mzalendo naona aibu kwa niaba yao, kwanza they weren't supposed to even question, not furthest going there tena kundi kubwa kabisa still using wazalendoz quick cuts, man, this shame mwajua hata wale wazungu wanatushangaa, how can one even start perceiving that. Kwanza hata tuhuma za rada walizikataa, then how the hell ten baada ya kuwaita watu makini na shupavu walioi-rais issue na kufukuzwa bungeni ati siyo wazalendo, lets respect ourselves during this period of living so that the future can not think of us being unadorable ghosts!
   
 4. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Mimi nituma tena nilitmia email zangu zote na nikafungua kama email 7 mpya kisha nikatuma tena, Mimi ni Mtanzania na siiamini Serikali ya Kikwete kwa kuwa ni ya Kifisadi, Kibinafsi, haifuati utawala wa Sheria, Corrupt na Sina imani nayo
   
 5. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45

  Mimi nilishatuma siku nyingi,

  Original massage
  We Tanzanians do understand that BAE Systems has formed an advisory board on Tanzania chaired by Lord Cairns in line with the settlement agreement with the UK 's Serious Fraud Office (SFO), approved by the UK’s High Court in December 2010. As part of the settlement BAE Systems agreed to pay the sum of £29.5 million for the benefit of the people of Tanzania.

  We are aware that a group of Tanzania all party parliamentarians have visited Britain to press for the payment of the settlement of 29.5 million pounds through the Tanzania’s Government rather than Non- Governmental Organizations (NGOs).

  On behalf of my fellow citizens who have no access to communication with you and are also monitoring this issue very closely and I want to express our strong support to BAE System for its decision to return the money to the Tanzanian people through NGO's instead of the same tainted corrupt Tanzanian Government officials. Please bear in that this all party parliamentarians visit in Britain is costing us already.

  Thank you for your continued cooperation.

  Yours sincerely,
  Angalia response

  "Thank you for taking the time to email us. I will ensure your comments are passed to our advisory board.
  Kind regards
  Lindsay"
   
 6. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Ndugai na serikali yake ya CCM waache unafiki..kwanza walisema hilo deal la rada lilikuwa safi na halina mawaa kwa hiyo kufuatilia hiyo hela ni unafiki at the highest level. Huyo ndugai aeleze pesa za EPA ziko wapi?
   
Loading...