Je Watanzania Huwa Na Nyimbo Za Kikabila Zinazosifika?

Sio Watanzania wote huwa wametelekeza asili yao, hususan Watanzania wanaoishi kwenye mipaka na nchi jirani. Ukiangalia kwa mfano huyo Saida Kaloli ametokea kwa Wahaya, nyimbo zake huwa zinapendwa sana Uganda maana Wahaya wapo mpakani na nchi hiyo.
Ukienda hata kule Kigoma wanapenda sana kucheza nyimbo zao za asili maana wamepakana na Warundi. Pia ukienda kwa Wanyakyusa kule Mbeya unakuta wamekaribiana na Zambia, Kwa kifupi ukiangalia Watanzania ambao bado wanapenda lugha zao za asili utakuta kwa njia moja au nyingine wanatengamana na makabila ya kutokea nchi jirani.
Lakini ukiingia ingia ndani wengi hata hawajui salamu kwa lugha za asili, kazi kuvaa milegezo hapo Dar na kupaka 'poda'.
What a poor research,
Mimi natokea Iringa, Naona jinsi huijui Tanzania.
Umekuwa ni wa Kawaida sana kaka.
 
Huku Kenya pia si jambo nzuri kuzungumza kikabila mkiwa na asiyeelewa hio lugha! Hapo sasa mtatangamana kivipi?

English and Kiswahili ni lugga mbili zinazotumiwa na wakenya kutoka tabaka mbali mbali kuungana.

Watanzania wengi wanazungumza Kiswahili kuliko makabila yao.
Kila siku nagombana na Wakikuyu wakikutana wawili hata wakiwa group la watu kumi wasio Wakikuyu hu-switch to Kikuyu bila aibu.
 
Sikusema umehama mada, nilisema umeacha point ya awali ya mikoa ya katikati mwa Tanzania kutokuwa na nyimbo za asili, ndo nikawa nasubiri utaje hiyo mikoa ili nikuonyeshe utamaduni wao maana kwa hali kusafiri tu kawaida sio rahisi kujua mambo ya ndani kama haya!

Kuhusu suala la kuksanya nyimbo za makabila tofauti kutoonyesha kuwa nadumisha asili yangu kama unavyodai!

Labda nikueleze hivi, ukiongelea asili unagusa nyanja nyingi! Kuna asili ya kabila, nchi na pia rangi/races. Sasa ukiongea kuwa tumemezwa hatuna asili, unamaanisha asili ipi?

Asili ya kabila utakuta kila kabila lina utamaduni wao unaowatambulisha na kuwatofautisha na kabila jingine japo baadhi ya mambo yanaweza kufanana kati ya kabila moja na jingine! Hapa ndo utakuta lugha, mavazi, chakula, nyimbo, imani nk!

Asili ya nchi mara nyingi huwa na mambo machache kama lugha,(ambapo Tanzania kama taifa asili ya lugha yetu ni kiswahili), mavazi nk!

Asili ya rangi inaeleweka sina haja ya kueleza sana! Sasa wewe unapong'aka kuwa wengi wetu wamemezwa sijui unataka uambiweje uelewe? Kuhusu watu wanaoishi mjini nimeshafafanua sana kwa nini kiswahili kinachukua nafasi kubwa, sina haja ya kurudia! Lakini bado wazazi wanaporudi kwenye majumbani hujitahidi kuwafundisha watoto lugha za asili!

Kwa wale wazazi ambao wameoana wakiwa ni kutoka kabila mbili tofauti ambazo hazielewani, watoto wao hujikuta wanatakiwa kuelewa lugha zote mbili, ya baba na mama ili wakienda kusalim wazee kijijini isiwe shida kuwasiliana! Mfano kama baba Mpare na mama mhehe basi baba atajitahidi watoto waelewe kipare huku mama akijitahidi waelewe kihehe! Kiswahili hicho ni automatic! Kama wazazi wote ni kabila moja kazi huwa ndogo zaidi! Hivyo ndivyo tz ilivyo!

Kwa mantiki hiyo hiyo hoja uliyopandikizwa kichwani kuwa lugha za asili zinachukiwa ni uongo mliouanzisha hapo Kenya ili muendelee kujionuesha kuwa mko juu baada ya kuona speed yetu inawatia tumbo joto! Hivi bila hata aibu unaweza kusema mbele za watu kuwa tunachukia lugha zetu? Mambo mengine uwe unafikiria kwanza kabla hujasema!

Pia umesema eti kuna miji mingine unakuta wapo watu wengi wa kabila moja lakini hawaongei kilugha! Labda nikuulize kuwa ni mji gani huo? Utaje, maana mpaka ukasema umeshauona, hebu useme tukupe majibu hapa!

Suala la kuwa tunaona wanaoongea kiingereza kuwa ni watumwa!

Sio kweli kuwa huwa tunasema kuwa wanaoongea kiingereza ni watumwa, La hasha! Maana hata sisi tunakiongea!

Ambacho huwa tunasema ni kuwa wanaoona kuwa kiingereza ndo kila kitu kuliko lugha zote, na kujivunia kiingereza hicho huku sio asili yao hao ndo watumwa! Na hili linawahusu ninyi wakenya, huwa mnajisifia sana lugha hiyo na kuipa kipaumbele kuliko vitu vyote, huo ndo utumwa tunaousema! Na kwa hili hamtaukwepa utumwa hadi hapo akili zenu zitakapobadilika na kuona kiingereza na kijaluo ni lugha sawa, tofauti ni matumizi tu!

Ziko nchi nyingi sana Africa ambazo zinaongea kiingereza lakini hawajivuni kama ninyi hapo Kenya! Angalia SA, wao wanajivunia Kizulu au Hoxha kuliko kiingereza, lakini wanaongea kiingereza ili kuwaunganisha! Uganda wanaongea kiingereza bora kabisa hapa Africa kuliko nchi yoyote, lakini hawajivuni kama ninyi! Wao wanajivunia kiganda zaidi na lugha nyingine! Kiingereza huwaunganisha tu! Angalia hata Nigeria, Igbo, Hausa na Yoruba zinathaminiwa kuliko kiingereza, na hawajivunii kiingereza kama ninyi mfanyavyo hapo utumwani Kenya!

Huo uzi ngoja nikufuate huko maana unataka kufanya mawazo ya mtu mmoja yawe mawazo ya taifa lenye watu 50+m

Hamna sehemu nilitaja kwamba nimehama mada, nilitumia neno 'point', na tangia hapo mwanzo hamna sehemu nilikana kwamba makabila yenu ya ndani hayana nyimbo za kitamaduni. Kauli yangu ni kwamba, kabila na jamii zote dunia hii zina mambo na tamaduni zao za asili. Lakini nyie mlichokifanya ni kutelekeza na kuona wanaozidumisha kuwa washamba na eti wanaotumia kingereza mnawaona watumwa. Mumekomaa kwenye kulazimisha kila mtu atumie Kiswahili muda wote.

Asili ya mtu huanza na lugha, pale anapozaliwa na kukuta watu wa kwao wanaongea lugha fulani, halafu wakati anakua, anaanza kujifunza tabia, mila na desturi za kwao. Akifikia umri wa kutengamana na watu wa nje ndio anakumbana na desturi za wengine, hatimaye anajitambua kwamba yupo ndani ya taifa lenye watu wa aina tofauti na mila zao tofauti lakini wameletwa pamoja kwa kutumia utaifa.

Hivyo anakumbatia huo utaifa, ila siku zote anafaa akumbuke ana asili ya alikotoka kwa babu zake, kabila lake, lugha yake ya asili, vyote hivyo lazima aviheshimu na kuvitunza. Kadiri anavyosafiri anapata kutambua mambo mengine mengi nje ya taifa lake, anaanza kujua kwamba kijiji chake, kipo ndani ya wilaya ambayo ipo ndani ya mkoa ambao upo ndani ya nchi ambayo ipo ndani ya bara ambalo lipo ndani ya dunia ambayo ipo ndani ya sayari n.k. Hawezi akaishia kwenye kutambua moja na kujifungia humo, lazima awe na uelewa wa jinsi anavyohusiana na maumbile ya sayari hii.

Sisi Kenya tunajivunia asili zetu, tatizo mlishakaririshwa na Nyerere kwamba mtu kujivunia asili yake ni ukabila. Nimesema mara sio haba humu kwamba ubaguzi ni tabia za mtu binafsi na hausababishwi na kabila. Nimewapa mfano wa Somalia ambapo wanaongea lugha moja na dini moja lakini ubaguzi kwa kwenda mbele. Hata kwenu hapo nmewahi kuona ubaguzi wa kidini wa kikanda n.k. pamoja na kwamba huwa mnajinadi watu wasiokua na ubaguzi wowote.
Leo hii nenda pale Zanzibar, wakiwa kwenye mfungo halafu uthubutu kuonekana ukila chochote, juzi kuna jamaa yangu hapo aliniambia mapolisi waliingia sehemu ya chakula na kutwaa vyote, waliwakuta watu wanakula mchana, wakiwemo waliotokea Tanzania bara wasiokua waislamu, na watalii wachache eneo linaitwa CCM, walivuruga amani na kutwa chakula chote. Huo ni ubaguzi maana unamlazimisha mtu aendane na imani yako.
Jana humu JF tuliona Dar es Salaam wafuasi wa kanisa katoliki wamezuiwa kwamba wasiingie kwenye desturi yao ya kuandamana kuadhimisha Eukaristi, kisa mwezi wa mfungo na watakinzana na wenzao.

Kenya tuna matatizo ya kikabila, ila utapata tunabaguana pale likija suala la kisiasa katika upigaji kura, lakini sio kwenye maisha ya kawaida. Mkikuyu na Mjaluo wanauziana kwenye maduka na kuishi pamoja bila matatizo, tunatumia lugha ya taifa Kiswahili, na lugha ya biashara Kingereza, lakini nikiwa na Mkikuyu mwenzangu haja gani niongee Kiswahili wakati tuna lugha yetu ya asili. Kiswahili ni pale kuna mtu hatuendani naye kwenye mazungumzo. Siasa za wanasiasa ndio huwa zinatuharibia, ila tunajivunia tamaduni na desturi zetu, umoja wetu.
Wakenya tunaongea lugha nyingi sana na wanasayansi wamebaini uwezo wa kuongea lugha nyingi unaboresha mtu hata kimawazo, hivyo tunahamasisha watoto wetu waweze kuongea lugha nyingi tu, mfano hai upo kwenye wanangu mimi, binafsi mimi Mkikuyu lakini mke wangu Mluhya, nimejitahidi kuhakikisha watoto wangu wanaongea lugha zetu mbili za asili, wanajua babu zao, desturi na asili ya kwetu. Wakiwa mjini wanaongea Kiswahili na Kingereza, japo pia wanafunzwa Kifaransa shuleni, na mara moja moja naongea nao kilugha na kuwafundisha nyimbo zetu za asili kwa lugha zetu.

Mimi hapa bnafsi nimejifunza lugha nyingi sana zikiwemo kadhaa za kwenu. Halafu hamna cha utumwa kwa mtu kujivunia uwezo wa kuongea Kingereza, hiyo ni lugha ya dunia na imeunganisha mataifa mengi sana na inatumika sana kitaalam, hivyo kujifunza hadi unaweza kuiogea, ni jambo la kujivunia na siwezi kujutia hata siku moja. Kingereza kimenisaidia sana kwenye taaluma yangu pale ambapo Kiswahili kilishindwa pakubwa, hivyo nina sababu nyingi za kukipenda na kujivunia pale ninakitumia bila matatizo.
Ttatizo lenu mna dhana ya sizitaki mbichi.....
 
Kwa hiyo kujua kiswahili kuliko kikabila tumekuwa watumwa, ha haa, Jamaa baada ya kukubaliana na utumwa wenu mmetafuta pa kutuita watumwa ili mfanane, ukaona uje na kiswahili, mkuu unapaswa ujue kiswahili kina asilimia kubwa ya misamiati ya lugha za kikabila za hili eneo la Tanganyika na Zanzibar. Kiarabu kireno na kiingereza vina mchango sumni sana. Najua umeshangaa neno sumni, sumni na kidogo vyote vina maana moja tu, kuna ya kibantu na arabu hapo. So it was agreed that all these tribes in order to unite, tuunge nguvu kwenye kiswahili ambacho kilikuwa kimesambaa zaidi. Hakuna utumwa hapo mkuu, sababu hata kikikuyu kina lugha ambazo zilikuwepo kabla ya current Kikuyu language, likewise kuna ancient Chinese and current one. So muingiliano wa watu huwezi kuucontrol buda, na muingiliano wa watu hukuza na kudiversify lugha, hence lugha hazitabaki the same, ww mwenyewe umejifunza zaidi kiswahili humu jamvini, na sasa unabonga zaidi na wanao kiswahili, na wanao wanajikuta wana baba mzungumzaji mzuri wa Swahili na wao wamezungukwa na jamii inabonga Swahili muda mwingi wakiwa home, skuli ndio kiingereza kwa sana, likizo kwa bibi na babu Kikuyu, ww kwa akili yako mwanao atakuwa bora kwenye lugha gani? Muda mwingi atatumia wapi na akiwa na watu wanasema lugha gani. Let's be analytical and burry this topic for good.

Sasa hapo kama una akili sawasawa utaona muda mwingi atakuwa around Swahili language, hence Swahili growth ma niga, ww unadhani ni kwann Swahili ni second most spoken language in Africa, ni tokana na social political factors which you as an individual ma Frnd can't stop it. Ndio maana unaona serikali ya Tz inataka kuiweka kwenye mtaala wa elimu, sababu no way out English speakers will surpass Swahili ones.
Kwa iyo hata Swahili kuingizwa kwenye mtaala wenyu wa elimu, hauepukiki, eti mnajaribu kupunguza kuenea kwa kuleta sheng, itabaki kuwa kama lugha ya kikabila cha watu wa Nairobee ambacho kitamezwa na Swahili.
Sababu inaongelewa Congo mshariki, Burundi, Rwanda, Ug, SA wameomba walimu, Zambia kaskazini, Msumbiji kaskazini, visiwa vyote bahari ya Hindi, Bongo enyewe kubwa kushinda Naija, imagine tukija kuwa MTU nyomi kama Naija, wote waswahili.

Swahili will become the first most spoken language, nations are making decisions, Zimbabwe, Ethiopia etc are cracking their minds on how to teach their people Swahili so that they are not left behind in the near future. Wewe baki hapo na utumwa wakati mtumwa anakuja kuwa mfalme like Joseph.

Wewe umetiririka insha, ila sijui nikujibu nini maana unazunguka zunguka bila kueleweka pa kutokea. Fahamu kwamba Kenya tunajivunia Kiswahili maana pia ni ukweli kwamba kilibuniwa kwenye Pwani zetu. Tumehusika katika kukipigia debe kwa majirani zetu Wahabeshi, Somalia, Sudan zote mbili na hata Uganda na DRC na Afrika na duniani kote.

Hivyo hayo yote unavyobwabwaja sijui tatizo nini, kwa kifupi ni kwamba sisi hatujaghubikwa kwenye lugha moja, tuna uwezo wa kuongea lugha nyingi na ndio desturi yetu. Tumedumisha asili yetu na tamaduni zetu na tunazipokeza kwa watoto wetu, hatupo radhi kuishi maisha ya kizombi ya kujua lugha moja tu basi, na hata lugha yenyewe unakuta wachache ndio wanaifahamu na kuitumia ipasavyo.
 
MK254

Nikukumbushe tena wakenya ndo mnaongoza kuacha mila zenu, sio lugha tu hadi mavazi! Hebu jikumbushe wenzio waliokuwa wanaandamana kudai mavazi ya kimagharibi halafu useme hapa nani kaacha asili kati yetu na nyie!!

Eti my dress, my choice

Hii ndio nini, kwani watu kudai haki ya kuvaa watakavyo tatizo liko wapi, wewe hapo hiyo suruali uliyovaa hivi una taarifa mababu zetu Afrika hawakuvaa suruali??
 
Wewe umetiririka insha, ila sijui nikujibu nini maana unazunguka zunguka bila kueleweka pa kutokea. Fahamu kwamba Kenya tunajivunia Kiswahili maana pia ni ukweli kwamba kilibuniwa kwenye Pwani zetu. Tumehusika katika kukipigia debe kwa majirani zetu Wahabeshi, Somalia, Sudan zote mbili na hata Uganda na DRC na Afrika na duniani kote.

Hivyo hayo yote unavyobwabwaja sijui tatizo nini, kwa kifupi ni kwamba sisi hatujaghubikwa kwenye lugha moja, tuna uwezo wa kuongea lugha nyingi na ndio desturi yetu. Tumedumisha asili yetu na tamaduni zetu na tunazipokeza kwa watoto wetu, hatupo radhi kuishi maisha ya kizombi ya kujua lugha moja tu basi, na hata lugha yenyewe unakuta wachache ndio wanaifahamu na kuitumia ipasavyo.
Sijabwabwaja Mzee, nimekupa somo kubwa sana hapo, kufupisha na kuhitimisha ni kwamba hata mkomae na vilugha vyenu, kisheng kiingereza, hamtoweza kukizuia kiswahili kukuwa na kutawala ukanda wetu hadi Africa nzima.
Utaita ni utumwa or whatever, but you will not avoid Swahili.
And Swahili haikuzaliwa pwani yenu, mnapenda sana kujimilikisha, Swahili imezaliwa pwani ya Africa mashariki.
 
Kwani Pwani yetu sio ya Afrika Mashariki, nenda kapate tena somo la jiografia, pili naomba ufahamu kwamba hamna siku tumethubutu kuzuia Kiswahili, tumegoma kuruhusu kutekwa nacho na kuwa kama mazombi.
Lugha zetu za asili ndio lugha za kwanza, maana zinatuunganisha na mababu zetu, zinatupea asili na utambulisho wa kule tunakotokea, lugha zingine za kukuja tunazipokea na kuzikuza lakini haitowahitokea kwetu sisi tutelekeze lugha za asili.

Kiswahili kimebuniwa kwenye Pwani zetu na kilitukuta tukiwa na lugha zetu, mila zetu, asili yetu. Babu zetu walikua na tamaduni zao kabla Mwarabu hajaja na kuvuruga kwa ushirikiano wa mzungu. Leo hii Mnyamwezi au Mhehe unavaa milegezo hapo Dar na kukana asili yako eti wewe Mswahili, mfanye nyie lakini sisi tutaendelea kudumisha na kuzitunza lugha zetu.

Wakenya tumehusika pakubwa katika kufanikisha usambazaji wa Kiswahili, hivyo hamna sehemu tumekiponda au kukizuia, kinazagaa kwajili ya juhudi zetu. Lakini hakitatumeza tuishi kama mazombi yasiokua na asili.
 
Hii ndio nini, kwani watu kudai haki ya kuvaa watakavyo tatizo liko wapi, wewe hapo hiyo suruali uliyovaa hivi una taarifa mababu zetu Afrika hawakuvaa suruali??
enheeee nilijua tu utasema hilo! Na hapo ndo pengine bado hujaelewa! Yawezekana kweli suruali hizi mababu hawakuanza nazo hapo awali! Lakini hebu jiulize, ilikuwaje sisi tukazivaa!

Najua utasema zililetwa na wazungu, tuseme ndio, lakini ukweli ni kuwa jamii ndo ilizihitaji kwanza halafu ndio zikavaliwa! Wala wazungu hawakutulazimisha kuzivaa, na tena enzi za utumwa bado walitaka babu zetu waendelee kujifunga ngozi!

Ilifikia sehemu utamaduni wenyewe ukahitaji kuwa na vazi hilo, na jamii ikalitumia bila shida yoyote!

Wanachokidai hao ndugu zako ni kitu ambacho jamii haikihitaji! Kwa kisingizio cha utandawazi Halafu na wewe huoni shida katika hilo huku ukiendelea kujisifu kuwa unadumisha tamaduni zako!

Sasa utadumishaje tamaduni ambazo jamii haizihitaji?
 
Watanzania wengi wanazungumza Kiswahili kuliko makabila yao.

Sababu tumeshazitoa nyingi sana, Sisi hatutaki kwenye mkusanyiko wa watu uzungumze kitu ambacho wengine hawaelewi, hapo ni kama mnawateta wenzenu au basi mazungumzo yenu yanakuwa kelele kwa wenzenu!

Ndo maana kwenye mkusanyiko ambao hatuna uhakika kuwa watu wote waliopo pale ni wa kabila moja, ni vyema kutumia kiswahili ambacho watu wote wanaelewa!
 
Kwani Pwani yetu sio ya Afrika Mashariki, nenda kapate tena somo la jiografia, pili naomba ufahamu kwamba hamna siku tumethubutu kuzuia Kiswahili, tumegoma kuruhusu kutekwa nacho na kuwa kama mazombi.
Lugha zetu za asili ndio lugha za kwanza, maana zinatuunganisha na mababu zetu, zinatupea asili na utambulisho wa kule tunakotokea, lugha zingine za kukuja tunazipokea na kuzikuza lakini haitowahitokea kwetu sisi tutelekeze lugha za asili.

Kiswahili kimebuniwa kwenye Pwani zetu na kilitukuta tukiwa na lugha zetu, mila zetu, asili yetu. Babu zetu walikua na tamaduni zao kabla Mwarabu hajaja na kuvuruga kwa ushirikiano wa mzungu. Leo hii Mnyamwezi au Mhehe unavaa milegezo hapo Dar na kukana asili yako eti wewe Mswahili, mfanye nyie lakini sisi tutaendelea kudumisha na kuzitunza lugha zetu.

Wakenya tumehusika pakubwa katika kufanikisha usambazaji wa Kiswahili, hivyo hamna sehemu tumekiponda au kukizuia, kinazagaa kwajili ya juhudi zetu. Lakini hakitatumeza tuishi kama mazombi yasiokua na asili.
Ati lugha ya kwanza inawaunganisha na mababu zenu, ha haa, mababu wanakufa wameshakufa, wa kazi gani, au mnatambika, lazima wa Kikuyu mtakuwa mnatambika.
Sikiliza buda,hata Yesu alisema, wacha wafu wazike wafu wenzao, akasema tena, cha kwanza kitakuwa cha mwisho.
So I can say that you conservatives are holding on to that which is about to die by being engulfed with Swahili.
Hold on while it last
 
enheeee nilijua tu utasema hilo! Na hapo ndo pengine bado hujaelewa! Yawezekana kweli suruali hizi mababu hawakuanza nazo hapo awali! Lakini hebu jiulize, ilikuwaje sisi tukazivaa!

Najua utasema zililetwa na wazungu, tuseme ndio, lakini ukweli ni kuwa jamii ndo ilizihitaji kwanza halafu ndio zikavaliwa! Wala wazungu hawakutulazimisha kuzivaa, na tena enzi za utumwa bado walitaka babu zetu waendelee kujifunga ngozi!

Ilifikia sehemu utamaduni wenyewe ukahitaji kuwa na vazi hilo, na jamii ikalitumia bila shida yoyote!

Wanachokidai hao ndugu zako ni kitu ambacho jamii haikihitaji! Kwa kisingizio cha utandawazi Halafu na wewe huoni shida katika hilo huku ukiendelea kujisifu kuwa unadumisha tamaduni zako!

Sasa utadumishaje tamaduni ambazo jamii haizihitaji?

Watu tunadumisha tamaduni zetu na asili zetu ila kwa hiari sio kwa shuruti, hao akina dada wanataka haki ya kuvaa watakavyo maana miili ni yao na haituhusu. Hivi unajua tamaduni haslisi za Kiafrika wanawake walivaa vipi, bora hata hizo mini-skirts.
Hadi leo kuna jamii ambazo hayo mambo ni ya kawaida, agalia hii picha

tumblr_mkddxiS6eh1s92937o1_1280.jpg
 
Ndo muache sasa kujisifu maana hao wasichana walikuwa wanadai zinazoitwa haki zao huko kenya! Utamaduni wenu umebakwa huko!

BTW hiyo picha ya SA naona imekukaa
 
Back
Top Bottom