Synod
JF-Expert Member
- Oct 10, 2016
- 4,091
- 4,028
Ahaaaa! Naona point ya kwanza umeihama baada ya kuona haina uhalisia!Nyimbo wanazo sijabisha hilo, maana kila kabila dunia hii lina nyimbo zake za asili kama ilivyo kwamba wana lugha zao za asili, lakini ninachosema ni kwamba walishazitelekeza. Kupata nyimbo za asili sio issue, mbona kazi ya dakika chache tu, lakini cha msingi ni kwamba unakuta watu wa pale wengi hata hawana shughuli nazo na hawaziimbi wala kuongea lugha zao.
Hapa naweza nikakupa nyimbo za kizaramo, lakini kuwakuta wazaramo kitaa wakiziimba au wakiongea ongea lugha yao ya asili ni vigumu, wengi hawajui hata salamu na ndio taswira maeneo mengi Tanzania, watu wanaishi kama watumwa, hawajui asili yao na hawafundishi watoto wao mila na desturi zao. Mtoto anakua kama wale Wamarekani weusi wasiokua na asili wala kujua walitokea wapi. Wao hujua kwao ni Afrika, lakini hawajui chochote zaidi ya hapo na hutukanwa sana.
Kwanza fahamu kuwa ili lugha ya asili iongelewe vizuri ni lazima watu kadhaa wa lugha hiyo wakutane, au basi iwe nyumbani!
Miji mingi ya Tanzania ia mchanganyiko wa makabila, hakuna mji uko na kabila moja, mawili au matatu pekee. Sasa weww kama unapita tu mtaa huo utawaskia wapi wanaongea kilugha wakati wapo watu wa makabila mengi? Lakini hii haiondoi uhalisia kuwa hawajui maana hizo lugha ndo zimewakuza!
Twende na hili la kutokujua lugha za asili au kuziongea! Umetumia mfano wa wazalamo! Nami nikujibu kwa mfano huo huo!
Kwanza nikufahamishe kuwa moja ya watu ambao eneo lao la asili limeingiliwa na watu wengi kutokana na ukuaji wa mji ni wazaramo! Dar imekuwa kubwa kiasi kwamba makabila yote 126+ ya tanzania yanapatikana dar, ambako ndiko kwa wazaramo! sasa kwa mchanganyiko huo wa makabila yote hayo, unategemea wazaramo ambalo pia kwa asili ni kabila dogo, wakutane saa ngapi hapo dar ili uwaskie wanaongea kizaramo? Ndio maana kikawepo kiswahili kurahisisha mambo!
Lakini pia hao hao wazaramo ambao tunawatumia kama mfano wakirudi kwenye miji yao basi huongea! Pia, kwa wale wazaramo wanaoishi pembezoni kidogo hasa mkoani pwani ambako wanaishi kama jamii moja wanaongea sana na ndo lugha yao ya kwanza!
Makabila mengine yanaongea sana lugha hizi na ndio lugha zao za kwanza, kiswahili cha pili na kiingereza cha tatu!
Sisi sio kama huko kwenu, hapo nairobi unakuta wakikuyu wamejaa kila sehemu, kuna mitaa imejaa wakikuyu tupu hata mjaluo hagusi, na mitaa wamejaa wajaluo tupu,