Je, Watanzania hatuaminiani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Watanzania hatuaminiani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtanzania, Oct 11, 2008.

 1. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wanasiasa Tanzania hawaaminiki (From Majira)

  *Wamo polisi, wafanyabiashara, mabosi NGOs
  *Imani zaidi ni kwa ndugu, kabila, wanadini
  *D'Salaam yaongoza kwa watu wasioaminiana

  Na Joseph Lugendo

   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nini hasa tatizo la kukoseana uaminifu hapo?Ndio swali la kwanza la kujiuliza!Fedha imefanywa kuwa kila kitu na umaskini wa kupindukia.
  Vilevile Ukabila,Ubinafsi na Uchoyo.
   
 3. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni habari muhimu kwa jamii yetu.Inahitaji tafukuri.
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Njaa ndio mama wa matatizo yote hayo ya kutoaminiana, ukabila, udini, udugu nk.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni habari muhimu lakini jinsi ilivyoandikwa inanifanya nisielewe baadhi ya mambo. Wanasiasa wanashika nafasi ya 11 kwa kutoaminika na viongozi wa NGO nafasi ya 12. nani anashika nafasi ya kwanza, ya pili, ya tatu n.k?
  basisi ya utafiti huu wote ni nini? Mkukuta si inahusika na masuala ya umasikini, nini kiliwaplekea kufanya utafiti wa aina hii? Si kwamba nakosoa utafiti wenyewe, naangalia tu relevance ya Mkukuta kufanya research hiyo
   
 6. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  MN,

  Kama utasoma vizuri inaonyesha kuaminika kunaanzia chini, namba moja ni familia.

  MKUKUTA wanaweza kuhusika maana miradi ya TZ kwa asilimia kubwa chanzo cha mtaji sio banks, ni familia, marafiki nk. Kuaminiana na umaskini vina uhusiano.

  Yaani NGO inaaminiwa kidogo kuliko wanasiasa? Hii ni hatari kabisa.

  Binafsi naona utafiti huu ni muhimu sana na unaonyesha jinsi jamii zetu zilivyoporomoka. Hata viongozi wa dini hawaaminiki sana.
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na mpango wenyewe wa mkukuta unaaminika kiasi gani miongoni mwa wananchi?
   
 8. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ni ulaji kama NGOs tu.
   
 9. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mtanzania,

  Nashukuru kwa kuileta hii habari hapa. Pamoja na kuwa natamani sana niulize hivi MKUKUTA wanweza kutuambia wako umbali gani kukamilisha safari ya madhumuni ya kuanzishwa, inabidi niongelee kuhusu kura hizi za maoni.

  Naliangalia kwa macho ya kisiasa na kuhoji ikiwa Wanasiasa hawaaminiki, inakuwaje tunaendelea kuwa na viongozi na wanasiasa wale wale kila baada ya miaka mitano?

  Pili inaelekea wenyeviti wa kata na vijiji wanaaminika sana, je wenzetu wa Upinzani wameliona hili na kulichukulia kwa umakini kwa nini CCM inawapiga ngwala kila uchaguzi?
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,805
  Likes Received: 83,182
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikiri wanasiasa wanastahili kushika nafasi ya kwanza kwa kutoaminika akina fisadi Mkapa, Kikwete, Rostam, Chenge, Karamagi, Mkono, Mzindakaya, Mramba, Lowassa, Makamba na wenzao kutokana na scandals za IPTL, Mkapa kufanya biashara akiwa Ikulu, Kukupua Kiwira kutoka kwa Watanzania, kuhusika na ufisadi wa Rada, ufisadi wa uuzaji nyumba za serikali, kusaini mikataba mibovu ya uchimbaji wa madini ambayo haina maslahi kwa Tanzania, ununuaji wa magari na helicopters za jeshi, kukabidhi ripoti ya madini kwa Sinclair kabla ya Watanzania hawajaiona, kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria mafisadi wa EPA, Richmond, Meremeta, ujenzi wa Twin Towers, kujipatia mabilioni ya shilingi toka BoT kwa kazi ambazo wameshindwa kuzithibitisha n.k. nadhani wanaofuata wanastahili kuwa polisi halafu mahakama.
   
 11. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ingelikuwa huku West, NGO ingechukua nafasi ya juu. Kwa TZ ziko hata chini ya wanasiasa. Hawa ndio walitakiwa kusaidia jamii hasa za wanyonge.

  Hii ni dalili ya mafisadi kuingia kwenye sectors zote muhimu za kushughulikia jamii.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Oct 11, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  When a country loose leadership... this is what U get!

  Ukitazama kwa makini hoja nzima ya MKUKUTA inalenga kutazama leadership kwani kuamini mtu kunatanguliwa nafasi ya mtu huyo ktk jamii nzima..na tatizo kubwa linalojenga uongozi mbaya hutanguliwa na Mawasiliano kati ya mtu huyo na walengwa.
  Hivyo utaona kwamba watu waliochukua nafasi za juu ni wale wenye mawasiliano ya karibu kila siku na wananchi kuliko wale walioko mbali..
  Tujiulize ni Wabunge wangapi wanaishi ktk wilaya walizogombea?...
   
 13. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2008
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Sawa sawa Mkandara

  Natamani kusema kuwa JK anatakiwa achukulie huu uchunguzi serious, but then......oh well!

  My point ni kwamba, kwenye uongozi ambao huko makini kwenye kudeliver, report kama hii ndio hasa unapotakiwa kuitumia kujenga msingi imara wa jamii yake.

  Kama kiongozi imara, unaweza kutumia report hii kushughulikia matatizo ya kijamii. Unajua kuwa jamii haina imani na polisi, then you got business to take care in the police department......and so on.

  But then Watanzania tumeula wachuya. Tutazidi tu kuvuna magugu, kwani ndiyo hayo hasa tuliyoyapanda 2005. So until msimu wa kulima utakapoanza tena (hopefully tutapanda mazao msimu mpya), hatuna budi kuendelea kuumia matumbo kwa kula magugu.

  Hiyo report inazidi kuongeza maumivu kwenye kidonda
   
 14. m

  maggid Verified User

  #14
  Jul 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Na Maggid Mjengwa,
  NAANDIKA haya nikiwa nchini Hispania. Nilipata bahati pia ya kutembelea nchi ya Poland yapata wiki moja iliyopita. Hizi ni nchi mbili ambazo zinafanana katika mambo mawili makubwa; zote mbili zina historia ya kuongozwa kidikteta kabla ya kufikia hatua hii ya kuwa nchi za kisasa na kidemokrasia.

  Hispania ilikuwa na utawala wa kidikteta (Dikteta Franco) hadi alipofariki mwaka 1975, ndipo mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa yakapamba moto. Poland ilikuwa na udikteta wa chama kimoja ( Ukomunisti) hadi ukuta wa Berlin ulipoangushwa na mageuzi ya kisiasa , kiuchumi na kijamii yalipopamba moto. Na nchi zote hizi mbili ni za Kikatoliki na zina idadi ya watu inayolingana. Zote zina wakazi milioni 40.


  Mifumo kandamizi ambayo nchi hizi ilipitia ndiyo iliyosababisha zikawa kwenye matatizo makubwa. Na kubwa zaidi, imani ilikosekana.


  Na hakika, tatizo letu kubwa Watanzania kwa sasa ni kukosekana kwa imani miongoni mwetu. Hatuaminiani. Na mfumo uliotufikisha hapa bado hatujaubadili kwa kiwango cha kuridhisha.

  Hili ni tatizo la nchi nyingi barani Afrika. Ndiyo, mathalan, Serikali nyingi Afrika hazipendi kuwepo kwa Tume Huru za Uchaguzi kwa vile hutoa nafasi kwa walio kwenye upinzani kuingia madarakani.

  Na kwa vile hawana imani nao, kwa maana ya wapinzani, mara na wao watakapoingia madarakani, Serikali hizo huona ni vyema kutokuwepo kwa Tume Huru za Uchaguzi. Hilo la mwisho linawabakishia matumaini ya kuendelea kubaki madarakani. Maana, anayeamua hatima ya uchaguzi si mpiga kura, bali mhesabu kura na mtangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi.


  Mfano, katika katiba yetu ijayo, kama itapendekezwa kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi , basi, huo utakuwa ni mwanzo wa mapinduzi makubwa ya kuifanya nchi yetu kuwa ya kisasa zaidi.

  Nahofia Tume Huru ya Uchaguzi itasubiri mpaka tuchinjane kwanza kwa kutuhumiana kuibiana kura kwenye chaguzi. Tatizo ambalo lingeweza kumalizwa kwa kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi itakayoaminika na pande zote zinazoshiriki chaguzi. Itakayoaminika na wananchi.

  Kuna wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki- Moon alitamka; kuwa tatizo kubwa la Serikali nyingi si nakisi ya bajeti bali nakisi ya imani ya Wananchi kwa Serikali hizo. Ndiyo, kupungua kwa imani. Ndiyo, inahusu imani na ni wajibu wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi kuirudisha imani ya wananchi kwa Serikali na chama hicho.


  Niliwahi kuandika kuwa nchi yetu iko njiapanda. Mbele yetu kuna njia mbili; moja inaelekea tunakopita sasa. Kwenye hali ya ‘kujifunga’ na kubaki tulipo bila kupiga hatua za haraka za maendeleo huku baadhi (wakiwamo viongozi), wakiwa na udhibiti mkubwa wa hali ya mambo.


  Njia nyingine inaelekea kwenye uhuru zaidi wa wananchi na uwezo wa kuwadhibiti na kuwawajibisha viongozi wao. Ni njia inayoelekea kwenye ustawi wa nchi.

  Watanzania wengi kwa sasa wana kiu kali ya kuianza safari ya kuipita njia ya pili. Njia yenye uhuru zaidi na matumaini ya ustawi wa taifa. Njia itakayotufanya tuondokane kabisa na njia ya kwanza, njia inayotufunga na kutubakisha hapa tulipo.

  Na siku zote, nchi haiwezi kupiga hatua za maendeleo ya kiuchumi bila kuwa na utulivu wa kisiasa. Kuna dalili, huko twendako, hakutakuwa na utulivu wa kisiasa kama tutaicha hali hii ya sasa iendelee kama ilivyo. Hali ya kutoaminiana na kukosekana kwa mwafaka wa kitaifa wa kisiasa.

  Na Profesa wa Uchumi, Jeffrey Sachs ana mfano hai wa Poland. Katika kuwashauri kuinuka kiuchumi Wapolandi,

  Profesa Sachs aliwaambia; “Political power must be shared”. Kwa tafsiri yangu ni kwamba; kuna umuhimu wa vyama kuwa na utayari wa kugawana madaraka ya uongozi wa kisiasa.

  
Ndiyo, Fundi Umeme yule Lech Walensa wa chama cha wafanyakazi na aliyeanzisha vuguvugu la mapinduzi ya kujikomboa kutoka Ukomunisti aliambiwa hivi na Profesa Jeffrey Sachs; “ Chama chako cha Solidarity kiwe radhi kuunda Serikali ya Mseto na Chama Cha Kikomunisti”.


  Baada ya uchaguzi ikawa hivyo, kimoja kikatoa Waziri Mkuu na kingine Rais. Kukawepo utulivu wa kisiasa. Poland ikaanza kupiga hatua za maendeleo ya kiuchumi. Ndiyo, hakuna uchumi unaokua bila uwepo wa utulivu wa kisiasa. Katiba Mpya itakayohakikisha, mbali ya mambo ya mengine inatupa Tume Huru Ya Uchaguzi. Nahitimisha.


  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
  +46 736 966032
   
 15. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uko sahihi kabisa.Tukiacha ubinafsi na tukaamua kwa dhati kuaminiana katika ujenzi wa Taifa hili tutashuhudia maendeleo makubwa na ya haraka. kuna mambo yanatukwamisha kama jamii kusonga mbele. mambo yanayo tukwamisha ni; UBINAFSI, MATUMIZI MABAYA YA RASILIMALI ZETU,USIMAMIZI MBOVU WA FEDHA ZA UMMA,POOR INVESTMENT KATIKA ELIMU NA KUTOKUJUA PRIORITY.Utajiri tulionao watanzania ungekuwa ni wa kenya wangekuwa kama ulaya.
   
 16. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
 17. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #17
  Jul 11, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Maandiishi mengi,,,lakini ilo la kutoaminiana hapa kwetu lipo na linafanywa na chama cha mabwepande CCM, imani yetu ipo juu ya CHADEMA aka nguvu ya umma na ndipo maana kikaasisi kuundwa kwa katiba mpya magamba wanachofanya nikuujumu mchakato tu,

  Wasalimu huko ughaibuni usirudi bongo kuna kitu kinaitwa MABWEPANDE chini ya ACP Msangi na Zoka wananyofoa kucha na meno balaa, usirudi mkuu.
   
 18. abudist

  abudist JF-Expert Member

  #18
  Dec 6, 2016
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 620
  Likes Received: 465
  Trophy Points: 80
  Tanzania na Morroko zimetajwa ndiyo nchi zisizokuwa aminifu zaidi duniani kati ya nchi 159 zilizofanyiwa utafiti. Utafiti huo umefanywa na jarida la week la Nature ambao umegusa maeneo ya Rushwa, Udanganyifu wa Kodi, Siasa, Kivuli cha Uchumi, Kipato cha mwananchi, Haki za kisiasa, Ufanisi wa serikali, Kuwalazimisha Watendaji nk.. Kenya pia imo katika orodha hiyo nchi zisizo aminifu. Nchi zilizotajwa kuwa aminifu zaidi kuliko zote duniani ni Uingereza, Uholanzi na Austria.

  Tafsiri:

  A study conducted by Nature, an international weekly journal of science, has named Tanzania and Morocco as the most dishonest countries in the world. The most honest countries, according to the study, were the United Kingdom, Austria and the Netherlands, while other dishonest countries included Kenya, Indonesia and Guatemala. The report, which examined 159 countries for their varying levels of corruption, political and tax fraud, also studied shadow economies, the prevalence of rule violations, government effectiveness, GDP per capita, political rights, constraint on executives and individualism.

  wabongo.png

  Source: Intrinsic Honesty and the Prevalence of Rule Violations across Societies
   
 19. MpiganiaUhuru

  MpiganiaUhuru JF-Expert Member

  #19
  Dec 6, 2016
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 783
  Likes Received: 763
  Trophy Points: 180
  Iko sawa, viashiria tajwa viko wazi mno!
   
 20. mitale na midimu

  mitale na midimu JF-Expert Member

  #20
  Dec 6, 2016
  Joined: Aug 26, 2015
  Messages: 5,582
  Likes Received: 9,040
  Trophy Points: 280
  ndio maana tunaogopa kuungana na majirani kwenye mambo mengi maana hatuaminiki na hatuaminiani.

  Hizi tafiti ni aibu tena kipindi ambapo hata bunge liko gizani, matumizi ya pesa hayaeleweki, siasa ziko kapuni. Unaweza kuja kugundua ulipigwa mwaka 2017 mwaka 2023.

  Kuna haja kama taifa tukae tujitafakari tulianguka wapi ili tuirudie njia kuu
   
Tags:
Loading...