Je Wassira ni Mzushi au Muongo wa kutupwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Wassira ni Mzushi au Muongo wa kutupwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GIB, Mar 19, 2012.

 1. GIB

  GIB JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Soma kwa makini kisha toa maoni yako.
  KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa jana alitua Arumeru Mashariki na kuhutubia mkutano uliotikisa eneo la Kwapole – Soko la Ndizi, huku wazazi wa mgombea wa chama hicho, Joshua Nassari wakipanda jukwaani kujibu matamshi yaliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira(TYSON) dhidi ya mtoto wao.

  Mchungaji Samuel Nassari na mkewe, waliwaambia mamia ya watu waliofika kwenye uwanja huo kuwa walitoa baraka kwa Joshua kugombea nafasi hiyo wakisema mtoto wao ni mwadilifu anayefaa kuwawakilisha wananchi wa Arumeru Mashariki bungeni.

  Kauli ya Mchungaji Nassari inatokana na matamshi ambayo yamekuwa yakitolewa na Wassira katika kampeni za kumnadi mgombea wa CCM, Sioi Sumari kwamba mgombea wa Chadema hana nidhamu na kwamba amewachosha wazazi wake kwa kutokuwa na nidhamu.

  Lakini jana, baba wa mgombea huyo akiwa na mkewe jukwaani alisema: "Mimi siyo mwanasiasa, lakini nimelazimika kupanda jukwaani leo kutokana na matamshi yaliyotolewa na Wassira, napenda kusema hivi Joshua alipata baraka za familia."

  Alisema kabla ya kugombea, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alifika nyumbani kwake Songoro na kuwaeleza kuwa wanamtaka Nassari kugombea tena na kusema kwamba familia ilikubali na kumpa baraka zote ikiwa ni pamoja na kuwaita wachungaji kumwombea.

  Mchungaji Nassari pia alikanusha madai kwamba mwanaye alikuwa jeuri tangu shule akisema hajawahi kufukuzwa wala kusimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu tangu akiwa shule ya msingi hadi alipohitimu masomo ya shahada, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Mchungaji huyo alisema, mtoto wake alisoma katika shule ya msingi, Sekondari ya Bagamoyo kidato cha kwanza hadi cha nne na Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora kidato cha tano na sita.

  "Alipokuwa chuo kikuu, ninatambua kwamba alikuwa mtetezi wa wenzake, hivyo ndugu zangu Joshua Nassari anafaa kuwa mbunge na suala kuwa hajaoa halina msingi kwani mke bora mtu anapewa na Mungu na siyo utashi wake au hamu yake, kwani mke siyo kitunguu cha kununua sokoni," alisema Mchungaji Nassari

  source : gazeti la mwananchi jumatatu
   
 2. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna mambo mengine ya ajabu, Mtu kama wasira (a.k.a. TYSON), anapewa wizara ya mahusiano ambayo mtu anatakiwa kuwa na diplomasia ya hali ya juu ili kukuza mahusiano, lakini yeye wakati wowote anasababisha mahusiano kuharibika. Mimi binafsi simshangai wasira kutamka maneno hayo na labda niwaulize wana JF je tangu huyu TYSON alipoteuliwa katika nafasi hiyo ameshafanya kitu gani ambacho mnafikiri amekuza mahusiano???
   
 3. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280

  Aliyekosea ni aliyempa wizara hiyo, bora angemuacha kule kule wizara ya chakula.
  Huyu mzee hana busara kabisa, ndio sababu kapewa jina la Tyson. Jiulize kwa nini alikimbia NCCR na kurudi magamba?
   
 4. GIB

  GIB JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mzee naona anazeeka vibaya . Sera zimemuisha imebaki kutukana tu. Ashindwe na alegee , tena ashindwe kupotosha
   
 5. BJEVI

  BJEVI JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 1,360
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  WASIRA is hope less.Unakuza mahusiano kwa kuweka chuki na fitina kwenye jamii!

  Lakini siyo makosa yake ULEVI ni NOMAAAAAAAAAAAAAAAAA................
   
 6. m

  mbwagison Member

  #6
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Tyson alikuwa anasinzia jukwaani, kule kuropoka ni ndoto zile alikuwa usingizini. Halafu sura ya huyu mshikaji ipo poa kinoma,vitani huhitaji kupaka masizi!
   
 7. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa magamba bado hawajapata pointi ya kuwateka watu wa Arumeru kwa hiyo bado wanapapasa gizani kutafuta cha kuwaambia wana Arumeru, maana Igunga walitumia udini sasa huko pamekuwa pagumu zaidi ya kuongea matusi tu.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Asingekuwa mwanasiasa asingepanda Jukwaani, angeongelea kwenye media.
   
 9. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nahisi harufu ya magamba! Yani kijana wako achafuliwe kwenye jukwaa la siasa alafu wewe kukanusha uende kwenye media wakati anatafuta kura na ana baraka zako!¿ Huo ni uvivu wa kufikiri na ndilo tatizo kubwa la utawala wetu.
   
 10. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  wassira tunakuona na ubunge wa fadhila
   
 11. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
   
 12. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,746
  Trophy Points: 280
  Kweli duniani watu wawili wawili huyu hapa na Mheshimiwa Tyson kopi raiti kabisa.
   
 13. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Hata sura yake haina. Mahusiano na binaadamu
   
 14. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wasira bado yupo usingizini jamani naomba mwenye ile picha anayokoroma bungeni. Unategemea ataongea nini? Kachoka hana hata moja kichwani.
   
 15. Micro E coli

  Micro E coli JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mkuu zipange pamoja copy yake na picha yake halisi mkuu.
   
 16. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, huko NCCR alienda kwa kazi maalum alipoikamilisha akarudi kwa aliyemtuma kazi!
   
Loading...