Je, wapinzani mngefikia hata robo ya Rais Magufuli?

Surveillance

Member
Dec 2, 2018
25
22
Rais gani ataufikia uzalendo wa Magufuli?
Nani ana uwezo wa kuwanyoosha majizi kama Magufuli?
Je, kama upinzani ungeshinda 2015 wangefikia hata robo ya JPM kimaendeleo?

Duh Magufuli anatisha katika kusimamia miradi ya maendeleo.

Jambo moja tu linalomwangusha Rais Magufuli ni kuteua watu wasio na uwezo wala uzoefu wa utumishi wa umma na utendaji kuwa wakurugenzi na wakurugenzi watendaji wa halmashauri.

Laiti angewateua wakurugenzi wenye uzoefu, halmashauri zisingeshikika. Lakini kwa sasa tumebugi kwenye wakurugenzi kwenye halmashauri. Serikali inapeleka fedha nyingi lakini miradi ya huduma za jamii haikamiliki. Naamini hili litarekebishwa ili Tanzania isonge mbele kwa kasi.

Kwa ujumla, kwa kasi hii Rais ameweka rekodi ambayo ni kazi kwa marais watakaofuata kuivunja. Hongera Rais mwanasayansi, Rais mtendaji asiye mwanasiasa. Hongera sana.
 
Surveillance

Rais gani ambaye hajali watumishi wa umma?

Kwa miaka mi 4 mfululizo hakuna nyongeza mshahara wala Watumishi kupanda madaraja. Hivi ni vitu vipo kisheria na wala sio HISANI.

Nchi si ipo vizuri kama anavyosema, mbona hapindishi mishahara ya watumishi?

Unababaika na midege hiyo ambayo hata procurement yake Bunge haiifahamu? Ndege ambazo Watanzania hawajui kwanini manunuzi yake hayapo wazi?

Grow up Mbwiga. Acha Ushamba wewe.
 
Mie naamini wangefanya zaidi ya hapa ili waaminike kwa wananchi ili waendelee kutawala
 
Rais gani ambaye hajali watumishi wa umma..??

Kwa miaka mi 4 mfululizo hakuna nyongeza mshahara wala Watumishi kupanda madaraja. Hivi ni vitu vipo kisheria na wala sio HISANI...

Nchi si ipo vizuri kama anavyosema, mbona hapindishi mishahara ya watumishi..??

Unababaika na midege hiyo ambayo hata procurement yake Bunge haiifahamu?? Ndege ambazo Watanzania hawajui kwani manunuzi yake hayapo wazi??

Grow up Mbwiga..Acha Ushamba wewe.

Kwani nchi hii ni ya watumishi pekee tumechoka nyimbo zenu kila siku, kama vipi acha kazi uje uraiani uonje joto lake
 
Hii "BILI YA VOCHA ZA JERO JERO" ambazo wanahongwa "WAPIGA DEBE WA LUMUMBA" kujiunga MB iliwaje kusifia upuuzi JF, inatoka katika mfuko gani??

Inatoka mfuko wa "CCM" au "SERIKALI KUU KULE HAZINA"???
 
Back
Top Bottom